Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi. Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza. Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.

Nilichokupendea umeweka mpaka DATA kwenye maelezo yako.

Kama rais Magufuli hana udini , mbona haitokei 70% ya teuzi kuwa ni waislam.

Huyu rais wa sasa anatugawa Kwa udini na ukanda..

Afu anasema tumuombee ili azidi kuleta Udini.
 
Mbona kaongea kwa facts? Nafikiri anayepinga naye alete data hapa..
Sidhani kama Rais huteua watu kwa kuhoji dini zao. Pia kuna ukweli kuwa taasisi za elimu za Kikristo zimekuwa zikijitahidi sana kuendeleza watoto kielimu tofauti na taasisi nyingi za Kiislamu ambazo zimekuwa zikihimiza zaidi elimu ya Madrassa na lugha ya Kiarabu.
 
Huyu shekhe anahitaji kupewa ushauri nasaha kwa upole. Lakini, niseme tu kwamba, manung'uniko yake ni kama ya kina Hellen Kijo Bisimba kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika teuzi za JPM. Kina Hellen wanataka nafasi za uteuzi zigawiwe pasu kwa pasu kati ya wanawake na wanaume. Sasa shekhe anataka nafasi zigawiwe kwa kuzingatia uwiano fulani kati ya makundi mbalimbali ya kidini na kikanda. Naona auanongelea Ukristo dhidi ya Uislam, Umashariki dhidi ya Umagharibi. Amesahau kuongelea ujana dhidi ya uzee, Ukulima dhidi ya Ufanyabiashara, Usomi dhidi ya Kutosoma, na migawanyiko kama hiyo.

Yeye pamoja na kina Bisimba ni watu wa kuelimishwa hivi: Vyeo havigawiwi kwa kuangalia vigezo vinavyohusiana na migawanyiko ambayo haina tija katika ofisi. Kwa mfano, mwalimu wa hesanu anaweza kuwa mwanamke au mwanamume, mkristo au muislamu, mmashariki au mmagharibu, kijana au mzee. Lakini hawezi kuwa mkulima wala mfanya biashara kama ambavyo hawezi kuwa asiye na kisomo. Vigezo vya ujuzi, ustadi, uzoefu na utayari vinahusika. Hivi hoja hii ni ngumu?

Kuna performance indicators in good governance wanatuletea hawa development partners kama vile gender equity, denominational equity, geographical equity, inter generational equity, n.k. Haya mambo tuyakatae kwa hoja kwa kuwa hayana tija. Tukikubali kila kitu tutakuwa kama madodoki.
 
Maneno hayo hayo"mtukufu" kaambiwa na rais mmakonde na sheikh zuber sioni uzushi wowote tena walimwambia uso kwa uso wala si uzushi ni uhalisia ..ingawa binafsi nachukia mambo ya udini.
 
Mh.rais hangalii dini ya mtu anachoangalia ni uwezo wa huyo mtu atafaa sehemu husika atakayopewa kama anafaa atampa hayo majukumu, Halafu sijaona sehemu yoyote kwenye katiba ambayo imesema mh. Ampe mtu nafasi ya kuteuliwa kwa kuangaliaa dini yake.Huyo shekhe atulie taka yake si taka ila taka ya mh.rais ndio taka.Yeye aendelee na majukum yake kama shekhe,Nafasi za kuteua amuchie mheshiwa rais.
 
Mleta mada akili zako inabid zikapimwe sasa huyo shekhe khalifa kakosea nin? Wakat idad inajionyesha kwamba waislam kiduchu sana kwenye teuzi
 
Kwa kweli mbali ya kua muislam, kuna haja ya waislam kuwasomesha watoto wao madrasa na pia shuleni wakasome elimu ya kawaida. La sivyo tutaishia kulalama na kuibua hoja zczo na mantiki. Unakuta watto wanaenda kusoma Qur'an kila siku badili ya kutenga mda wao pia kusoma elimu dunia. Sasa ukimuliza huyo sheikh mtto wake kasoma mpk wapi atakwambia kahifadhi juzuu.

zuu
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi. Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza. Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
 
Huyu shekhe anahitaji kupewa ushauri nasaha kwa upole. Lakini, niseme tu kwamba, manung'uniko yake ni kama ya kina Hellen Kijo Bisimba kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika teuzi za JPM. Kina Hellen wanataka nafasi za uteuzi zigawiwe pasu kwa pasu kati ya wanawake na wanaume. Sasa shekhe anataka nafasi zigawiwe kwa kuzingatia uwiano fulani kati ya makundi mbalimbali ya kidini na kikanda. Naona auanongelea Ukristo dhidi ya Uislam, Umashariki dhidi ya Umagharibi. Amesahau kuongelea ujana dhidi ya uzee, Ukulima dhidi ya Ufanyabiashara, Usomi dhidi ya Kutosoma, na migawanyiko kama hiyo.

Yeye pamoja na kina Bisimba ni watu wa kuelimishwa hivi: Vyeo havigawiwi kwa kuangalia vigezo vinavyohusiana na migawanyiko ambayo haina tija katika ofisi. Kwa mfano, mwalimu wa hesanu anaweza kuwa mwanamke au mwanamume, mkristo au muislamu, mmashariki au mmagharibu, kijana au mzee. Lakini hawezi kuwa mkulima wala mfanya biashara kama ambavyo hawezi kuwa asiye na kisomo. Vigezo vya ujuzi, ustadi, uzoefu na utayari vinahusika. Hivi hoja hii ni ngumu?

Kuna performance indicators in good governance wanatuletea hawa development partners kama vile gender equity, denominational equity, geographical equity, inter generational equity, n.k. Haya mambo tuyakatae kwa hoja kwa kuwa hayana tija. Tukikubali kila kitu tutakuwa kama madodoki.
Mawazo yako mazuri ila tu ya KINAFIKI, Kama unabisha Sio unafiki maelezo hayo yaweke ilipokuwa awamu ya Nne ili ujione ulivyo
 
Mh.rais hangalii dini ya mtu anachoangalia ni uwezo wa huyo mtu atafaa sehemu husika atakayopewa kama anafaa atampa hayo majukumu, Halafu sijaona sehemu yoyote kwenye katiba ambayo imesema mh. Ampe mtu nafasi ya kuteuliwa kwa kuangaliaa dini yake.Huyo shekhe atulie taka yake si taka ila taka ya mh.rais ndio taka.Yeye aendelee na majukum yake kama shekhe,Nafasi za kuteua amuchie mheshiwa rais.
Punguzeni unafiki, Rais akiwa muislam Mbona hamuongeagi hivyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom