Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Ndege kawaida uwa zinafanyiwa checks au services. Kuna Check A yaani night check, ndege inapokuwa imesafori siku nzima, kuna Check B, hii ufnywa baada ya muda fulani yaani kuanzia masaa 160-180 na inatakiwa ikamilike katika siku moja mpaka tatu kwenye hanga za uwanja wa ndege. Tatu kuna check C hii ni mandatory kwa ajili ya airworthiness kulingana na CAA nayo ufanywa na ndani ya miezi 20-24. Hii ufanya large majority of the aircraft's components. Zamani ikifanyika kwenye Hanga za Dar Airport na KIMAFA ilikuwa imejengwa kwa ajili hiyo lakini serikali ya Mkapa ilihujumu kitengo hicho ikiwa ni pamoja na KADCO. Na nahisi kwa sababu ya hujuma hiyo ndiyo maana ndege zetu zipelekwe Canada.
Nne kuna Check D- This is performed approximately every 400-600 flight hours or 200–300 cycles (takeoff and landing is considered an aircraft "cycle"), depending on aircraft type. It needs about 50-70 man-hours and is usually on the ground in a hangar for a minimum of 10 hours.
Nimetoa maelezo hayo ili watu wasije kufikiri ndege inapelekwa uko kwa ajiri ya ubovu bali ni mandatory. Ndege siyo kama bus au roli kwamba unaendesha mpaka iharibike ndio upeleke garaji. Ndege inachekiwa kila baada ya masaa yaliyokubaliwa
sawa mkuu maelezo mazuri....
 
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).


WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.


“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.


Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.


Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.


“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.


Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.




Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.


Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.


Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.


Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.


Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
haya twende kazi mzee wa kukurupuka.....katuzolea used mbayaaaaaa
 
Kukarabati ndege ni jambo la kawaida. Ila hapa ndipo tutapojifunza kuwa biashara ya ndege ni zaidi ya kununua tu ndege lukuki.

Na ndiyo maana mashirika mengi huwa hata ndege zao ni za kukodisha, eg south africa airways. Kazi ya kampuni ya ndege inatakiwa iwe ku-manage routes zenye faida na kuhakikisha ndege zinakuwa angani zikiwa zimejaa abiria kila wakati. Najua wengi hamtaelewa mpaka muone.
Ndio maana kampuni za simu pia hazimiliki minara. Kampuni ina concentrate on core competency -wateja.
 
Someni kilichomo ndani msisome heading na kuanza kukosoa au kupongeza, don’t judge the book from its cover neither should you judge the content from its heading, you have to read the whole story and find the facts there in stipulated
mkuu kilichomo ndani kimepakwa pakwa mafuta tu lakini ukweli ndio huo, tulichagua koroma.

hiyo gharama ya matengenezo imezidi income iliyotokana na ndege hizo, hata hivyo bado ni mapema mno.
 
Ndege zina services schedule zake kila baada ya miaka kadhaa (ni vitu ambavyo avikwepeki) ndio maana unawasikia wakipiga kelele kufufua hangar la Arusha kupunguza hizo gharama za kupeleka ndege Canada.
Kia ni Arusha?
Huwa mnasomaje habari, usipoongeza chumvi huoni raha.
 
Baada ya mafanikio makubwa kwenye Uchumi wa Viwanda..
Sasa tupo kwenye Uchumi wa Ndege..
Ni kununua Ndege nyingi kadiri iwezekanavyo..
Ndege zinalipa sana.
Pesa zote walizopata bilion 13 sasa zinaenda Canada kukarabati ndege ni vigumu ATCL kupiga hatua kwani ufujaji wa pesa kupitia 10% upo pale pale
 
Back
Top Bottom