Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Wakati wa mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (TAHLISO) uliofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma jana, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeanza kujenga kampasi za vyuo vikuu katika mikoa mbalimbali ukiwemo Kigoma, Tabora, Singida, Tanga, Ruvuma, Kagera ili kutoa fursa kwa watoto wa Kitanzania kupata elimu ya juu.
Pia alisema serikali itajenga jumla ya vyuo vya ufundi stadi (VETA) 65 ambapo vyuo 64 vitajengwa katika wilaya 64 ambazo hazina VETA na kimoja cha mkoa kitajengwa mkoani Songwe.
Ameeleza kuwa Serikali imeamua kujenga kampasi hizo katika maeneo hayo 14 ambayo hayana kampasi ili kuwawezesha watoto wa kitanzania kupata elimu bora.
Vilevile Profesa Mkenda alisema serikali pia imetenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha wahadhiri wa vyuo vikuu vya serikali na binafsi ambapo dola milioni moja imetengwa kwa ajili ya kuwaendeleza kilimo wahadhiri katika vyuo binafsi.