Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 19
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imebainisha kuwa hadi kufikia Juni mwaka huu, shule za msingi zilikuwa na walimu wapatao 58 wenye Shahada ya Udakatari wa Falsafa (PhD) wakati walio na Shahada ya Uzamili ni 75, Shahada ya Kwanza 1,099 na Stashahada ya Ualimu ni walimu 6,512.
Hata hivyo, pamoja na makundi hayo matatu, pia imeonesha kuwa idadi ya walimu wa Daraja la Tatu A ni 148,986 na wa Daraja B na C idadi yao ni 9, 123 sawa na asilimia 5.8 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya BEST 2006-2010.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu katika Wizara hiyo, Rose Massenga, alibainisha hayo Novemba 8 wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Jumanne Sagini, kufungua mkutano wa wakuu wa vyuo vya ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali mjini hapa.
Kwa mujibu wa Masenga, upande wa walimu wa shule za sekondari wanaofundisha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, wenye Shahada ni 9,910, Stashahada 22,171, wenye leseni ni 3,997 sawa na asilimia 12.46 na wengine 4, 439 sawa na asilimia 13.84.
Hata hivyo, alisema mahitaji ya walimu wa elimu ya awali na msingi kwa mujibu wa PEDP katika mwaka 2010 hadi 2011, wanahitajika walimu 18, 783 kati ya hao 15, 783 ni wa msingi na 3,000 wa elimu ya awali, ambapo elimu ya sekondari kwa kipindi hicho wanahitajika walimu 30,075.
Alisema mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya msingi na ule wa elimu ya sekondari, imesababisha ujenzi wa shule nyingi za msingi na sekondari uliambatana na uandikishaji wa wanafunzi wengi kwenye ngazi hizo na matokeo yake kusababisha mahitaji makubwa ya walimu.
Hivyo alisema ni vyema ieleweka kuwa msimamizi wa utoaji wa mafunzo ya ualimu unazingatia mambo mengi vikiwemo sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayoelezeka katika viwango vya kitaifa na kimataifa.
Naye mgeni rasmi, Sagini alisema shule za msingi zina uhaba wa walimu wasiopungua 45,000, wakati upungufu ni mkubwa zaidi kwa sekondari katika masomo ya sayansi.
Hata hivyo, alisema ngazi ya elimu ya msingi idadi ya wanafunzi imeongezeka maradufu kutoka milioni nne mwaka 2001 hadi milioni 8.4 mwaka 2010, ambapo shule za sekondari idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka chini ya 300,000 mwaka 2001 hadi milioni 1.6 mwaka 2010.
Sagini alisema wakati idadi ya wanafunzi ikiongezeka kwa kiwango hicho kikubwa, idadi ya walimu imekuwa ikiongezeka kwa kiasi kidogo ambacho hakitoshelezi mahitaji ya ngazi ya msingi na sekondari.
Pamoja na hayo, amekipongeza Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kupendekeza na kukubaliana kutafakari hoja ya kuimarisha mafunzo ya ualimu na kupata utaratibu wa mafunzo ya ualimu ulio bora zaidi utakaowezesha kufanikisha malengo ya elimu kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vya ualimu na vyuo vikuu.