Herr muller
JF-Expert Member
- May 28, 2018
- 1,017
- 1,214
ni vile tu watz wengi wako na uelewa mdogo sana mkuu, hizi ndege ni mikebe kabisa

utangoja sana mkuu, acha tulipe ndege kwanza
Tulishapigwa hizo,jiwe mwenyew haelimishiki,gambagamba lisilobadilikani vile tu watz wengi wako na uelewa mdogo sana mkuu, hizi ndege ni mikebe kabisa
Tunazisubiri kwa hamu kubwa hapa Montreal.Maana yake kati ya ile faida ya bilioni 23
Bilioni 13 zarudi Canada........
Faida inapungua hadi 10
Sent using Jamii Forums mobile app
Iwe inafanyiwa baada ya miezi miwili mwaka mmoja haijalishi. Mlisaini mkataba nao matengenezo yoyote Canada wazungu waliona wajinga ndio waliwao. Mkiwavuruga na madini watasubiri ndege iende kwa service halafu wataishikilia END OF THE MOVIE
Acheni kujipa moyo mmelikoroga
Muwe mnasikiliza
Hivi wewe masikini unadhani kila mtu ni mjinga ? unachekwa ujue !
kila kitu inafikia muda kinahitaji ukarabati ni kweli haijalishi kimetumika muda gani.... Kwa maelezo mazuri haya yanatia moyo kiasi.Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742
14JAN 2019
Bombardier kukarabatiwa Canada kwa bilioni 13.9/-
SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao. Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.
“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.
Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo. Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.
“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.
Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.
Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa. Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.
Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi. “Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.
Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege. Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.
Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.
Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
Kama zimeharika zitawezaje kwenda Kanada?
SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao. Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).
N siasa tu hzoNi ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

Lissu mnamdanganya tu jamani. Hata kura 200000 hawezi pata. Hana issue yaani. In short, hakuna mtu wa kushindana na JPM kwa sasa. Iwe nje au ndani ya chama chake. Propaganda pigeni lakini ukweli mnaujua.CAG akague kwa sheria gani bunge lilishapitisha sheria ya kumzuia kukakua ATCL na migodi #2020 Lissu#
Kadanganye mafala wenzakoAcha uongo,hiyo ni ile ndege ya pekee ambayo atcl walikuwa nayo kabla Serikali haijaanza kununua zingne.usiwe unaongea kitu bila kuchunguza
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi naamania kinachogomba hapa ni kwanza LUGHA na pili ni CHUKI BINAFSI! Nafafanua. LUGHA inagomba hasa hasa kaw uwepo wa neno SERVICE. Kwa wale ambao mmeshawahi kumiliki vyombo vya moto au mashine mbalimbali, mnajua hilo neno SERVICE, yaani kukifanyia chombo chako ukaguzi wa kitaalamu na kiufundi aidha kwa kubadilisha mafuta au oil au some delicate PARTS. Pia hili ni pamoja na kuendana na muda wa saa za kufanya kazi, and in this respect, muda wa kuruka angani. Haya mambo hayana ushabiki, muda wa service ukifika lazima u- complile irrespective na bila kujali Dogo au Mwepesi au Shimo atasema nini. Pili nadhani ushabiki wa kisiasa ndio unasukuma watu kusema na kuandika waandikayo! Na kwa vile ni watu wanao subiri jambo ndiyo waseme kwa sababu wameishiwa HOJA, basi linapotokea jambo kama hili, BASI wanapata kisemeo na wengine wanafuata tu hata kama hawajui suala lenyewe liko vipi!