Mwlmgomaji
Member
- Aug 3, 2012
- 93
- 6
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MTIHANI WA UCHAGUZI- 2015
Muda: saa 3000;MTIHANI WA UCHAGUZI- 2015
Taratibu na Maelekezo:
1. Jibu maswali yote kwa ufasaha zaidi bila kujali itikadi ya chama ulichopo au ukipendacho au ukichukiacho.
2. Kuwa mkweli na mtenda haki daima kwenye ujibuji wako.
3. Usiweke ushabiki wa vyama mbele lenga uwezo wako wa kufikiri sio nadharia.
4. Toa ukweli na onesha wazi ulivyoguswa na Maswali haya chini.
Maswali:
1. Tanzania ni nchi ambayo ina mfumo wa vyama vingi vya Kisiasa na vingine vikiendelea kuanzishwa kwa siku za usoni, Je unadhani mfumo huu unafuatwa ipasavyo ndani ya mipaka ya Tanzania kama nchi zingine? Kama Jibu ni ndio, Toa HOJA zako. Na kama jibu ni HAPANA toa maelezo ya kina katika Jibu lako.
2. Ni kweli Demokrasia ya Tanzania imekua kwa kasi ya Ajabu kama inavyoripotiwa na mataifa mengine na baadhi ya viongozi wazoefu na wakomavu katika Siasa? Toa maelezo ya kina katika jibu lako.
3. "Kuwepo kwa vugu vugu kubwa la kisiasa Nchini Tanzania na kuwafanya Watanzania wote kuamka Kisiasa mwaka huu na miaka minglne iliyotangulia ni kutokana na Juhudi za ELIMU bora au MAISHA bora kwa KILA MTANZANIA ama UMASKINI uliotukithiri AKILINI, MWILINI HADI KWENYE LIMI au UGUMU WA MAISHA KWA KILA MWANANCHI". Eelezea usemi huu je UNATIJA gani kwa TAIFA letu KUKOMBOKA na TABAKA la UMASKINI.
4. Ni kwell uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti na chaguzi zingine zilizowahi kufanyika huko nyuma na uwepo wa repot mbali mbali za wasomi kuwa utawahusisha wananchi wailiowengi mamilioni kwa mamilioni wa MJINI na VIJIJINI. Je unadhani au kuhisi MABADILIKO ya KWELI KWA WATANZANIA yataletwa na CHAMA KONGWE au CHAMA CHENYE MUUNGANIKO wa VYAMA VINGINE au CHAMA cha WATANZANIA wenyewe. Elezea kwa kina kwa mifano dhahiri.
5. Kuendelea kuchafuana MAJUKWANI na TUHUMA zisizo kuwa na RIPOTI maalumu au maelezo yoyote kutoka katika vyombo vyenye dhamana vya dola vinavyohusika na KUWAJIBISHA viongozi JE? Ni kweli upotoshaji huu unamnfaisha nani katika TAIFA la watu walio MASKINI kama SISI? Je SHERIA zipo wapi mpaka TUHUMA zihararishwe na kuwa ndo HUKUMU. Kwanini waliowachache wanapotosha waliowengi kwa kutotoa uwelekeo maulum na nini kifanyike katika kufungua mashtaka na kama KUNA UPOTOSHAJI ndani yake na ALAUMIWE kwa upotoshaji huu?
6. UFISADI ni hali ya mtu au kundi la watu fulani kudhamiria au kuhusishwa au kushinikizwa kufanya jambo fulani baya au kuhujumu uchumi wa Taifa kiujumla kunyima maendeleo fulani kutimia na kujinufaisha binafsi ili kupisha uooo.zo kuendelea kufanyika ndani ya serikali fulani hususani TAIFA changa kama TANZANIA. Je, katika ORODHA ya MAFISADI ni mmoja tu katika nchi hii ambae anaendelea kuchafuriwa? Na kama wako wengi zaidi kwanini wasichafuliwe wote na ujulikane uooo.zo wa TAIFA letu kwa DUNIA ya SASA. Na kama tuna wachafua wachache na ni kwa FAIDA ya nani?
7. TANZANIA katika siasa tuna jikita zaidi na KUSEMANA, KUCHAFUANA, KUDHARIRISHANA, KUHARIBIANA JINA, KUJISHUSHIA HESHIMA TULIZONAZO KWA JAMII. Je kwa Uwezo wako wa UFIKIRI unadhani kuna HAJA ya ELIMU ya UONGOZI kutolewa kwa kila MGOMBEA kwa KITI chake husika?
8. Heshima ya MTU awe MSANII,ASKARI,MAPADRI, MASHEHE, MWANAJESHI, MWALIMU, DAKTARI, MWANDISHI wa HABARI, ambae sio MWANASIASA na SIO MFUASI wa chama chochote cha siasa akiwa KAZINI pake ni VYEMA akajihusisha na SIASA ya SASA au IJAYO katika mahali pa KAZI? Je utoaji wa MAUDHUI yake kwa Jamii ya sasa itakuwa inayofuata misingi ya HAKI na USAWA kwa JAMII nzima au Itakuwa ya UCHOCHEZI, UPENDELEO, UPOTOSHAJI kwa UMMA kwa kipindi Hiki cha Mpito wa KISIASA? Na BAADA ya siasa hizi tutakuwa na MTAZAMO gani juu ya HAWA WATU WENYEHESHIMA NZITO kwa JAMII hii?
9. UPENDO, AMANI, UMOJA, USHIKAMANO, UZALENDO, UTII WA SHERIA, KUTOMILIKI SILAHA NZITO, Je kwa UPEPO huu wasiasa za LEO unaweza KUDHOHOFISHA haya yote MWAKA HUU na kuendelea kujuta miakia yote ijayo kama majirani zetu wanavyopata pigo hili? JE nini KIFANYIKE kabla ya WAKATI mambo yakipanganyuka?
10. TANZANIA ni mali ya chama kimoja tu cha siasa? Au ni mali ya wanachama wa vyama vyote vya KISIASA, je kwani katika MIADHARA na MAHALI popote yafanyikayo MIHADHARA ya KIDINI kwani watanzania wa DINI zote si huwa wanakuwepo? Sasa swall langu, KUKATALIWA, KUKUBALIWA, KUWAAMURU wenye sifa za KUPIGA kura KUHUDHURIA mikutano au mkutano fulani wa chama fulani cha SIASA ni UMAKINI WETU, AKILI ZETU ZA KUZALIWA, UTAIRA WETU WA KUTO FIKIRI, UPOTOSHAJI KWA JAMII, AU NI UBABE wA KISHERIA, UZEE WETU WA KISIASA. UFINYU WA UFIKIRI TULIO NAO. AU NI MIANYA YA RUSHWA? Toa maelzo ya kina.
11. Kuendelea KUJITOKEZA kwa watu kama mheshimiwa. SLOW SLOW na Dk. Silahaa. KUELIMISHA umma juu ya MUOVU mmoja katika jamii yetu, Je kuna DHANA YA UPOTOSHAJI, UKWELI DHABITI, UBABAISHAJI WA SIASA, UKOMAVU WA KISIASA, RUSHWA KUSHAMIRI baina yao KULENGA upande mmoja wa shillingi na KUNUFAISHA walio wachache na kupoteza dira ya WALIOWENGI(WATANZANIA).AU NDO UBABE WA KISIASA za SASA.
12. Kuendelea kutoa SHERIA kandamizi kwa WATANZANIA kwa kipindi HIKI cha UCHAGUZI na KUONGEZA NGUVU kubwa ya SHERIA ichukue MKONDO wake kwa wale watakao kiuka sheria. JE? kuna misingi yoyote ya kivyama kuingilia UTENDAJI mkubwa wa VYOMBO vya SERIKALI kama MAHAKAMA, TCRA, NEC?
13. Elezea vyombo vya HABARI jinsi vinavyojihusisha na KIASA kwa namna moja ama nyingine katika utangazaji we wa kill siku, Au VIKWAZO wavipatavyo katika chute TAARIFA sahihi na nini maoni yako juu ya HILI. Je kuna USAWA? HAKI? UMAKINI? BUSARA? Katika MAADILI ya utangazaji wa HABARI kwa kipindi hiki cha UCHAGUZI?
14. Je, kupanda kwa bei za BIDHAA mbali mbali, Huduma za gharama kuongezeka na kupungua katika mitandao, umeme kwa mwaka huu wa SIASA za USHINDANI na Mfumuko wa bei ya vitu, Kuipa nafasi zaidi Dollar ya US ni vyema kabisa serikali yetu imeingia kwenye vugu vugu la KISIASA na kuwasahau wananchi wake wakiteseka kaputa huduma stahiki kwa maisha yao ya kila siku? IKiwemo na KUKATIKA kwa UMEME, HUDUMA za AFYA, na hoodlum zingine
nayo yamekaa KISIASA?
15. Uwepo wa kauli kama hizi MAJUKWAANI "Ushindi ni lazima" "Ushindi ni asubuhi na Mapema" "CCM chali" "Tutashinda kwa GHARAMA yeyote ile" "Hata kwa goli la mkono tutashinda tu" hizi na zingine zina MAANA gani au kuashiria kitu gani ambacho kwa siasa za sasa, Kwa upepo huu kuna maana Gani? AU ni HAMSHA HAMSHA na kauri mbiu za wagombea wa vyama husika?
16. USHAURI wako kwa chama kinachotawala sasa KUFANYA MICHAKATO YA AMANI katika uchaguzi, Kusiwe na Matumizi ya SILAHA za MOTO dhidi ya wananchi waandamanaji, MABOMU kama ya MBAGALA na mengineyo.
17. USHAURI wako juu ya vyama vingine vya siasa visitumie NGUVU kubwa kupigana na DOLA kwa mawe au silaha kali endapo mambo yakiwa OVYO(HATUOMBEI IWE HIVI) watumie amani na SHERIA katika MAHAKAMA HURU kudai HAKI zao vyema. NA KUWE NA UHURU WA HABARI KUTOA TAARIFA.
18. USHAURI wako kwa chama KITAKACHO SHINDWA KUSHIKA DOLA TENA, AU KUSHINDWA NA KINGINE KWA KURA HALALI au KWA WIZI au UJANJA wa KIUZOEFU
MWISHO: CHAGUA CHAMA CHENYE MISINGI BORA YA FIKRA NA MAONO na SIO CHENYE MISINGI BORA YA NADHARIA NA MBWEMBWE za RANGI, MAANDISHI au MAVAZI YA KILA AINA.
"KIJANA SIO MZEE, KIJANA NDIYE MWENYE KULIJENGA TAIFA LAKE, MZEE ATALINDWA NA KIJANA WAKE DAIMA KWANI YEYE ALIULINDA UTOTO WAKE WAKATI WA UJANANI WAKE. KAMA WEWE NI KIJANA AMKA SASA TAIFA HALIKUSUBIRI TUMIA FIKRA KUFIKIRI, AKILI KUPEMBUA, TANZANIA SIO MALI YA CHAMA KIMOJA, ZINDUKA SASA USISUBIRI KUAMSHWA WAKATI "GEAR IMEBADILISHWA ANGANI MDA...""