Katibu Idara ya Mahusiano ya Kimataifa Vyuo na Vyuo Vikuu Akutana na mlezi, viongozi wa serikali ya wanafunzi na viongozi wa UVCCM

Shabani Ajaha

Member
Aug 18, 2021
78
60
*NDG. MARTINE AKUTANA NA MLEZI, VIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI NA VIONGOZI WA UVCCM TAWI LA CITY COLLEGE MIKWAMBE.

Juni 22, 2023.
Upanga, Dar es Salaam.

Katibu Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Ndg. Emanuel Martine, amefanya mazungumzo na Walezi, Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi na Viongozi wa Tawi la UVCCM City College Mikwambe katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2023.

Lengo la mazungumzo hayo ni kusikiliza na kupokea mawazo na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wa City College Mikwambe na vyuo vya kati Kada ya Afya na kushauriana namna bora ya kuzitatua.

Ndg. Martine, amempongeza sana Mkuu wa Chuo cha City College Mikwambe pamoja na Mlezi wa Tawi la UVCCM kwa Mahusiano mazuri waliyonayo na Tawi la UVCCM City College na kuwaomba waendelea kuwalea na kuwashauri vyema vijana hao kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla.

City College Mikwambe (Tawi la UVCCM na Serikali ya Wanafunzi) mmekuwa washiriki wakubwa katika matukio mbalimbali ya Chama na Serikali endeleeni na mwendo huo huo bila kusahau dhamira iliyowapelska hapo chuoni. Endeleeni kuweka misingi Imara ya kuendelea kuwavuna na kuwashawishi Vijana wengi zaidi wajiunge na Chama cha Ukombozi Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ndg. Martine, amewasisitiza Viongozi hao kuendelea kuishi katika misingi bora ya Uongozi na kufanya maamuzi kwa mujibu wa makubaliano ya vikao na sio kuwa na maamuzi binafsi ili kuepusha migogoro isiyokuwa na lazima.

Aidha Ndg. Martine, ametumia muda huoa kutoa salamu za Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Mohammed Ali KAWAIDA (MCC) na kusema ya kwamba Cde. Kawaida anatambua uwepo wenu hapa Ofisini leo anawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM) huko vyuoni.

"Taifa letu asilimia kubwa ni Vijana ambao ndio walinzi wa Chama na Serikali tunawajibu mkubwa wa kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mhe. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa namna anavyoendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-25 yenye kurasa 303 kwa nia ya kuleta Maendeleo.

"Tumieni taaluma na maarifa yenu kutatua Changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii na kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu kada ya Afya hasa pale wanapotokea Maharamia wa mitandao kutumia mitandao yao kupotosha Umma wa Watanzania.

Mwisho Ndg. Matine amemaliza kwa kuwaachia Viongozi hao mambo matatu 3 (Majukumu 3) ambayo wakiyafanya kwa ufanisi basi watakuwa wamepiga hatua:-
1. Kukijenga na kukilinda Chama cha Mapinduzi (CCM)
2. Kuwa na Maadili Mema na nidhamu katika kutimiza majukumu hao.
3. Kutimiza wajibu kwa ukamilifu.

Imetolewa na
Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM.

IMG-20230622-WA0457.jpg
 
Back
Top Bottom