Serikali yabainisha walimu 58 wenye PhD shule za msingi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yabainisha walimu 58 wenye PhD shule za msingi!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Ustaadh, Nov 9, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imebainisha kuwa hadi kufikia Juni mwaka huu, shule za msingi zilikuwa na walimu wapatao 58 wenye Shahada ya Udakatari wa Falsafa (PhD) wakati walio na Shahada ya Uzamili ni 75, Shahada ya Kwanza 1,099 na Stashahada ya Ualimu ni walimu 6,512.

  Hata hivyo, pamoja na makundi hayo matatu, pia imeonesha kuwa idadi ya walimu wa Daraja la Tatu A ni 148,986 na wa Daraja B na C idadi yao ni 9, 123 sawa na asilimia 5.8 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya BEST 2006-2010.

  Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu katika Wizara hiyo, Rose Massenga, alibainisha hayo Novemba 8 wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Jumanne Sagini, kufungua mkutano wa wakuu wa vyuo vya ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali mjini hapa.

  Kwa mujibu wa Masenga, upande wa walimu wa shule za sekondari wanaofundisha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, wenye Shahada ni 9,910, Stashahada 22,171, wenye leseni ni 3,997 sawa na asilimia 12.46 na wengine 4, 439 sawa na asilimia 13.84.

  Hata hivyo, alisema mahitaji ya walimu wa elimu ya awali na msingi kwa mujibu wa PEDP katika mwaka 2010 hadi 2011, wanahitajika walimu 18, 783 kati ya hao 15, 783 ni wa msingi na 3,000 wa elimu ya awali, ambapo elimu ya sekondari kwa kipindi hicho wanahitajika walimu 30,075.

  Alisema mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya msingi na ule wa elimu ya sekondari, imesababisha ujenzi wa shule nyingi za msingi na sekondari uliambatana na uandikishaji wa wanafunzi wengi kwenye ngazi hizo na matokeo yake kusababisha mahitaji makubwa ya walimu.

  Hivyo alisema ni vyema ieleweka kuwa msimamizi wa utoaji wa mafunzo ya ualimu unazingatia mambo mengi vikiwemo sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayoelezeka katika viwango vya kitaifa na kimataifa.

  Naye mgeni rasmi, Sagini alisema shule za msingi zina uhaba wa walimu wasiopungua 45,000, wakati upungufu ni mkubwa zaidi kwa sekondari katika masomo ya sayansi.

  Hata hivyo, alisema ngazi ya elimu ya msingi idadi ya wanafunzi imeongezeka maradufu kutoka milioni nne mwaka 2001 hadi milioni 8.4 mwaka 2010, ambapo shule za sekondari idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka chini ya 300,000 mwaka 2001 hadi milioni 1.6 mwaka 2010.

  Sagini alisema wakati idadi ya wanafunzi ikiongezeka kwa kiwango hicho kikubwa, idadi ya walimu imekuwa ikiongezeka kwa kiasi kidogo ambacho hakitoshelezi mahitaji ya ngazi ya msingi na sekondari.

  Pamoja na hayo, amekipongeza Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kupendekeza na kukubaliana kutafakari hoja ya kuimarisha mafunzo ya ualimu na kupata utaratibu wa mafunzo ya ualimu ulio bora zaidi utakaowezesha kufanikisha malengo ya elimu kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vya ualimu na vyuo vikuu.
   
 2. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Give me a break!!!! PhD wanafundisha promary schools au sijakuelewa?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  not understand...au kiiengli swahili kigumu
   
 4. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,402
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  PhD..............!!!!!!!!!!! .............Primary................!!!!!!!!!!!!!! there must be a typing error somewhere............
   
 5. B

  Bobby JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Its possible mkuu, what if ni kama ile ya jk? zote c ni PhD jamani au?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  SURE!
  NI SHULE GANI HIZO na ziko wapi?
  This is like a fairy tale!
   
 7. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  USTAADH hebu tufafanulie hizo PhD zinazofundisha Shule za msingi wakati baadhi ya Universities wanatafuta
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  hapo napo
   
 9. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wala usishangae, hawa ni watanzania wajariamali wenye PhD ambao wamewekeza katika sekta ya elimu na kufungua shule za msingi (English Medium, St Mama Mdogo etc) ambao katika kuwasilisha orodha za waalimu, wameweka na majina yao!! Unashangaa nini, mbona kuna Dispensary zina waganga ambao ni Professors? Yaani watanzania Professors wajariamali ambao wamewekeza katika sekta ya afya na kufungua dispensaries ambao katika kuwasilisha orodha za waganga wakaweka majina yao! Ukitaka kushangaa ya Musa nenda huko shuleni/dispensary kama utawakuta wakifanya kazi, wanaofundisha huko ni walimu wa kawaida (UPE with long experience, Grade A, Diploma etc) / wanaotibu huko ni waganga wa kawaida (Medical Assistants. Assitant Medical Officers etc) . Wao ni owners, please, give me a break!
   
 10. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Originally Posted by StaffordKibona [​IMG]
  USTAADH hebu tufafanulie hizo PhD zinazofundisha Shule za msingi wakati baadhi ya Universities wanatafuta  hapo napo  Bongo zipo hizi jamani, mnasahau Open university wanatoa PhD! Hizi ndo PhD za hawa walimu wa primary. I am sure if they are confident enough that they hold PhD, they would not continue to be where they are.
   
 11. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mama Mdogo,
  Hao wajasiriamali wenye St. Mama wewe, hawafundishi wao, wao wanakusanya mafungu tu.Wenyewe wanashughuli zao zenye fungu nene, tena wengine ni waheshimiwa. Hata hizo dispensari waganga ni wale wale wa Mount Meru, muhimbili, Meta na rufaa, Morogoro,Dodoma na Mawenzi. asubuhi hospitali ya serikali jioni kwa wajasiriamali. So hakuna phd,masters,degree wala diploma huko shule za msingi hata za magumashi kama za watu fulani.
   
 12. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Good explanation! unanikumbusha enzi hizo kampuni yetu ikiomba consultancy, kwenye CV za team members tunaazima mpaka majina ya PHD holders halafu mkienda field wanashangaa huyo DR. anakuja siku ya kwanza siku zinazofuata kazi inapigwa na nyoka (diploma/bachelor holders).....uchakachuaji uko kila kona, sijui kama tutaendelea siye wabongo!
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Nasikia hata Bank Tellers wenye PhD nao wapo!!! lol; heri niingie kwenye movie sasa!!!
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kuna mpaka mama wa nyumbani wenye Phds mbona. Wanawake na phds zao ambao wamefungua makampuni yao kwenye mikoba na muda mwingi wako kwenye mizunguko ya kazini, lakini kwa vile hawana address maalum, utasikia mama wa nyumbani.

  takwimu zilizokuwa hazijafanyiwa analysis ya kutosha ndio kaa hizi.
   
 15. s

  sha Senior Member

  #15
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35  nafikiri ni kutokana na hivyo ndio maana examiner,s report inaonyesha darasa la saba wanamaliza wakiwa hawajui kusoma wala kuandika
   
 16. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Bongo zipo hizi jamani, mnasahau Open university wanatoa PhD! Hizi ndo PhD za hawa walimu wa primary. I am sure if they are confident enough that they hold PhD, they would not continue to be where they are. [/QUOTE]

  Kwani PhD za Open University ni tofauti na zingine?
   
 17. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,593
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Hii kasumba ya ubwana mkubwa katika maisha ni mbaya kwelikweli.
  sasa ni nini cha ajabu hapo mtu mwenye PHD kuwa mwalimu wa primary?. vipi kuhusu mapenzi ya mtu binafsi kufundisha?, vipi kuhusu ile hisia za kupenda kuwasaidia wengine, hususan watoto wadogo?.

  Jamani elimu ni kwa ajili ya huduma, na pale mtu anapotoa huduma hivi kweli inafaa adharauliwe au apongezwe?.
  kwa taarifa zenu siyo kila mwenye phd anaweza kufundisha vyuoni.
   
 18. October

  October JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unadhani kwenye Movie ndio hakuna uchakachuaji?
  Jaribu utajionea mwenyewe....
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mama Mdogo,

  Hivi mmiliki wa Shule anaweza kuwa kwenye list ya waajiriwa wa shule "as a member of staff"?

  Kwahiyo wakija wakaguzi naye anakaguliwa "Kitabu cha Maadalizi ya somo e.t.c"!

  Kweli Tanzania hakuna lisilowezekana!
   
 20. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  What is the difference between Harvard PhD and Open University PhD? especially when the OUT PhD is not honorary one like Boyz II Men ones :lalala::lalala:
   
Loading...