Ya Gekul hayajaisha, Wakili Madeleka kukata rufaa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,716
218,263
Kabla hata sherehe za kufurahia Gekul kufutiwa kesi iliyomkabili , ile ya kumtumbukiza Chupa makalioni kijana mmoja huko Manyara haijaanza , Tayari Mawakili wa Mlalamikaji huyo wametangaza kukata rufaa kupinga Uamuzi wa DPP wa kuifuta kesi hiyo.

Tayari nyaraka zimeanza kukusanywa ili kulianzisha upya jambo hilo.
---
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini imeondoa Kesi ya namba 179 ya mwaka 2023 ya shumbulio la mwili iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambapo upande wa Mbunge huyo ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Ephraim Kisanga huku upande wa mlalamikaji Hashimu Ally ikiwakilishwa na mawakili watatu ambao ni Thadei Lista, Peter Madeleka na Joseph Masanja.

Kesi hii kwa mara ya kwanza imesikilizwa hii Leo katika mahakama ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara na Hakimu wa mahakama hiyo Victor Kimario ambapo amesema kesi hiyo imeondolewa kwa mujibu wa sheria namba 91 kifungu kidogo cha( 1) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura namba 20 Kama ilivyorekebishwa mwaka 2022, ambayo inampa mkurugenzi wa mashitka mamlaka ya kuondoa kesi yeyote ya jinai mahakamani kabla haijafikia hukumu.

Kwa upande wa Mawakili wa mlalamikaji wameelezwa kutokuridhishwa na kitendo kilicho endelea mahakamani hususani kufutwa kwa kesi hiyo na wameeleza kukata rufaa.

Pia soma

Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis

Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

Nani anamlinda Gekul? DPP asema hana mpango wa kuendelea na kesi
 
Kabla hata sherehe za kufurahia Gekul kufutiwa kesi iliyomkabili , ile ya kumtumbukiza Chupa makalioni kijana mmoja huko Manyara haijaanza , Tayari Mawakili wa Mlalamikaji huyo wametangaza kukata rufaa kupinga Uamuzi wa DPP wa kuifuta kesi hiyo .

Tayari nyaraka zimeanza kukusanywa ili kulianzisha upya jambo hilo .

View attachment 2854740
Tukutane barabarani wapenda haki wote!
 
Kabla hata sherehe za kufurahia Gekul kufutiwa kesi iliyomkabili , ile ya kumtumbukiza Chupa makalioni kijana mmoja huko Manyara haijaanza , Tayari Mawakili wa Mlalamikaji huyo wametangaza kukata rufaa kupinga Uamuzi wa DPP wa kuifuta kesi hiyo.

Tayari nyaraka zimeanza kukusanywa ili kulianzisha upya jambo hilo.
---
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini imeondoa Kesi ya namba 179 ya mwaka 2023 ya shumbulio la mwili iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambapo upande wa Mbunge huyo ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Ephraim Kisanga huku upande wa mlalamikaji Hashimu Ally ikiwakilishwa na mawakili watatu ambao ni Thadei Lista,Peter Madeleka na Joseph Masanja.

Kesi hii kwa mara ya kwanza imesikilizwa hii Leo katika mahakama ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara na Hakimu wa mahakama hiyo Victor Kimario ambapo amesema kesi hiyo imeondolewa kwa mujibu wa sheria namba 91 kifungu kidogo cha( 1) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura namba 20 Kama ilivyorekebishwa mwaka 2022, ambayo inampa mkurugenzi wa mashitka mamlaka ya kuondoa kesi yeyote ya jinai mahakamani kabla haijafikia hukumu.

Kwa upande wa Mawakili wa mlalamikaji wameelezwa kutokuridhishwa na kitendo kilicho endelea mahakamani hususani kufutwa kwa kesi hiyo na wameeleza kukata rufaa.
Duh...!, hawa watakuwa ni mawakili wa ajabu sana!, uamuzi wa DPP kwenye Nolle hauhojiwi na yeyote hata rais wa JMT!, sasa hiyo rufaa uta file kwa merits gani?.

The best way forward ni
1. Kufungua Private Prosecution
2. Kufungua Civil case ya criminal trespass
P
 
Duh...!, hawa watakuwa ni mawakili wa ajabu sana!, uamuzi wa DPP kwenye Nolle hauhojiwi na yeyote hata rais wa JMT!, sasa hiyo rufaa uta file kwa merits gani?.

P

..hata ktk mazingira ambayo uamuzi wa "nolle" unaelekea kudhulumu haki za watu?

..kwamba DPP anaruhusiwa kufanya anavyotaka ktk shauri lolote na hakuna wa kumhoji?

..sidhani kama waandishi wa sheria zetu walilenga kumpa Dpp mamlaka hata ya kuvunja haki kwa kutumia " nolle. "
 
Back
Top Bottom