Serikali yamuumbua RC Mbeya

Umefikia wakati wakuu wa mikoa na wilaya wakachaguliwa kwa kura na wananchi badala ya kuteuliwa na Raisi kama ilivyo sasa.
 
Ulisikia wapi kesi ya nyani akapelekewa ngedere???

Huyo mkuu wa wilaya ya Kyela, Ndg Mshimba ndiyo huyo huyo aliyekuwa anatumiwa na Mwakipesile ili Dr. mwakyembe asipokewe na kwa maandamano na wananchi wa Kyela hadi Mkuu wa polisi wilayani Kyela aliposimama kidetekuthibitisha kuwa haoni kama kungetokea vurugu. Hata nakala za barua walizokuwa wakitumiana Mwakipesile na Mshimba zilipatikana mpaka wakaishia kuumbuka tu.

Pia Ukumbuke mwaka jana ni huyi huyo Mshimba alimzuia Prof Mwandosya (waziria wa Mazingira wakati huyo) ku-officiate harambee ya akina mama wilayani Kyela ya ku-raise fundi yao hata pale mbunge wao (Dr. Mwakyembe ) alipomsihi mkuu wa wilaya huyo awaruhusu akina mama kuendesha shughuli zao, lakini aligoma kwa shinikizo kutoka kwa Mwakipesile na Lowassa. Sababu aliyotoa mkuu wa wilaya ni kuwa yeye ndiyo mkuu wa wilaya na eti hapata taarifa ya waziri kwenda wilayani kwake kufanya kazi ile, huku akisema hajamzuia kuindgia Kyela ila kufanya shughuli rasmi kama zile.

Je, huyo ndio tumwamini????

Ahsante,
 
maneno mazito hayo; tatizo ni kuwa siasa za Kyela zinahistoria ambayo watu wengi kitaifa hawazijui na hazijapata exposure kama siasa za Upareni na Dayosisi ya Arusha.

Siamini kuwa masuala ya kisiasa ya Kyela ni ya siasa tu na hakuna elements nyingine hasa baada ya sakata la dayosisi ya Rungwe???

Binafsi naamini itakuwa vizuri sana kuleta mkuu wa mkoa mwingine kabisa Mbeya itasaidia sana kuzima haya baadhi ya maneno kwani siyo tu yameingilia siasa za wilayani (Kyela) bali pia za mkoani na ambazo zinanukia hadi kwenye Taifa.

Mwanakijiji,

Mimi na dini ni mbalimbali pamoja na kwamba nililelewa kwenye familia ya dini sana.

Kwa uelewo wangu mdogo juu ya matatizo ya dini kule Kyela, nitasema dini sio issue kwenye hili tatizo la Mwakipesile na Mwakyembe. Naweza kuwa na makosa maana sijawahi kumuulizia mtu yeyote kama dini ni issue kwasababu mimi huwa siongelei mambo ya dini (ukisearch threads za dini hata hapa JF, hukuti mtanzania). Ninahisi dini sio issue.

Kwahiyo sasa Kyela kuna mipasuko miwili, ule wa dini kati ya Kyela na Rungwe na sasa huu wa wanasiasa. Bahati nzuri hawa waliozua mgogoro mkubwa wa dini, mimi nawafahamu vizuri mno, walikuwa ni viongozi wa dayosisi pale Rungwe wakati mimi nasoma Rungwe Sec. Ndio maana wengine hatuendi makanisani maana kama watu ni hao, afadhali wengine tubaki nje. Bahati mbaya watu kama hao ndio wanasababisha mpaka wafuasi wao wanauana, huku wao wanatanua kwa kutumia jina la mungu.

Nafikiri tatizo la sasa la Kyela ni siasa na pia Mwakipesile kupewa kuwa mkuu wa mkoa kumechangia sana.

Kwa wenzetu walioendelea, anayeshinda anakuwa wa kwanza kwenda kumponza aliyeshindwa. Kwa TZ washindi huendeleza vijembe na maneno mengine ya kashfa. Ndicho kilichotokea Kyela, kipigo cha Mwakipesile hakikuishia kwenye chumba cha uchaguzi, kiliendelea mpaka mitaani.

Na yeye alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa naye watu wake wakaenda mtaani na kufanya vijembe na kashfa zao.

Inayoumia hapo ni Kyela. Ndio ingefaa kama Mwakipesile angeondolewa Mbeya, lakini je kama haondolewi ndio mkoa wote utekwe nyara shauri ya ugomvi wa watu wawili?

Kwanini kila mtu asitimize wajibu wake na kutuacha wanachi tuamue nani anafaa?

Wasubiri 2010 tutawauliza juu ya ujinga wao huu kama wote wataamua kugombea.
 
Ulisikia wapi kesi ya nyani akapelekewa ngedere???

Huyo mkuu wa wilaya ya Kyela, Ndg Mshimba ndiyo huyo huyo aliyekuwa anatumiwa na Mwakipesile ili Dr. mwakyembe asipokewe na kwa maandamano na wananchi wa Kyela hadi Mkuu wa polisi wilayani Kyela aliposimama kidetekuthibitisha kuwa haoni kama kungetokea vurugu. Hata nakala za barua walizokuwa wakitumiana Mwakipesile na Mshimba zilipatikana mpaka wakaishia kuumbuka tu.

Pia Ukumbuke mwaka jana ni huyi huyo Mshimba alimzuia Prof Mwandosya (waziria wa Mazingira wakati huyo) ku-officiate harambee ya akina mama wilayani Kyela ya ku-raise fundi yao hata pale mbunge wao (Dr. Mwakyembe ) alipomsihi mkuu wa wilaya huyo awaruhusu akina mama kuendesha shughuli zao, lakini aligoma kwa shinikizo kutoka kwa Mwakipesile na Lowassa. Sababu aliyotoa mkuu wa wilaya ni kuwa yeye ndiyo mkuu wa wilaya na eti hapata taarifa ya waziri kwenda wilayani kwake kufanya kazi ile, huku akisema hajamzuia kuindgia Kyela ila kufanya shughuli rasmi kama zile.

Je, huyo ndio tumwamini????

Ahsante,

Nsololi,

Yote uliyoyaandika ni sawa lakini upande mwingine nao una yake. Mbunge naye alikuwa anaandika barua kisiri kumwandikia PM Lowassa na JK kwamba kumpa
ukuu wa mkoa Mwakipesile mtu ambaye wana Kyela wamemkataa ni dharau kwa mkoa wa Mbaya na Kyela. Bahati mbaya, kumbe wenzake wanamwonyesha hizo barua Mwakipesile.

Pia kuna mengine mengi tu.

In fact kamati ya usuluhishi ya Kinana ilimkuta Mwakyembe kama ana makosa na aliomba msamaha.

Mimi najiuliza ni sababu zipi zilimfanya Mwakyembe aombe msamaha? Maana mtu kama huna makosa kwanini uombe msamaha?

Kwa maoni yangu binafsi wote wawili wana makosa makubwa ya kukuza huu mgogoro. Wasipoangalia wote wawili wanaweza kuja kupay kisiasa.
 
Nsololi,

Yote uliyoyaandika ni sawa lakini upande mwingine nao una yake. Mbunge naye alikuwa anaandika barua kisiri kumwandikia PM Lowassa na JK kwamba kumpa
ukuu wa mkoa Mwakipesile mtu ambaye wana Kyela wamemkataa ni dharau kwa mkoa wa Mbaya na Kyela. Bahati mbeya, kumbe wenzake wanamwonyesha hizo barua Mwakipesile.

Pia kuna mengine mengi tu.

In fact kamati ya usuluhishi ya Kinana ilimkuta Mwakyembe kama ana makosa na aliomba msamaha.

Mimi najiuliza ni sababu zipi zilimfanya Mwakyembe aombe msamaha? Maana mtu kama huna makosa kwanini uombe msamaha?

Kwa maoni yangu binafsi wote wawili wana makosa makubwa ya kukuza huu mgogoro. Wasipoangalia wote wawili wanaweza kuja kupay kisiasa.

Mt,

Hata kama kulikua na matatizo kati ya Mwakyembe na Mwakipesile hajustify kunyanyasa wanaich ambao wanastaili kupatiwa msaada pale kunapotokea majanga kama yaliyowakuta. Personal issues kati yao haijustify yaliyotokea.

Mbona kuna wilaya zinaongozwa na sisiem na majimbo yanashikiliwa na upinzani bado hayatokei yaliyotokea????
 
Mtanzania, nakubaliana na wewe; lakini kuna baadhi ya matatizo ambayo lazima watu wayaangalie kwa karibu badala ya kuyakwepa.

a. Dini ni sumu mbaya sana ambayo hupita kizazi kimoja kwenda kizazi kingine. Sumu yake ni sawa kabisa na sumu ya ukabila au ubaguzi wa rangi. Lakini, sumu ya dini is more potent kwa sababu inahusiana na mambo ya umilele.

Watu wengi wameumia, kuuawa na mali kuharibiwa kwa sababu ya msukumo wa dini. Wakati mwingine matatizo ya kisiasa na mengine katika jamii yanaasili na chembe za dini. Hivyo, katika kutafuta suluhisho la kweli dini lazima iangaliwe kwa ukaribu.

b. Suala la kukubali kushindwa ni muhimu. Siyo tu kukubali kushindwa bali pia kumpa mshindi nafasi ya kufanya anachotaka kufanya badala ya kuwa kikwazo cha u tendaji wake.

Kusubiri nafasi nyingine ya kumuondoa mshindi ni sehemu ya demokrasia lakini kumharibia (sabotage) ni kujiharibia mtu mwenyewe.

c. Hata hivyo inapotokea matatizo na malalamiko kama ya Kyela, hakuna zaidi cha kufanya isipokuwa kumuondoa mmoja wao na katika hili anayehamishika ni Mwakipesile na si Mwandosya au Mwakyembe.

d. Endapo atakuja mtu mwingine ambaye si mwenyeweji wa Mbeya na matatizo yakaaendelea basi wananchi watajua kuwa yawezekana tatizo SI Mwakipesile...
 
Mt,

Hata kama kulikua na matatizo kati ya Mwakyembe na Mwakipesile hajustify kunyanyasa wanaich ambao wanastaili kupatiwa msaada pale kunapotokea majanga kama yaliyowakuta. Personal issues kati yao haijustify yaliyotokea.

Mbona kuna wilaya zinaongozwa na sisiem na majimbo yanashikiliwa na upinzani bado hayatokei yaliyotokea????

Bowbow,

Kama ni kweli nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Mimi sijui kama Mwakipesile alikataa au kukwamisha misaada yoyote. Hata kwa nyepesi nyepesi ninazopata toka huko wilayani, bado sijasikia hicho kitu.

Najua kuna diwani mmoja ambaye ni mtu wa Mwakipesile alikataa misaada kwa madai kwamba Mwakyembe alimtumia mtu wake ambaye anataka kugombea udiwani kwenye kata hiyo. Yeye anadai kama yeye ni diwani kwanini yeye asihusike.

Wote tulimlaani maana huwezi kukataa misaada wakati watu wana njaa. Mtoa misaada ana haki ya kuamua nani afikishe misaada full stop.

Sasa haya ya Mwakipesile ni kama ni kumzulia tu.

Jamani Kyela kuna mengi mno, kadri hayo matatizo yanavyonaswa na watu wa nje ndivyo huo ugomvi unavyozidi kuwa mkubwa kwani hata jambo ambalo huenda ni bahati mbaya linageuzwa kuwa njama.

Kwasasa njia ni kumhamisha Mwakipesile ingawaje binafsi najua hata akihamishwa, ugomvi utahamia kwa mkuu wa mkoa mwingine kwasababu sasa una sura zaidi ya wilaya. Kuna mambo ya Kyela na kuna mambo ya mtandao against pro. Mwandosya.

Mbona prof. Mwandosya na JK wanafanya kazi pamoja tu mbali na kila mtu kujua hawaelewani? Aliyesema binadamu huchagui jirani yako hakukosea.
 
Lakini kuna haja ya kuangalia pia jinsi gani JK anaweza kushiriki katika ku defuse hiyo pressure ya Mbeya. Afunge safari na Mwandosya, Mwakyembe na Mwakipesile.... Lakini kuendelea kuikwepa Mbeya haisadiii sana inachochea hisia za njama tu...
 
Kweli na huyoo JK pia aone aibu sasa ina maana Mbeya hakuna jipya?mbona haendiii ???inasikitisha kama ndio mpasuko wa chama basi ndio huoo....JK mtoe Mwakipesile,Nenda ukafanye ziara Mbeya watu waliokupa kura zaoo wanakusubiri.......na ahadi zako ulizowapa bado wanakumbuka.....achana na kina Mwakyembe na Mwandosya maana hutawaweza kamwe kwa lolote labda uchawii tuuuuuuu.........maana ndio uliokuweka hapo na unaoutegemea 99%
 
Nsololi,

Yote uliyoyaandika ni sawa lakini upande mwingine nao una yake. Mbunge naye alikuwa anaandika barua kisiri kumwandikia PM Lowassa na JK kwamba kumpa
ukuu wa mkoa Mwakipesile mtu ambaye wana Kyela wamemkataa ni dharau kwa mkoa wa Mbaya na Kyela. Bahati mbaya, kumbe wenzake wanamwonyesha hizo barua Mwakipesile.

Pia kuna mengine mengi tu.

In fact kamati ya usuluhishi ya Kinana ilimkuta Mwakyembe kama ana makosa na aliomba msamaha.

Mimi najiuliza ni sababu zipi zilimfanya Mwakyembe aombe msamaha? Maana mtu kama huna makosa kwanini uombe msamaha?

Kwa maoni yangu binafsi wote wawili wana makosa makubwa ya kukuza huu mgogoro. Wasipoangalia wote wawili wanaweza kuja kupay kisiasa.

Mtanzania, kwa maneno yako hapo ndio umethibitisha kabisa kuwa kuna matatizo Mbeya na kuyaacha yaendelee ni kujiandaa kwa ugomvi usio wa lazima. Siku moja shabiki wa Mwakyembe atampiga kibao shabiki wa Mwakipesile... na cheche hizo zitakapoanza tusije tukakaa na kuulizana "what happened"... Binafsi ningependa kujua Mwamunyange (CDF) yuko upande gani hapa...
 
Baadaye utataka na kujua Mtanzania yuko upande gani kwi kwi kwi!!!!

Kama unamjua Mwamunyange, usitegemee hata siku moja kujihusisha na huo ujinga. Yule jamaa haingiliki kabisa.

Mchapo nje ya maada, alipoteuliwa kuwa chief of staff, kuna Wambeya walitaka kwenda kumpongeza akasema hataki hata kusikia.
 
Nimekupata... nilitaka tu kuhakikisha kuwa CDF haijingiizi au haoenekani kujiingiza katika mambo haya. Vizuri to hear he is above local politics.
 
Kyela bado kwa mbali wanaendeleza mambo ya kichifu, ukichanganya na mambo ya kiserikali kunakuwepo na mgongano fulani kiutawala
 
Huyu Mwakipesile hapo amechemsha kabisa kama anamwalibia ili yeye agombee mwananchi gani ambaye atampa kura wakati anaona kabisa anatendewa vibaya.
Tunajua JK amembeba tu huyu Mwakipesile kwa kuulinda mtandao wake wa kumpaliza Mwandosya CCM makundi bado yapo na asipo angalia MWandosya atamzidi kete JK akiamua kuchukua fomu kugombea NEC.
TANGU MWANZO SABABU YA KUMWEKA UYO LOSER MWAKIPESILE ILIAWAKOTROL PROF NA DR SASA EBU TIZAMA BAADA YA ZARI LA RICHMONDULI ETI KUNA VUNZA ALIZUIA MAPOKEZI YA HARISSON DU ILI JAMAA AONEKANE KAMA KAWATENGA BA -IJIMBO LAKINI WALISHINDWA WAKALEGEA.
 
Matatizo ya Mwakipesile tunayajua. Ni sehemu ya mtandao ambao umevurugika baada ya Lowassa kuachia ngazi. Ijabu
 
Unajua Mwakipesile Ndiyo Yale Mamula Ya Kyela Hana Jipya Tuliangalia Duuuu Huyu Jamaa Ataweza
 
Back
Top Bottom