Mkuu Kiswila ukitaka kusema uongo jitahidi kuuelewa hata wewe huo uongo. Fastjet anadiawa au ana deni la USD 200 milioni. Faida yake iko wapi? Pamoja na ukweli kuwa comments za hapa sio za kitaalamu bali siasa naona nichangie kidogo kuwapa mwanga maana ndege na biashara yake naijua, kidogo!. CEO wa ATCL kakwepa asubuhihii akiwa TBC1 kuhusu gharama aliyosema Waziri na kudai hilo ni swala la uendeshaji, kwa maana halisi, amejitenga na maneno na takwimu za Waziri. Hata hivyo katoa shule ambayo inauhalisia wa nini kinafanyika. Kasema sio matengenezo ya ubovu bali uchunguzi na matengenezo yaliyopangwa (scheduled maintenance au check C kwa kitaalamu) baada ya ndege kufikisha masaa 4,000 ya kuruka. Miaka miwili kwa ndege zinazofanya kazi kama inavyotakiwa ni muda tosha na huenda zikawa zimechelewa kufikisha masaa hayo kutokana na kutotumika sana. Ukichukua wastani wa masaa 12 ya kuruka kwa siku, ingewachukua ATCL mwaka mmoja tu kufikisha masaa 4,000. Kwa mwenye uelewa wa maswala ya ndege hili la masaa lina uhalisia ukiacha wapiga porojo wa JF ambao hutafuta ncha ya kushika na kuifanya issue hata kama ni butu. Tatizo lililopo, kwa uelewa nilionao, ni hiyo hesabu aliyotoa huyo Mh Waziri. Nafikiri ni siasa bila kujua madhara yake ili aonakane kasema na kuonyesha pesa ipo. Kwa uzoefu wangu Check C inaweza kufanyika hapa Tanzania na kama itabidi iende nje basi Addis Ababa ndio rahisi zaidi na siyo Canada kama huyu Mheshimiwa anavyojitapa. Hajui hata gharama za hayo matengenezo zinatokana na nini. Kuipeleka ndege Canada ni kuongeza gharama zisizo za lazima maana utahitajika kulipia mafuta, vibali vya kuruka katika anga ya nchi unazopita na kutua, na gharama ya crew (marubani na mafundi). Kama ndege zitafanyiwa matengenezo hapa Tanzania, nina hakika kwa ndege moja haitazidi USD 135,000 karibu shilingi 300,000,000. Magufuli bado yuko sahihi kununua ndege aangalie tu nidhamu ya utendaji hasa ya wanasiasa nje ya ATCL ambao watatafuta kiki kwa kujifanya wanajua kumbe wanaharibu! Wawaachie ATCL ambao wameonyesha uwezo mkubwa wafanyekazi yao bila wkuingiliwa na wanasiasa.
Ndege zinaendeshwa kwa Ruzuku kila mwaka Fastjet kila mwaka walikua wakitengeza faida na bei zao ziko chini sana zinashindana na mabasi ATCL, pamoja na kubaki wenyewe, Fastjet kunyimwa vibali nakubaki wenyewe bado wanaomba Ruzuku Serekalini Watanzania tusikubali kufuka jini ATCL ni jini,Watu wanaziogopa kuzipanda Kitwanga ali hoji ubora wa hizo ndege wakampuuza na kumuita mlevi akiwa wazi na mwana ccm, #2020 Lissu # tuzipige mnada zote tujenge shule na miundombinu mbali mbali nchini