Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Sidhani kama uliyemjibu amesema ni boeing. Lipind cha mkapa atcl (wakati huo ikiitwa atc) . Iliwahi kununua bombadier Q300. Na hii ndio ndege pekee atcl walikuwa nayo.. iliharibika na kupelekwa kwenye hanger.
Hizi mpya ni Q400.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu uko sahihi kama Wikipedia inavyozungumzia historia ya Bombardier Q300 na Q400 kwa ATCL, Kuna wakati nilisikia kuwa moja ya ndege mpya ilipata majanga ikiwa Mwanza au ndio hiyo wanayozungumzia hapa?
 
Kumbe service za ndege ni ghali sana. Inabidii Atcl wapambane sana ili waweze kupata faida kubwa kufidia hizo gharama.

Mkuu umenena, muhimu kuja na Mpango kabambe, ndani ya saa 4,000 wanapata nn?
Kuweza manage hizo costs za services?

Bado zile nyingine, hatujui ni Baada saa ngp?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,
Ndege ni hasara tupu,

Nisawa na Mtumishi wa Serikali mwenye mshahara wa 700k unaendesha Crown Majesta cc 3000.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kujifanya vichwa vigumu tu!! Kwenye biashara ya ndege unaifanyia sifa?!! Lazima utaumia tu, ila kwakuwa tunaoumia ni walipa kodi, inasikitisha sana!! Na kamwe CAG, hataruhusiwa kuzifanyia ukaguzi kwani ni aibu, jiwe ndiye atakuwa anaturisha matango poli tu, kwa kuleta hesabu za mapato kuwa ndio NET PROFIT!!!
 
Ila cover lazima liendane na kilichomo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli, ila ilikupata taarifa zaidi ili uweze kuchangia mjadara huna budi kuyapitia Tena kwa umakini yaliomo ndo utapata points za kuchangia iwe kusifia/support au kupinga/kutusi/ kukashifu au hata kutoa maani yako neutral.......

Mfano.... Kuna wachangiaji wengi kwenye uzi huu wanabishana kuhusu Ni ndege vipi zilizoongelewa kwenda kufanyiwa service, ili Hali habari imeeleza hayo yote tena kwa wazi na ufasaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 993773

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kuwa, Ndege 2 za Bombardier zitapelekwa nchini Canada kwa service itakayogharimu bilioni 13.9, Mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi, akiongea na TBC leo asubuhi, ameeleza kuwa, kwa kawaida ndege hufanyiwa service kwa masaa na kwamba service kubwa hufanyika kila baada ya ndege kukimbia kwa muda wa masaa 4,000.

Matindi alisema kuwa wakati wa kuifufua ATCL ilikuwa na Marubani 11 lakini kwa sasa ina Marubani 50, kati yao 48 wazawa na 02 wageni.
Mipango iliyopo ni kufikisha marubani 60.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, maboresho makubwa yamefanyika ya kuajiri wahandisi wapya na wa zamani na kufikisha idadi ya wahandisi 80.

Matindi alisema kuwa, wanatarajia kuanzisha program ya kuchukua wanafunzi kutoka vyuoni mmoja kwa moja na kuwafundisha na kwamba watakaoonyesha moyo wa uzalendo na maadili wataajiriwa.
ATCL wapambane ili waweze kuifufua karakana yetu kule KIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.

“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.

Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.

Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.

“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.

Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.

Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.

Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.

Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.

Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.

Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
Inayokarabatiwa ni bombardia Q 300 ile ZAMANI ambayo haifanyikazi Na nyingine ile ya Rais siyo bombrdia.Over!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ndoto kwa ATC kukua na kuendelea kibiashara hata kama wangemiliki ndege kibao kama Ethiopia airline kwani kuna wajanja wengi ambao bado wanapanga njama za kupiga pesa kisayansi zaidi.
 
Tuliambiwa hizo ndege ni mpya kabisa sasa hata miaka 2 tunaingia kwenye ghalama kubwa kiasi hicho?
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.

“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.

Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.

Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.

“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.

Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.

Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.

Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.

Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.

Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.

Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila baada ya masaa 4,000
Service canada.
HIZO NDEGE ZINA FAIDA AU HASARA

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hiyo hesabu ikoje kila baada ya masaa 4000! Unatoa shililngi bilioni 6.7 kwa services tu, kuna faida tena hapo utakayo kiwa unapata?? Kuna kitu hakiko sawa!!!je hayo masaa hiyo ndege inakuwa imeshazarisha hiyo faida kweli?!!
Surely, ni gharama kubwa ndio maana hata Waziri Kamwelwe alilifafanua hilo na kusema Serikali iko mbioni kukarabati hanga lililopo KIA.

IMG_0619.JPG
 
Back
Top Bottom