Serikali yawalipia viingilio Maafisa Habari wa Serikali kushuhudia mechi ya Tanzania Vs Uganda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Wizara ya Habari itawalipia Maafisa Habari wote viingilio vya kwenda kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Mkapa (Jumanne Machi 27. 2023).

Waziri Mkuu amesema hayo wakati akihutubia katika Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Njerere, Dar es Salaam, leo Jumatatu Machi 27, 2023.

Mbali na kuwalipia kiingilio cha mchezo huo, Msemaji wa Serikal, Gerson Msigwa amesema Wanahabari hao wataandaliwa usafiri pia wa kwenda na kurudi.

Mchezo huo wa kuwania Kufuzu Michuano ya Afrika AFCON ni wa marudio baina ya timu hizo baada ya Tanzania kushinda goli 1-0 katika mchezo uliopita wa Kundi F.
FsKoF9lWIAIFHve.jpg


FsKoF9mXgAMopQf.jpg
 
Pesa za wajinga.. zinatembea

Badala ya kutoa huduma muhum kwa wananchi ikiwemo kuwekeza kwenye maendeelo ya viwanda na kilimo kila siku ni bla bla na kutapanya pesa
Just motivation Ili waende uwanjani na Kwa kuwa maafisa habari wote wapo dar kwenye semina waongeza idadi ya watazamajii japo si washangiliaji.
 
Ndiyo kusema hizi pesa zinazoendelea kuchezewa kila siku, hazina mwenyewe, au?
 
Kodi Za Watanzania hizo.....!

Zinatapanywa hovyo hovyo...!

Zingeweza kununulia Hata Panadol tu...!
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza Ofa ya tiketi na usafiri kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wote wanaoshiriki kikao kazi Cha 18 kwenda Uwanjani kuishangilia Taifa Stars itakapocheza na Uganda The Cranes Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, ikiwa ni mchezo wa kufuzu AFCON mwaka 2024.

Mhe. Majaliwa ametangaza ofa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Maafisa hao, leo Machi 27, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati akifungua kikao kazi cha 18 cha Maafisa hao kinachofanyika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Saidi Yakubu ameshiriki.

Taifa Stars itacheza na Uganda The Cranes Machi 28, 2023 ikiwa ni mechi ya marudiano baada ya kuifunga Goli 1 Kwa 0 katika mchezo wa awali uliochezwa Machi 24, 2023 mjini Ismailia nchini Misri.

IMG-20230327-WA0029.jpg
 
Just motivation Ili waende uwanjani na Kwa kuwa maafisa habari wote wapo dar kwenye semina waongeza idadi ya watazamajii japo si washangiliaji.
Doing what if they can't afford it... tuache mchezo na kodi zetu jamani.
 
"Tuna wachezaji wachache waandamizi ambao wanaongoza mabadiliko ya kizazi na tunategemea zaidi kizazi kilichoshiriki Afcon U20 kule Mauritania. Hakuna mahali pazuri pa kumbadilisha mtoto kuwa mwanaume zaidi ya Benjamin Mkapa," alisema Micho.
 
NI UJINGA.
Afisa habari wa wizara ni wakukosa kiingio cha elfu tano kuingia mwenyewe uwanjani?.
Au ni LAZIMA?
Vipi kwa atakaekataa kwenda pamoja na kulipiwa?.
Ataadhibiwa?
PM Majaliwa anataka hao maofisa habari waende kujifunza ili wawe active kama wale wa Simba, Yanga, Mtibwa, na Ruvu Shooting, hilo ndio lengo la kuwapeleka huko.
 
"Tuna wachezaji wachache waandamizi ambao wanaongoza mabadiliko ya kizazi na tunategemea zaidi kizazi kilichoshiriki Afcon U20 kule Mauritania. Hakuna mahali pazuri pa kumbadilisha mtoto kuwa mwanaume zaidi ya Benjamin Mkapa," alisema Micho.
Hili ni biti la kiutu uzima, anamaanisha patachimbika hapo Kwa mkapa iwe mvua au jua, kimbunga au upepo lazima mwanaume ajulikane ni nani.
 
Back
Top Bottom