Ndugu zangu,
Anasema hayo Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre; kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.
Kwenye hili la Bunge lijalo la Katiba, JK akiwa Mbeya alisisitiza umuhimu wa majadiliano. Na kwamba kwenye siasa nguvu ya hoja ndiyo yenye kushinda na wala si hoja za nguvu. Kwamba kwenye siasa hakuna kupigana bali kushindana kwa hoja. Nakubaliana na JK, na hata Freeman Mbowe, kwa alivyokaririwa na media, naye ameonyesha kukubali umuhimu wa mazungumzo badala ya matumizi ya nguvu.
Na hakika, kwenye hili la Katiba, tunapofikiri kugombana kwa kupigana kwa ngumi na kuumizana,na kwa misingi ya tofauti za rangi za vyama, maana itikadi zinaonekana zimo chumba cha mahututi, basi, huko ni sawa na kukubali kuzipumzisha akili zetu. Kwamba tumechoka kufikiri. Na kwamba tumekuwa wabinafsi mno. Hatufikiri kuhusu nchi yetu tuliyozaliwa na hatma yake. Tunajifikiria sisi , makundi na vyama vyetu. Vyote vya kupita, wakati nchi itabaki.
Maana, kutengeneza Katiba ya nchi ni sawa na kulima shamba la pamoja. Na kwanini basi wenye kulima shamba moja wagombanie majembe? Hakika, huo utakuwa ni uwendawazimu, ni kwa vile, watakachopanda na kuvuna ni cha faida yao wote.
Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufikiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana, ng'ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.
Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kufikiri.
Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake, wanaume, na hata kivuli cha mti.
Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazamana juani.
Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.
Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si kuhamasisha vurugu au mapigano.
Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, na panakosekana mazungumzo, ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani.
Na kama alivyosema Shaaban Robert, kuwa watu wa Nchi ya Kusadikika, huwa na desturi ya ajabu sana. Desturi ya kuitafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio