IPECACUANHA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 3,230
- 1,925
Nimeona majina ya wadaiwa Sugu wa bodi ya mikopo 90% ni wale walioteuliwa na Raisi hili linamuhusu sana sheikh kuliangalia
[emoji2] [emoji2] [emoji2] wanaanza kuleta neno la Mungu[emoji1] [emoji1]mmeanza na ninyi
[emoji2] [emoji2] [emoji2] wanaanza kuleta neno la Mungu[emoji1] [emoji1]
hapa US na mabepari wenzie wakitaka kupora rasilimali zetu hawatapata shida kwa hali hii Mkuunimegundua udini ni "fault line" (ufa) mbaya na wa kutisha katika nchi hii, iwapo huu ufa utalelewa, ama kwa matendo ya viongozi yenye kuuendekeza, adui akija kutugawa ni vigumu sana kusimama kama Taifa moja lililoungana.
ni vyema teuzi zikaakisi demography za Taifa!
nani mnafkiMaisha bila unafiki haiwezekani.
Nani mpuuzi?Acheni upuuzi, anachokisema sheikh ni sahihi kabisa, katika ngazi zote zote za uteuzi hamna usawa,wakristo ndio wengi . Kumbukeni kipindi cha J.K wakristo mlimuandama sana ktk uteuz, maaskofu walikua na taasis za kikristo zilikua zikitoa matamko na vitisho kila kukicha,lakin leo kwakua JPM kafanya ubaguz wa hali wa ya juu ktk uteuzi ,
Acha porojo zako.Unaweza kuwa unaumia sana kwa sababu labda huelewi.
Manung'uniko ni sehemu ya maisha.Huwezi kumridhisha kila mtu.Yaani kwa akili yako unataka uongozi ugawanywe kama zawadi.Wanaolalamika ni wengi kuanzia Ombaomba,Maafa kagera,Wanafunzi,Wakulima,Wafanyakazi mishahara midogo,Daladala,Mipaka ya nchi na nchi mf.Malawi,Matokeo ya Uchaguzi,Wagonjwa n.k.
Kimsingi ni kuangalia malalamiko gani ni ya Msingi na kuyafanyia kazi.
Hili la kupewa vyeo vya upendeleo eti kwa sababu ni waislamu halina maslahi kwa taifa kwa sababu kila kabila nalo litataka lipewe upendeleo.
Mtu anachaguliwa kulingana na uwezo wake si kwa sababu anajua sana kuswalisha au
Idadi ya Waislam na Wakristo Tanzania ni karibu nusu kwa nusu. Kama sheikh yuko sahihi basi Waislam wana kila haki ya kuhoji. Kisingizio cha kuwa eti Waislam hawajasoma labda hilo ni tatizo la miaka ya zamani. Napata shida kuelewa katika teuzi kama rais alikuwa anahakikisha kwamba Wakristo wanapata nafasi nyingi zaidi au ilitokea kwa bahati tu. Lakini pia lazima ikumbukwe kuna vyeo mbalimbali kama wakuu wa mikoa, mawaziri, wakurugenzi wa bodi na wa halmashauri nk. ambao wengi wao ni Wakristo. Maana yake kila alivyokuwa anateuwa watu katika hayo makundi ya vyeo niliyoyataja hapo juu ilikuwa inatokea bahati tu kuwa Wakristo wanakuwa wengi.
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.
Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.
Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.
Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.
Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.
Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.
Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.
Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?
Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.
Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.
Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.
Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
Mawazo yetu ndiyo hayo?Mleta mada akili zako inabid zikapimwe sasa huyo shekhe khalifa kakosea nin? Wakat idad inajionyesha kwamba waislam kiduchu sana kwenye teuzi
mleta mada kang'ata weee, mwishoni akapuliza.Mleta mada acha unafiq.
Mambo mengine bwana watu wanaropokaga ili mradi waonekane wanaongea, kwanza udini sio kigezo cha kuteua mtu kwenye serikali,pili kwan waislam na wakiristo tupo nusu kwa nusu au,mana tungekua nusu kwa nusu angeweza hata kudai hivyo,afu pia sio kila kitu ni cha kulalamika tatizo huyo shekh anachanganya dini na siasa ndo mana wanasababishaga machafuko,kwa sababu hawajui nn wanakitaka kati ya dini na siasaKwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.
Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.
Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.
Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.
Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.
Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.
Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.
Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?
Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.
Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.
Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.
Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
Acheni upuuzi, anachokisema sheikh ni sahihi kabisa, katika ngazi zote zote za uteuzi hamna usawa,wakristo ndio wengi . Kumbukeni kipindi cha J.K wakristo mlimuandama sana ktk uteuz, maaskofu walikua na taasis za kikristo zilikua zikitoa matamko na vitisho kila kukicha,lakin leo kwakua JPM kafanya ubaguz wa hali wa ya juu ktk uteuzi ,
Tangazo liko gazeti mwananchi toleo 5955 LA tarehe 16/11/2016 ukurasa wa 13Ukisoma hayo majina hapo juu waliofadhiliwa kwenda kusomea mafuta na gesi shahada Shahada ya uzamili na kampuni ya BG TZ,Asilimia 100% kati ya kumi ni wakristu,hapa maanake nini mzee wangu Mohamed Said????hakuna waislamu wenye sifa za kupata ufadhili au BG ni sawa na NECTA wanawapendelea wakristu?