Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

i anaombwa yeye binafsi badala ya kutumia michakato ya kisheria siyo
Mchakato wa kishheria ni upi? Hivi nyie mnalipwa kuwa wajinga? Mchakato wa kisheria ndio huo wa kila fungu la matumizi ya pesa za umma kupewa kibali na Mkuu wa nchi na serikali. Ninyi wana-Ufipa mnataka mchakato gani?
 
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.

“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.

Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.

Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.

“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.

Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.

Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.

Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.

Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.

Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.

Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
Duh!! JUZI tu? Zishaharibika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmawia ndege inayozungumziwa hapa si bombedier Q400, bali ni Q300 ambayo ilikuwepo sikunyingi sana.. sema ilikwa mbovu.
Zinazokarabatiwa ni Q300 na moja ambayo rais ametoa amri ipelekwe atcl kufanya kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hebu soma kipande hiki cha gazeti acha kupotosha watu
IMG_0619.JPG
 
Ndege zina services schedule zake kila baada ya miaka kadhaa (ni vitu ambavyo avikwepeki) ndio maana unawasikia wakipiga kelele kufufua hangar la Arusha kupunguza hizo gharama za kupeleka ndege Canada.
Wanategemea gari umeinunua miaka miwili unaibuluza tu road..! ile Hangar iko Kilimanjaro
 
weka maelezo, hizi za juzi tu zimeshaharibka? Makopo haya yalikuwa mitumba kama ni hivyo!

Watu kama wewe ndiyo wanapendwa na kina Zitto na Lissu humu mitandaoni na kwenye makongamano yao huko mikoani. Mkuu inakuwaje unaweka akili zako kando, ulitaka ndege zisifanyiwe service au ulifikiri ndege hazifanyiwi service?
 
Haina uwezo wa kufanyia Service ndege hizo ndio maana zinapelekwa Canada. Kwa maana nyingine hatuna wataalamu wa kuzihudumia hizo ndege.
Wataalam wapo. Mbona precision air inao wataalam wake... na wengi ni watanzania?
Ni hiv tatizo hakuna karakana kubwa ambazo zinaweza kubeba hizo ndege.
Wataalam wapo.. karakana zilizopo ni ndogo na hazina uwez wa kuingiza hizo ndege

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu humu kuna mazuzu wengi
Waziri alipewa taarifa kama mwezi ujao hizi bombadier mbili zinatakiwa kufanyiwa service kwa ghalama ya bilion 13,
Waziri akampelekea Taarifa mh Rais
Rais pamoja na waziri wamekubaliana ndege zitatengenezwa Arusha
Rais amekubali kutoa pesa kwa ajili ya kukarabati karakana yetu pale arusha ili ndege zetu zitengenezwe pale arusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yatakiwa CAG atembee hapo juu ya usalama wa kodi zetu,tuliambiwa kitu kipya ndani ya Miaka 2 service tena,imeingiza faida bei gani.Ni sahihi kumiliki kitu ambacho ni mzigo lengo kumfurahisha mwanasiasa Kwa gharama za kodi zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Good thinking nimelipenda hili neno ''usalama wa kodi zetu'' hapa wachache wanafaidi keki ya Taifa
 
Hawa jamaa wa awamu ya tano ni vilaza kweli kweli..!!
Eti rais ndo anatoa fedha utafikiri ni zake..??
Bunge liko wapi?
Na supika akiambiwa bunge lake ni dhaifu anatoka mapovu debe!

Wakati nchini Marekani mabunge yao yana nguvu ya kuinyoosha serikali na kiongozi wake yeyote anayeenda kinyume na matakwa ya taifa lao.. Sisi huku mtu mmoja nakuwa ni kama mungu na shetani kwa wakati mmoja...
Eti "Busara zake" ndo mustakabali wa taifa..!

Nadhani wakati wengine tayari wanaitwa binadamu... watu wengine wako kwenye mchakato wa kuitwa binadamu..!!
Wenye akili ndogo pengine wasinielewe... Ijulikane kuwa binadamu ana nguvu kubwa na akili nyingi za kujikwamua kutoka kwenye mgando wa mawazo na changamoto za kimfumo!!
 
Ndege zinaendeshwa kwa Ruzuku kila mwaka Fastjet kila mwaka walikua wakitengeza faida na bei zao ziko chini sana zinashindana na mabasi ATCL, pamoja na kubaki wenyewe, Fastjet kunyimwa vibali nakubaki wenyewe bado wanaomba Ruzuku Serekalini Watanzania tusikubali kufuka jini ATCL ni jini,Watu wanaziogopa kuzipanda Kitwanga ali hoji ubora wa hizo ndege wakampuuza na kumuita mlevi akiwa wazi na mwana ccm, #2020 Lissu # tuzipige mnada zote tujenge shule na miundombinu mbali mbali nchini
 
Hawa jamaa wa awamu ya tano ni vilaza kweli kweli..!!
Eti rais ndo anatoa fedha utafikiri ni zake..??
Bunge liko wapi?
Na supika akiambiwa bunge lake ni dhaifu anatoka mapovu debe!
''Things are going out of hands'' Wengi walisema Bunge ni kibogoyo waliweka pamba masikioni mengi tuna yaona ila kwa ubabe uliopo watu wanasema bora liende ''vyeo ni dhamana watapindisha sheria kwasasa kukidhi mahitaji yao lakini baadae yataondolewa tu! ''time will tell''
 
Watu kama wewe ndiyo wanapendwa na kina Zitto na Lissu humu mitandaoni na kwenye makongamano yao huko mikoani. Mkuu inakuwaje unaweka akili zako kando, ulitaka ndege zisifanyiwe service au ulifikiri ndege hazifanyiwi service?
sasa mkuu ukarabati kwa ndege iliyokuja juzi tu ! Duh !
 
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.

“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.

Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.

Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.

“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.

Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.

Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.

Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.

Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.

Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.

Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
Swali fikirishi je hizo ndege zimeingiza zaidi ya sh.Bilioni 13.9
 
Back
Top Bottom