Serikali yaipa TCU bilioni 6.1 kuimarisha ubora vyuo vikuu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
SERIKALI imeipatia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Sh. bil 6.4 kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa ajili ya kuimarisha uthibiti ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu ambapo zaidi ya mitaala 300 ya vyuo vikuu iko katika hatua mbalimbali za kufanyiwa mapitio ili kuhuishwa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa wakati akieleza kuhusu mafanikio ya tume hiyo katika mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma.

Profesa Kihampa amesema mafanikio mengine kuwa ni kuendelea kuandaa na kuratibu mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa viongozi na wanataaluma wa vyuo vikuu kuhusiana na uendeshaji wa vyuo vikuu, utengenezaji mitaala inayozingatia ujuzi na inayoendana na soko, mbinu za ufundishaji kwa Wahadhiri ambao hawakusoma fani za ualimu, ulinganifu wa programu za masomo, uthibiti ubora na utengenezaji na utumiaji wa mifumo ya kompyuta.

Aidha, amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba, 2022, jumla ya viongozi na wanataaluma 575 wameshanufaika na mafunzo hayo ambayo yamelipiwa na Serikali kwa asilimia 100.

Chanzo: Nipashe
 
Wananchi kuajiri vijana wapo wanagawa pesa tu ziliwe , waboreshe vyuo au waibe

USSR
 
Back
Top Bottom