Serikali yamuumbua RC Mbeya

Mtanzania,

...........sio madhumuni yangu HATA SIKU MOJA kukuza/kuchochea migogoro.....kwa jumbe ninazoandika hapa.......sijui huo ujumbe wangu ni kwa vipi unakuza mgogoro!!......

well....siku hizi Tanzania ni mwendo wa kujuana kwa vilemba eeehh......anyhow......nilifikiri kuchangia kwangu hoja hapa, kwa namna moja au nyingine ni kusaidiana kimawazo...........i'm deeply sorry kama nimekukwaza.

Mkuu Ogah,

Nilikuwa sikusemi wewe na wengine ambao mnachangia kwa nia njema kabisa hapa JF. Ni wale ambao wanaenda kule na kutafuta kuna jungu gani kati ya hawa waheshimiwa.

Tuendelee kuchangia si ajabu wapambe wao wanawafikishia. Wakiona wananchi hatutaki huo ugomvi wao, labda watabadilika.

Samahani ujumbe wangu haukueleweka.
 
Uamuzi wa Serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Kyela kwa ajili ya waathirika wa mafuriko makubwa yaliyotokea wilayani humo, unamuumbua RC wa Mbeya ambaye kwa mwezi mzima sasa amekuwa akidai kuwa hakuna maafa Kyela na mafuriko yaliyotokea ni ya kawaida tu!

Ingekuwa nchi zingine, kiongozi wa aina hii angefukuzwa kazi kwa kuzuia misaada na kuihujumu Serikali kwa wapiga kura.

Tatizo la Mwakipesile ni kuwa katika miaka 10 ya ubunge wake yametokea mafuriko mengi Kyela na hakuwahi kugawa hata kilo moja ya mchicha kwa walioathirika. Hivyo ameamua kumvurugia Mbunge wa Kyela, Dk. H. Mwakyembe ambaye alipambana naye kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Kyela mwaka 2005, Mwakipesile akashindwa vibaya na sasa anatumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa kumrudi mbaya wake.

Lazaros

Hili haliwezi kuwa geni kwa sababu inakuwaje rais anamchagua mkuu wa mkoa tena anampeleka kule ambako ameshindwa hata kupata ubunge na anakuwa na mamlaka makubwa kwa mkoa mzima.

Hii inaonyesha jinsi JK alivyo out of touch na wananchi wa Mbeya ambako tangu achaguliwe hajafanya ziara rasmi (Quote JF members). Je hii ni kuwakomoa wananchi wa Mbeya waliomnyima rafiki yake ubunge?

Je Comoro alikokwenda na wanajeshi wetu walimchagua yeye?
 
Hili haliwezi kuwa geni kwa sababu inakuwaje rais anamchagua mkuu wa mkoa tena anampeleka kule ambako ameshindwa hata kupata ubunge na anakuwa na mamlaka makubwa kwa mkoa mzima.

Hii inaonyesha jinsi JK alivyo out of touch na wananchi wa Mbeya ambako tangu achaguliwe hajafanya ziara rasmi (Quote JF members). Je hii ni kuwakomoa wananchi wa Mbeya waliomnyima rafiki yake ubunge?

Je Comoro alikokwenda na wanajeshi wetu walimchagua yeye?

na JK mpaka leo hajakanyaga mbeya (since achaguliwe)..inakuonyesha anajali vipi watu wa mbeya...ngurdoto na marekani sijui ameenda mara ngapi
 
na JK mpaka leo hajakanyaga mbeya (since achaguliwe)..inakuonyesha anajali vipi watu wa mbeya...ngurdoto na marekani sijui ameenda mara ngapi

Hivi kuna mkoa mwingine ambao JK hajakanyaga toka achaguliwe kuwa rais?

Mnaojua tuwekeni sawa.

Mimi sielewi JK anaogopa nini Mbeya maana naona bado ana wapenzi wengi tu kule wala hawezi kuzomewa, hasa kama ataongozana na prof. Mwakyembe.

Si ajabu kuna watu wanamwambia mambo ni mabaya sana huko wakati huenda hali ni tofauti kabisa.

JK, wewe nenda tu Mbeya na wala hawatakuchuna ngozi!
 
Mkuchika ajitosa siasa za Mbeya


na Christopher Nyenyembe, Mbeya



NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kapteni mstaafu George Mkuchika, amejitosa katika siasa za Mbeya.

Habari zilizopatikana jijini hapa zinaeleza kuwa, katika ziara yake hivi karibuni mkoani humu, Mkuchika alifikia hatua ya kuwakemea baadhi ya viongozi katika vikao vya ndani.

Imeelezwa kuwa, katika vikao hivyo, Mkuchika, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, alisema chama hicho kimechoshwa na misuguano ya kisiasa inayoendelea mkoani hapa.

Aliwataka viongozi wa chama hicho ngazi za wilaya na mkoa kuacha ugeugeu na kutumia majukwaa na mgawanyiko wa makundi kumgombanisha Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya.

Habari za ndani ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka kwenye vikao kadhaa vilivyofanyika mkoani hapa wakati wa ziara ya Mkuchika, zinaeleza kuwa Mkuchika alitumia fursa hiyo kuonya na kukemea makundi yanayowachafua viongozi wa chama hicho, kwa kuwa viongozi hao ni safi na hawana ugomvi wowote.

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu na kile cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, zinaeleza kuwa Mkuchika alionya dhidi ya tabia zilizofanywa na watendaji wa chama hicho, hasa makatibu ngazi za wilaya na mkoa, ambao walitumia nafasi zao kumpiga vita Profesa Mwandosya.

Habari ambazo zimekuwa zikishika kasi na kushabikiwa na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani humu, zinadai kuwa kuna msuguano kati ya Rais Kikwete na Waziri Mwandosya.

Inadaiwa kuwa msuguano huo ndio unamfanya Rais Kikwete asite kuutembelea Mkoa wa Mbeya, na kukwama kwa baadhi ya miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe.

Mmoja wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, aliyeomba jina lake lisitajwe kwa sababu zilizo wazi, alisema kuwa, naibu katibu mkuu huyo hakutaka kuficha kitu na kuwapasha ukweli viongozi waliojiingiza kwenye makundi na kuharibu sifa nzuri ya chama hicho mkoani humu.

“Migongano hii yote na makundi mliyoyaunda ya kuchafuana, kumchafua rais na Profesa Mwandosya ndio iliyovipa umaarufu vyombo vya habari mkoani Mbeya ambavyo vimekuwa vikiandika migogoro ambayo nyie wenyewe ndio mliokuwa mkiianzisha. Sasa nataka yaacheni yote yaliyopita, kijengeni chama na wapeni ushirikiano wanachama wenzenu walioshinda,” chanzo hicho kilimnukuu Waziri Mkuchika.

Mkuchika alisema kuwa, anazo taarifa kuwa makundi hayo yalishughulika sana kuhakikisha kuwa Profesa Mwandosya hashindi ujumbe wa NEC taifa kwa kumfanya aonekane ana ugomvi na Rais Kikwete.

Katika mazingira hayo, inadaiwa kuwa, Mkuchika aliweka bayana uhusiano mzuri uliopo kati ya Profesa Mwandosya na Rais Kikwete, na kwamba wanachama wa chama hicho wanaotumia fursa zao kuwachafua na kuwagonganisha, wajue wazi wanafanya hivyo kwa viongozi wa chama na serikali ambao ni marafiki na hawana ugomvi wowote.

Alinukuliwa akisema: “Rais Jakaya Kikwete hana ugomvi wowote na Profesa Mark Mwandosya, na kuonyesha kuwa hawana ugomvi huo, ameweza kumteua mara mbili mfululizo kuingia kwenye Baraza la Mawaziri na kwamba ni marafiki wakubwa ndani ya CCM.” Aliongeza kuwa iwapo kungekuwa na uhasama wowote, isingekuwa rahisi kwa waziri huyo kuteuliwa mara mbili mfululizo kuwa waziri.

Mkuchika alimwelezea Profesa Mwandosya kuwa ni mwanachama muhimu na mashuhuri anayetegemewa ndani ya CCM na serikali, na ndiyo maana anaheshimika.

Katika kuhakikisha kuwa uongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa unaacha migongano, mjumbe mwingine alisema kuwa kazi kubwa sasa ipo mikononi mwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mullar, ambaye kwa kushindwa kusimamia katiba na kanuni, amekuwa akiitisha vikao vyenye nia ya kuwadhalilisha viongozi wengine, wakiwemo wabunge, kinyume cha utaratibu wa vikao vya chama.

Aidha, Mkuchika alipinga tuhuma kuwa Rais Kikwete hatembelei Mbeya kutokana na kutoelewana na Profesa Mwandosya na kuwahakikishia wajumbe kuwa, ziara za kiongozi huyo wa juu wa serikali zitafanyika mkoani humu kutokana na ratiba aliyopangiwa, na kwamba hawezi kuwaogopa wananchi wake waliompa dhamana ya kuiongoza nchi.
 
Kwanini Mwandosya mwenyewe na Kikwete wasifanye ziara ya pamoja Mbeya pamoja na Mwakyembe na Mwakipesile?
 
Back
Top Bottom