benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Serikali kupitia Wizara ya Afya, imetoa ajira ya mkataba kwa Mariam Mwakabungu, mwanamke anayejitolea kukumbatia watoto niti waliotelekezwa katika Hosptali ya rufaa ya mkoa Amana jijini Dares Salaam.
Ajira hiyo imekuja siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan kutuma salamu za pongezi zilizoambatana na fedha taslimu Sh milioni 2
Julai 16, gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii ilichapisha habari hukuhusu Mariam Mwakabungu (25) ambaye ameokoa maisha ya watoto njiti watatu hospitalini hapo kwa kuwakumbatia kwa njia ya kangaruu baada ya kutelekezwa na mama zao.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamis Julai 20, 2023 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameeleza utaratibu utakaotumika katikia kumpa ajira Mariam.
"Tutampa ajira ya mkataba kwanza, changamoto iliyopo bado hana sita za kuajirika, tutamshauri ajiendeleze kielimu ili aweze kupata sifa za kuajirika Serikalini.
"Madaktari wanasema yule mama anajitoa na anapenda kufanya hiyo kazi ana moyo yaani ni kitu anapenda sasa kwa sababu hajasomea uuguzi itabidi aingize katika utaratibu huo ili aweze kupata sifa," amesema Waziri Ummy na kuongeza;
"Ana miaka 25 bado anamuda anaweza akaenda kusoma uguzi ngazi ya astashahada akawa muuguzi wa watoto njiti.
Tunaendelea kumpongeza a tutamshauri ajiendeleze kielimu ni jambo zuri na tumemuomba afanye hivyo, amesema.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma