Kwa hili la kuwasafirisha Yanga, natofautiana na Serikali

Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
419
638
Siku ya jana Jumatatu April01, 2024, baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti vikiwakariri baadhi ya viongozi wa serikali wakitoa taarifa ya kugharamia safari ya mashabiki wa club ya Yanga kwenda na kurudi nchini Afrika kusini ili kwenda kuishangilia timu hiyo itakapoumana na timu ya Mamelody Sundowns ya huko Afika ya kusini katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya ligi ya mabinwa Afrika unaotarajiwa kupigwa siku ya tarehe 5, April , mwaka huu.

Hapana shaka kitendo hiki cha serikali ni cha kupongeza, kwani kinaunga mkono maendeleo ya michezo na vilabu nchini.

Hata hivyo serikali ilipaswa kutafakari kwa kina kama kweli Yanga walistahili kupewa huo msaada!....Unatoaje msaada kwa mtu ambaye anaweza kufanya kazi na kutengeneza fedha kwa jasho lake lakini kaamua kutoa huduma bure alafu gharama zinapomfika anakuwa ombaomba?

Kwa ukubwa, msisimko na mvuto wa ile mechi kati ya Yanga na Mamelody ni Dhahiri hapakuwa na sababu ya kuweka kiingilio bure na Yanga ingeweza kutengeneza pesa ndefu ambayo leo hii ndio wangeitumia kugharamia hizo gharama badala ya kwenda kuomba msaada wa serikali.

Ni ajabu Serikali kila siku inazihamasisha taasisi zake kuweka mkazo kwenye kukusanya mapato na kuna viongozi wengi tu wametumbuliwa ama kwa kuzembea kukusanya mapato au kutumia vibaya fedha za makusanyo ya mapato, alafua leo hii serikali hiyohiyo inakuja kumgharamia mtu ambaye anaachia mapato yanapotea kizembe wakati angeweza kuyakusanya kirahisi kabisa kuna miradi kibao ya wananchi imekwama kwa kukosa fedha za kuiendesha.

Sikatai serikali kusaidia kugharamia michezo , hapana lakini kwa hili la Yanga kuna kitu hakipo sawa, sababu mechi hiyo ya mkondo wa pili sio ya kushtukiza, bali tangu mwanzo Yanga walifahamu fika kuwa baada ya mechi ya mkondo wa kwanza watakuwa na mechi nyingine ya mkondo wa pili hivyo walipaswa kuweka mkakati wa kukusanya fedha ili kuwezesha hilo.

Tena walikuwa na nafasi kubwa kabisa ya kulifanikisha hilo sababu kampeni yao ya uhamasishaji wa mashabiki kuja uwanjani ilifanikiwa vya kutosha, ajabu kumbe walikuwa wakitangaza kutoa huduma bure huku upande mwingine wanawaza kwenda kuikamua serikali!

Nihitimishe kwa kusema serikali ifanye tafakari upya, hapa itajibebesha mzigo wa gharama usiokuwa na sababu kwa uzembe wa watu wachache. Fedha hizo kama kweli serikali itazitoa basi tukubali tuna tatizo katika menejiment ya fedha za umma tunazozipata na hii ni mojawapo ya sababu zitakazotufanya tuendelee kukopa huko mataifa ya Magharibi mpaka mwisho wa dunia hii.
 
Yanga imeruhusu wananchi wa serikali kuingia bure uwanjani ili kukuza soka na kuongeza mapenzi ya soka nchini, Leo serikali ishindwe kurudisha fadhila kwa kugharamia safari ya kwenda bondeni? Acha Nongwa!
 
Sikatai serikali kusaidia kugharamia michezo , hapana lakini kwa hili la Yanga kuna kitu hakipo sawa, sababu mechi hiyo ya mkondo wa pili sio ya kushtukiza, bali tangu mwanzo Yanga walifahamu fika kuwa baada ya mechi ya mkondo wa kwanza watakuwa na mechi nyingine ya mkondo wa pili hivyo walipaswa kuweka mkakati wa kukusanya fedha ili kuwezesha hilo. Tena walikuwa na nafasi kubwa kabisa ya kulifanikisha hilo sababu kampeni yao ya uhamasishaji wa mashabiki kuja uwanjani ilifanikiwa vya kutosha , ajabu kumbe walikuwa wakitangaza kutoa huduma bure huku upande mwingine wanawaza kwenda kuikamua serikali!.

Sio kwamba uongozi wa Yanga haukujipanga kuhusu swala la kupeleka mashabiki kwenye mechi ya marudiano, kama ulikuwa mfuatiliaji kwenye ukurasa wa Yanga walikuwa wanahamasisha mashabiki na hadi gharama wakaweka wazi ni kiasi gani cha pesa unaweza kwenda Afrika kusini kutazama mechi na kuna watu kadhaa tayari walikuwa wameshatoa pesa kwaajili ya kwenda kuangalia hiyo mechi.
Na ndio maana baada ya serikali kuamua kuunga mkono kusaidia safari ya mashabiki, mashabiki wamerudishiwa pesa zao. Hizo ni jitihada za uongozi wa Yanga kuamua kuwawezesha mashabiki wake. Awali waliruhusiwa kuingia bure na sasa wamewaombea kwa serikali iwawezeshe. Hata uongozi wa Simba wangekuwa na maono haya wasingekataliwa kuwezeshwa.
 
Timu huwa inaruhusu mashabiki kuingia bure endapo tu imeonekana hakuna mashabiki wa kutosha. Sasa uto wanajifanya wajamaa wakati kuweka hata kapeti pale kaunda kumewashinda. Timu inaendeshwa kiuswahili swahili.
Timu hii hii inayoendeshwa kiswahili swahili itawapita kimaendeleo. Subiri muda utaongea kwanzia uwanjani hadi nje ya uwanja (miundombinu)
 
Yanga imeruhusu wananchi wa serikali kuingia bure uwanjani ili kukuza soka na kuongeza mapenzi ya soka nchini, Leo serikali ishindwe kurudisha fadhila kwa kugharamia safari ya kwenda bondeni? Acha Nongwa!
Unakuzaje soka wakati timu tu za vijana ni chupli chupli. Na ni chupli chupli sababu ya umasikini wa vilabu. Sasa unaacha hela ambazo zingekusaidia kuwakuza vijana halafu useme unakuza soka kwa kuacha hela wakati kiuchumi haupo vizuri. Hakuna timu yenye mashabiki wengi huwa inaruhusu mashabiki kuingia bure.
 
Timu huwa inaruhusu mashabiki kuingia bure endapo tu imeonekana hakuna mashabiki wa kutosha. Sasa uto wanajifanya wajamaa wakati kuweka hata kapeti pale kaunda kumewashinda. Timu inaendeshwa kiuswahili swahili.
Kwa kuendesha timu "Kiswahili" Simba ni No.1.
 
Yanga imeruhusu wananchi wa serikali kuingia bure uwanjani ili kukuza soka na kuongeza mapenzi ya soka nchini, Leo serikali ishindwe kurudisha fadhila kwa kugharamia safari ya kwenda bondeni? Acha Nongwa!
Double standards ndio kitu kinachopingwa hapa?

Je maendeleo ya soka hapa nchini yanaletwa na Yanga tu? Hakuna team nyingine?

Simba wapo katika hatua moja ya mashindano na Yanga. Je kwanini upendeleo ufanywe kwa upande mmoja tu?
 
Unakuzaje soka wakati timu tu za vijana ni chupli chupli. Na ni chupli chupli sababu ya umasikini wa vilabu. Sasa unaacha hela ambazo zingekusaidia kuwakuza vijana halafu useme unakuza soka kwa kuacha hela wakati kiuchumi haupo vizuri. Hakuna timu yenye mashabiki wengi huwa inaruhusu mashabiki kuingia bure.
Kwa hiyo kina Bakhresa, GSM, au taasisi kama NMB CRDB zinapotoa misaada kama madawati mashuleni, inamaanisha wao wenyewe wamejitosheleza? Huo ni msaada kama misaada mingine! Serikali imerudisha fadhila
 
Double standards ndio kitu kinachopingwa hapa?

Je maendeleo ya soka hapa nchini yanaletwa na Yanga tu? Hakuna team nyingine?

Simba wapo katika hatua moja ya mashindano na Yanga. Je kwanini upendeleo ufanywe kwa upande mmoja tu?

Double standard imetoka wapi?
Yanga wameomba serikali na wala sio serikali ndio iliyowafuata Yanga, sasa je uongozi wa Simba umewaomba serikali kisha wakakataliwa?
Mnaacha kulaumu viongozi wenu kwa kukosa maarifa ya kutumia fursa mnalia na serikali. Nyie mmejifanya mnajimudu wakati Yanga wao wamejishusha na kujifanya hawajimudu hivyo serikali imeombwa iwasaidie.
 
Nyie hamkuonyesha uzalendo kama wa Yanga kuruhusu mashabiki waingie bure kutazama mechi
 
Double standard imetoka wapi?
Yanga wameomba serikali na wala sio serikali ndio iliyowafuata Yanga, sasa je uongozi wa Simba umewaomba serikali kisha wakakataliwa?
Mnaacha kulaumu viongozi wenu kwa kukosa maarifa ya kutumia fursa mnalia na serikali. Nyie mmejifanya mnajimudu wakati Yanga wao wamejishusha na kujifanya hawajimudu hivyo serikali imeombwa iwasaidie.
Trash
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom