Shairi la Leo........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi la Leo...........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by CAMARADERIE, Aug 30, 2011.

 1. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Fikiri zako fikira, ufikiri kila tendo,
  Fikiri lilo na dhara, ufikiri na Ia pendo,
  Fikiri lilo tohara, ufikiri na uvundo,
  Fikiri fikiri tendo, Ia amani na busara.

  Fikiri sana dunia, ina mzuri mdundo,
  Fikiri sana yalia, ina mzuri mshindo,
  Fikiri mwisho sikia, unapasuka msondo,
  Fikiri fikiri tendo, Ia amani na busara.

  Fikiri ndugu dahari, dunia ina mikondo,
  Fikiri hizi habari, ni kushuka na mipando,
  Fikiri dunia pori, chaka Ia uwi na kondo,
  Fikiri fikiri tendo, la amani na busara.

  Fikiri dau muundi, muunda dau muundo,
  Fikiri lende kilindi, daule likaze mwendo,
  Fikiri dau halendi, nguvu za dau upondo,

  Fikiri ninakariri, usiwe mwenye mfundo,
  Fikiri tena fikiri, kila ovu liwe kando,
  Fikiri mno hatari, ukiwa na mbovu nyendo,
  Fikiri fikiri tendo, Ia amani na busara.
   
 2. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hongera sana
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Kofia nakuvulia, Camaraderie hima,
  Ushairi metulia, Nakupatia heshima,
  Vina umevipatia, Pia nayo mizania
  Hakika nimefikiri, kabla sijakupongeza.

  Narudi kitandani, kufikiri kwa kina.
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mapenzi yana ran dunia!! Shairi linaran wap cjui!!!
   
 5. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Fesi buku umkweli, mapenzi yanaraha duniani.
  Shairi sio kubeli, rahayake ipo kichwani.
  Tusi lete ufedhuli, tuyasomapo gazetini.
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Shahiri limeeleweka hasa kwa wenye akili timamu,
  Endelea kutujuza hasa kwa yale mema.
   
 7. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  umeongezea verse?
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ok na mm nna shairi languushikwapo shkamana kilichoko mfukoni mwako ndio chako, usipigie hesabu cha mwenzako!!!!
   
 9. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Camarade wa Luthuli,siyo yule wa kimango ,
  Usia ka warasuli,umefikia viwango,
  Sije leta ufedhuli,wakaharibu mpango,
  Ulonena ninakili,yamesheheni mafunzo
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Hongera zako,limekaa vizuri.
   
 11. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mashallah! Shairi dhuri! nimelipendaaaa!
   
 12. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Fikiri lililo mbele , la nyuma liweke kando
  Fikiri usiwe msukule, utakosa kaa na gando
  Fikiri acha kelele , kimya kimya uwe mwendo
  Fikiri hili na lile , uziepuke skendo

  Fikiri utafakari , dunia tambara bovu
  Fikiri utahadhari, usije acha makovu
  Fikiri kwa Indhari, uache wako utovu
  Fikiri usitahayari , epukana na uchovu

  Fikiria familia , yako ilokuzunguka
  Fikiria daharia, zinavyokupukutika
  Fikiria usijelia , usije ukaumbuka
  Fikiria zingatia, maisha yalivyochafuka

  Fikiria wenye njaa, kama wewe ushatoka
  Fikiria wanaotambaa, kama waweza kuruka
  Fikiria walivyozagaa , mayatima walochoka
  Fikiria kila saa, ni wapi uliposhika?
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Hahahaha.......Fellow tablet katika kufikiri na kutafakari.......ngoja niendelee kumla mbuzi wa iddi kwanza.
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa,
  Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa,
  Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa,
  Toka kama mlizamu, funika palipozibwa,
  Titile mama litamu ,Jingine halishi hamu.

  Lugha yangu ya utoto,hata sasa nimekua,
  Tangu ulimi mzito,sasa kusema najua,
  Ni sawa na manukato,moyoni mwangu na pua,
  Pori bahari na mto,napita nikitumia,
  Titile mama litamu,jingine halishi hamu.
   
 15. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Fikiri ukila mbuzi, nyunyiza na pilipili
  Fikiri wake mchuzi, ndimu weka ya ukali
  Fikiri simtie nazi , itaharibu misuli
  Fikiri akigoma mbuzi, itumie four wheeli
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Namba nawe mlimwengu, pulikiza matamko
  Nikweleze neno langu, uzinduwe bongo lako
  Nayo nda M'ngu si yangu, na ayani haya yako
  Uwatapo haki yako, utaingiya motoni

  Simama uitete, usivikhofu vituko
  Aliyo nayo mwendee, akupe kilicho chako
  Akipinga mlemee, mwandame kulla endako
  Uwatapo haki yako, utaingiya motoni

  Amkani mulolala,na wenye sikio koko
  Isiwe mato kulola,natutizame twendako
  Tuwate na kuduwala,usingizi si mashiko
  Uwatapo haki yako,utaingiya motoni

  Teteya kwa kula hali, usiche misukosuko
  Siche wingi wala mali,sabilisha roho yako
  Unyonge usikubali, ukaonewa kwa chako
  Uwatapo haki yako, utaingiya motoni

  Siche kifaru na ndovu, wangazidi nguvu zako
  Wapempe kwa uwekevu, unusuru haki yako
  Siandame wapumbavu,kilicho chako ni chako
  Uwatapo haki yako, utaingiya motoni

  Cha mtu hakifitiki,kikafungiwa kiliko
  Huzuka kikawa hiki,kazana utwae chako
  Uwatapo yako haki,fahamu ni dhara kwako
  Leo na kwa Mola wako,utaingiya motoni

  Fumbuwa unyang'arize, uone duniya yako
  Bure sijiangamize,kuangalia wendako
  Utatupa upoteze,wende ambapo si pako
  Uwatapo haki yako,utaingiya motoni

  Kadhalika nako pia,huko ambako sikwako
  Huwezi kujitetea,wala huwi na mashiko
  Basi iwaze duniya,kwani ya kale hayako
  Uwatapo haki yako ,utaingiya motoni

  Kadi tamati shairi,sitii la ongezeko
  Mwanati iwa tayari, utete haki yako
  Unyonge usiukiri,Jifunge ufe kwa chako
  Uwatapo haki yako, utaingiya motoni
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Fikiri hii dunia, ni wapi ilipotoka
  Fikiri na jinsia, kisa cha kutenganika
  Fikiri viumbe pia, vile walivyoumbika
  Fikiri jee ngamia, nundule lahitajika?

  Fikiri na macho yake, yenye vizibo viwili
  Fikiri na mwili wake, kiu kustahamili
  Fikiri na kwato zake, moto wa jangwa himili
  Fikiri muumba wake, muweza wa kila hili

  Fikiri nae farasi, aendae akipuma
  Fikiri na yake kasi, nguvuze zenye kuvuma
  Fikiri na ufanisi, pale unapo mtuma
  Fikiri jitanafasi, jisogeze kwenye mema
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Tulikuwa tunapewa dozi hizi mashuleni........na Malenga wetu RTD!.......yule jamaa sijui kaishia wapi aliyekuwa akitusomea mashairi redioni
   
 19. data

  data JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,795
  Likes Received: 6,573
  Trophy Points: 280
  Tafuta mistari mizuri ya kumsifu JAKAYA
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
Loading...