BabuMkubwa
JF-Expert Member
- Feb 11, 2017
- 2,281
- 3,343
Wananchi wamethibitisha mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa huo ugonjwa upo na umeua watu kadhaa ( taarifa ya habari ITV saa 2 usiku 08/02/2021)
Habari saa mbili.Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima ameagiza kusimamishwa kazi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chunya, Dkt. Felista Kisandu kupisha uchunguzi kwa madai ya kutoa taarifa zisizo sahihi za ugonjwa usiofahamika...
Nchi hii viongozi sahv sijui wanafanyaje kaziHabari saa mbili.
Wananchi , mbele ya Mkuu wa Mkoa, wamethibitisha kuwepo ugonjwa huo na kusema toka mwaka 1996, wameshakufa watu 34 ambao wanafahamika, ikiwa ni pamoja na mwalimu wa sekondari.
Mama Dr Gwajima , mpira uko kwako!
ITV sijui watakuwa na kosa gani hapa maana wao wamechukua taarifa toka kwa ofisa wa serikali, msemaji wa taasisi anayoiongoza na kuirusha hewani...Dr. Kisandu, Diwani pamoja na ITV walijisahau wakafikiri kuwa Tanzania bado ipo kwenye utawala wa kidemokrasia. The worst is yet to come folks!
uchonganiahi huo.muacheni dada wawatu afanye majukumu aliyopewa bana.
wanafanya kazi kumfurahisha jamaa yaoMwanzoni nilimuona mchapakazi saivi nimegundua ni lijinga linalotumiwa kisiasa
Nani atanunua ubongo wa ng'ombe hiyo?Uza ubongo huo ww, kwani kuwa na maambukizo ya ugonjwa fulani ni lazima kuwe na vifo? Kwani kila aliyepata HIV amefariki?
Huyu waziri wa afya baliokotwa wapi?Hii kitu Mkuu wa mkoa na azam jana wamierusha vizuri zaidi na mkuu wa mkoa kaunda tume.
sasa m,bona juzi walikurupuka na huo mbarua wa kulaumu ITV.
CCM ni janga la taifaWaziri wa Afya, Dorothy Gwajima ameagiza kusimamishwa kazi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chunya, Dkt. Felista Kisandu kupisha uchunguzi kwa madai ya kutoa taarifa zisizo sahihi za ugonjwa usiofahamika.
Amesema hata kama ugonjwa huo ungekuwepo waziri ndiye anatakiwa kutoa taarifa.
View attachment 1696883View attachment 1696884
Msipendelee sana kuweka chumvi kwenye mambo ambayo hatuna uhakika nayo - mfano: nani kathibitisha kwamba Ifumbo kuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola??Tatizo la serikali kuficha ugonjwa.
Zika - Aliondolewa Dr Mwelentuli Malecela
Ebola - Imemuondoa Mganga wa huko Ifumbo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Chalamila na mbunge wa Chunya wamezuru kijiji cha Ifumba wilayani Chunya kupata taarifa za ugonjwa usiojulikana.Serikali haifanyi kazi kama genge!
Kuna taratibu zake za uwasilishaji wa taarifa!
Je huyo daktari alifanya jitihada gani kuwasiliana na ngazi za juu kiutawala ili kujirudhisha kabla ya kukimbilia kwenye Media?
Taratibu za kiutunishi zinamhusu.
Msitake kufanya mambo yote kama jukwaa la jamiiforums ambako kila mwenye simu janja basi ni mjuaji wa kila jambo.
Tulieni na muache mihemko.
Pambaneni na kutafuta riziki kulisha familia zenu.
Bila utaratibu kufuatwa kila mtu atakuwa msemaji wa serikali ebo!
Hayo mambo yako kwa mama Dangote tu.
Serikali ina kitu inaitwa collective responsibility!
Sisi tunasikiliza wananchi na siyo misukule ya kisiasa! samahani bi kidude gwaji girl! We have everything now You can go to hell! You dont care about us but your damn tumbo street!Mkuu wa mkoa wa Mbeya Chalamila na mbunge wa Chunya wamezuru kijiji cha Ifumba wilayani Chunya kupata taarifa za ugonjwa usiojulikana.
Wananchi wamesema ugonjwa huo ni kweli upo na umeshaua watu zaidi ya 30 na kwa sasa kuna wagonjwa 22 ambao wamelazwa na wengine wanaugulia majumbani.
Ndipo mbunge wa Chunya akamuomba RC Chalamila aingilie kati swala hilo kwani wapiga kura wake wanateketea.
RC Chalamila akatoa agizo kwa mganga wa wilaya kuhakikisha wagonjwa wote 22 wanapelekwa hospitali ya Rufaa Mbeya kwa uchunguzi zaidi na matibabu.
Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
Aliekuambia utuoe maoni nan? Umeona ni Mercury ?? Umethibitisha??Msipendelee sana kuweka chumvi kwenye mambo ambayo hatuna uhakika nayo - mfano: nani kadhibitisha kwamba Ifumbo kuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola??
Kwani nani aliona wagonjwa wakitokwa damu masikioni,puani na kwenye macho?
Tumeambiwa ugonjwa huu unalikuwepo on and off tangu 1996 na wala Chunya haipakani ni jimbo la Congo DRC lenye matatizo ya ugonjwa huo.
Tukumbuke kwamba Chunya wachimbaji dhahabu wadogo wadogo wantumia sana zebaki(mercury)kusafishia dhababu, ni rahisi mercury vapour (mvuke) kuadhili mwili, mapafu na mfumo wa digestive systems - mvuke wa mercury unabaki kwenye nguo,hair na kuchani na kwenye viazio vya maji - wakimwaga mabaki ya mercury yanaingia aridhini mvua ikinyesha inasafirisha mabaki kwenyevianzio vya maji ya kunywa, kuogea na kufuria - maoni yangu.
Aliekuambia utuoe maoni nan? Umeona ni Mercury ?? Umethibitisha?