benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,035
Picha: Rais Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wamenunua jumla ya tiketi 4,000 za mechi ya kufuzu AFCON 2023 kati ya Tanzania na Uganda.
Tiketi hizo zitagawiwa kwa mashabiki ili waende kushuhudia mechi hiyo itakayochezwa uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Machi 28 mwaka huu.
===
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hasaan na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wamenunua tiketi 4,000 kwa ajili ya mashabiki kwenda uwanjani kuishangilia Taifa Stars itakapokuwa inacheza dhidi ya Uganda.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupitia simu ya Meneja wa Habari wa Simba Ahmed Ally alitoa taarifa ya kununua tiketi hizo wakati wa kampeni ya kununua tiketi ili kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani kuishangilia timu ya Taifa.
Jumanne Machi 28,2023 Taifa Stars itacheza mechi ya marudiano dhidi ya Uganda kuwania kufuzu Fainali za AFCON 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.