Serikali yatoa tahadhari ya Homa ya Manjano

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) ambapo amesema tarehe 03 Machi 2022 Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka WHO hapa nchini ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Kenya.

Amesema hadi kufikia tarehe 03 Machi 2022 nchini Kenya kulikuwa na wagonjwa wa Homa ya manjano 15 na vifo vitatu (3), Aidha ktk sampuli sita zilizopimwa maabara ya Kenya kwa kutumia vipimo vya serology na PCR sampuli 3 zilithibitika kuwa na maambukizi.

Ameeleza, "Hapa nchini taarifa ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita ktk mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa zinaonesha kuwa hakuna taarifa zinazoashiria kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya manjano, pia taarifa za ufuatiliaji wa tetesi za magonjwa haujaashiria kuwepo kwa ugonjwa huo"

Ameagiza Hospitali zote za Rufaa nchini kuwa na huduma za kupima na kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri na wenye uhitaji na pia ameagiza maafisa wa afya mipakani kuhakikisha wasafiri wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi wanakua na vyeti vya chanjo.

Ameongeza, "Tutaboresha mifumo ya kutoa vyeti vya kielektroniki vya homa ya manjano mipakani ili kuzuia udanganyifu unaoweza kufanywa na maafisa kuwapa vyeti watu ambao hawajachoma chanjo"

Waziri Ummy amewataka wananchi kuchukua tahadhari, na kujua dalili za ugonjwa wa homa ya manjano kama homa, kuumwa kichwa, maumivu ya misuli na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika, mwili kuwa na manjano, kutokwa na damu sehemu za wazi.

Chanzo: Wizara ya Afya
 
Hivi tunatakiwa kukagua mtu ambae ana chanjo ya hiyo homa au mtu ambae ana recent negative test? Mbona mi sielewi jamani?
 
Jiwe angesema sisi Tanzania Mungu wetu atatuokoa. Angekosoa viongozi wa dini na Umy Mwalimu angetumbuliwa maana ni jipu.
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) ambapo amesema tarehe 03 Machi 2022 Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka WHO hapa nchini ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Kenya.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alitolewa wizara ya afya na JPM na Samia.

Sasa samia kamrudisha tena wizara ya afya.
Ni nini kilichotokea? Mbona ninaona wazi kuwa samia alikuwa msaliti wa JPM?
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) ambapo amesema tarehe 03 Machi 2022 Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka WHO hapa nchini ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Kenya.

Amesema hadi kufikia tarehe 03 Machi 2022 nchini Kenya kulikuwa na wagonjwa wa Homa ya manjano 15 na vifo vitatu (3), Aidha ktk sampuli sita zilizopimwa maabara ya Kenya kwa kutumia vipimo vya serology na PCR sampuli 3 zilithibitika kuwa na maambukizi.

Ameeleza, "Hapa nchini taarifa ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita ktk mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa zinaonesha kuwa hakuna taarifa zinazoashiria kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya manjano, pia taarifa za ufuatiliaji wa tetesi za magonjwa haujaashiria kuwepo kwa ugonjwa huo"

Ameagiza Hospitali zote za Rufaa nchini kuwa na huduma za kupima na kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri na wenye uhitaji na pia ameagiza maafisa wa afya mipakani kuhakikisha wasafiri wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi wanakua na vyeti vya chanjo.

Ameongeza, "Tutaboresha mifumo ya kutoa vyeti vya kielektroniki vya homa ya manjano mipakani ili kuzuia udanganyifu unaoweza kufanywa na maafisa kuwapa vyeti watu ambao hawajachoma chanjo"

Waziri Ummy amewataka wananchi kuchukua tahadhari, na kujua dalili za ugonjwa wa homa ya manjano kama homa, kuumwa kichwa, maumivu ya misuli na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika, mwili kuwa na manjano, kutokwa na damu sehemu za wazi.

Chanzo: Wizara ya Afya
Eti ni kweli chanjo ya homa ya manjano inatolewa bure?
 
Back
Top Bottom