Serikali Yaahidi Kuchukua Kali za Kisheria kwa Mabaraza Yanayofanya Maamuzi ya Migogoro ya Ardhi kwa Mienendo ya Rushwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,987
960

SERIKALI YAAHIDI KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA MABARAZA YANAYOFANYA MAAMUZI YA MIGOGORO YA ARDHI KWA MIENENDO YA RUSHWA

"Lini Serikali itahamisha Mabaraza ya Ardhi kwenda kwenye mfuko wa Mahakama?" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Katika jitihada za kuboresha mfumo uliopo wa utatuzi wa migogoro ya Ardhi nchini, Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa mapendekezo ya kuhamisha shughuli zinazofanywa na Mabaraza ya Ardhi na nyumba ya Wilaya kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda Katika muhimili wa Mahakama. Taratibu zitakapokamilika Serikali italijulisha Bunge tukufu" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

"Wilaya ya Rorya haina Baraza la Ardhi la Wilaya, jambo hili hupelekea wananchi kusafiri umbali mrefu zaidi ya KM 60 mpaka KM 100 kwenda Tarime kupata huduma. Kutokana na umbali mrefu Wakati mwingine wananchi hukata tamaa kufuatilia haki zao za Kimsingi na kisheria za utatuzi wa migogoro ya Ardhi. Je, Waziri huoni kuna umuhimu wa kuanzisha Baraza la Ardhi la Wilaya ya Rorya? Kumekuwa na minong'ono mingi ya wananchi Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwenye utatuzi wa migogoro kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya. Nataka kujua mpango mkakati wa Serikali kuhakikisha vitendo hivi vya rushwa vinavyonyima haki kwa wananchi, Serikali mmejipanga vipi kushughulikia ili wananchi wapate haki zao za Kimsingi?" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Nia ya kuanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya yalikuja Wakati wa ripoti ya Prof. Issa Shivji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya kutatua migogoro ya kisheria katika kipindi ambacho Mahakama zilikuwa ufanisi wa kutosha. Kwa sasa Mahakama zimeboreka sana, zina mifumo ya kisasa na zimesambaa nchi nzima na ndiyo nia ya Serikali kuondosha Mabaraza ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi kupeleka kwenye Wizara ya Sheria na Katiba chini ya Muhimili wa Mahakama" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

"Nikiri kumekuwa na malalamiko mengi hata kwa waheshimiwa wabunge ya tuhuma za rushwa kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya. Wizara ilishatoa taarifa kwenye Kamati ya Bunge. Tutakapopata taarifa mahususi za Baraza ambalo limefanya shauri kwa kutumia maamuzi ambayo yanaonekana yameshawishiwa na rushwa tutachukua hatua. Nakubaliana na Mhe. Jafari Chege, Wizara inaendelea na taratibu ya kuongeza Wenyeviti wa Mabaraza na mpaka sasa tun Wilaya 36 ambazo hazina Mabaraza ikiwemo Wilaya ya Rorya na Tutakapopata Mwenyekiti tutampeleka na Baraza la Ardhi Rorya litaanzishwa" - Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

ielaYgTU_400x400.jpg
maxresdefaultvbghtyujk.jpg
 
Back
Top Bottom