Tumuomboleze Lowassa bila unafiki. Shule za kata ulikuwa uamuzi wa CCM

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,227
5,950
Kunatofauti ya kuamua na kusimamia maamzi. Ujenzi wa shule za kata nchi nzima ulikuwa uamuzi wa CCM na ulikuwa kwenye ilani ya uchaguzi 2005-2010
USHAHIDI HUU HAPA
Elimu ya Sekondari

61. CCM itazielekeza Serikali kuchukua hatua za kuendeleza elimu ya sekondari katika kipindi cha 2005 - 2010 kama ifuatavyo:-

(a) Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES

(b) Kuendelea kutekeleza azma ya kuwa na angalau shule moja ya sekondari kwa kila Kata.

(c) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa Kidato cha 1-4 kufikia asilimia 50 ya watoto wa rika lengwa la umri wa miaka 14-17 ifikapo mwaka 2010.

(d) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa Kidato cha 5-6 kufikia asilimia 25 ya vijana wa rika lengwa la umri wa miaka 18-19 ifikapo mwaka 2010.

(e) Kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari na kuongeza viwango vya kufaulu katika Kidato cha 4 na cha 6.

(f) Kujenga nyumba za walimu na kuendelea kuboresha maslahi yao.
 
alisaidia kusukuma gurudumu la ilani ya chama na huu ndio uzuri wa chama cha mapinduzi kuna watu ni kama makonda anavyo lisukuma gurudumu kwa sasa
 
wivu tu unakusumbua kama mtoto wa kike
Aliyofanya magu,na sasa samia yote yapo kwenye ilqni na wanasifiwa
Viongozi wapo kwa ajili ya kutekeleza ilani ata watumishi wa serikali wanatekeleza ilani ya chama kilicho madarakani
 
Wivu huoo...ENL ni Jembe sana kwenye hilo....kasimamia shule za kata zoote..kwa kasi....alitaka amalizemaabara ahamie kwenye vituo vya afya....

..
 
Afadhali ya wivu kuliko wewe uliyekuwa unamtukana kama hawa watu hapa

1707717868594.png

wivu tu unakusumbua kama mtoto wa kike
Aliyofanya magu,na sasa samia yote yapo kwenye ilqni na wanasifiwa
Viongozi wapo kwa ajili ya kutekeleza ilani ata watumishi wa serikali wanatekeleza ilani ya chama kilicho madarakani
 
Wivu huoo...ENL ni Jembe sana kwenye hilo....kasimamia shule za kata zoote..kwa kasi....alitaka amalizemaabara ahamie kwenye vituo vya afya....

..
Kwenye kusimamia nakubaliana na wewe kabisa- ILA UAMUZI ulikuwa wa CCM
 
Kwenye kusimamia nakubaliana na wewe kabisa- ILA UAMUZI ulikuwa wa CCM
Ilani ina kila kitu....uthubutu na kupambania ndio suala hapa.....Hata Kuhamia Dodoma ni uthubutu ule.....hapo utasemaje
 
Kunatofauti ya kuamua na kusimamia maamzi. Ujenzi wa shule za kata nchi nzima ulikuwa uamuzi wa CCM na ulikuwa kwenye ilani ya uchaguzi 2005-2010
USHAHIDI HUU HAPA
Elimu ya Sekondari

61. CCM itazielekeza Serikali kuchukua hatua za kuendeleza elimu ya sekondari katika kipindi cha 2005 - 2010 kama ifuatavyo:-

(a) Kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES

(b) Kuendelea kutekeleza azma ya kuwa na angalau shule moja ya sekondari kwa kila Kata.

(c) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa Kidato cha 1-4 kufikia asilimia 50 ya watoto wa rika lengwa la umri wa miaka 14-17 ifikapo mwaka 2010.

(d) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa Kidato cha 5-6 kufikia asilimia 25 ya vijana wa rika lengwa la umri wa miaka 18-19 ifikapo mwaka 2010.

(e) Kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari na kuongeza viwango vya kufaulu katika Kidato cha 4 na cha 6.

(f) Kujenga nyumba za walimu na kuendelea kuboresha maslahi yao.
Ndungu ENL alilisimamia hili kikamilifu sana, lakini pia suala la Tanzania ya viwanda lilikuepo kwenye ilani ya 20215-2020 na wahusika walijitahidi pia kusimamia utekelezaji wake 🐒

kila zama na kitabu chake....
maisha ni kitabu,
jitahidi kuishi vizuri ili kitabu chako kiwe na hadithi mzuri 🐒

R.I.P Laigwanan comrade EL
 
Kwani kuna mtu anasema shule za kata lilikuwa wazo la Lowassa? Kinachosifiwa hapa na kupongezwa ni uimara katika utekelezaji.

Leo hii mbona ilani ina mambo mengi, ni lipi limetekelezwa likaonekana?

Viongozi wa nchi hii wanayo mengi sana ya kujifunza kutoka kwa Lowassa, alikuwa waziri mkuu kwa muda mfupi sana ila alikuwa waziri mkuu kweli kweli! Sio hawa mawaziri wakuu wa sasa, kila baada ya neno moja utasikia "tunamshukuru mhe. Rais kwa kufanya hili kwa kufanya lile"

Nina mashaka pia kitendo cha Lowassa kuyatumia mamlaka ya waziri mkuu kama anavyotakiwa ndio ilileta wivu kwenye taasisi ya Urais!
 
hata kama ni ilani kuna mtu alikuwa champion ktk hilo nae ni Lowasa!
UDOM pia Lowasa alikuwa Champion na ndio ukweli!
Hata mkataba wa Richmond Lowasa aliukataa lkn alikuja kudondoshewa jumba bovu na rafili yake.
Hata mikataba mibovu ya GAS awamu ya 4 angekuwepo Lowasa kama waziri Mkuu asingekubali!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe!
 
Unapataga nini kuwashambulia marehemu?🐼

Rip Edward Lowasa

Rip Shujaa Magufuli

Rip Maalim Seif

Rip Kamilius Membe

Rip Anna Mgwhira
 
Lakini pamoja yote CCM ndio waliomloga Lowassa na yale maradhi ya kutetemeka kipindi cha kampeni na baada ya kushinda Uchaguzi na kuzulumiwa ushindi sikuona tena kule kutetemeka.

CCM acheni Ulozi.
 
Back
Top Bottom