mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Baada ya Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa kuonesha mwanga katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, kuna waliodai kuwa anafanya kazi ambayo ingefanywa na mahakama yenye jukumu la kutafsiri sheria hivyo anachofanya ni sawa na kazi bure. Hivyo kumtaka kuanzia mahakamani katika kutatua migogoro ya ardhi.
Waziri Silaa amefafanua kuwa katika Sekta ya ardhi ina jukumu la kitu kinaitwa administrative justice (inatoa haki ya kiutawala)
Ameongeza kuwa, yapo mambo na wataalam wa wizara ya ardhi ameshawaagiza waache tabia ya kugeuka washauri wa sheria wa wananchi.
Anasema unakuta raia anakuja na vielelezo vyote muhimu vya umiliki wa ardhi, lakini eneo lake anakalia mtu mwingine, hivyo anavyokutana na wataalam wa wizara, badala ya kutoa haki ya kiutawaka, wanageuka kuwa washauri wa sheria wanawaambia wananchi waende mahakamani, ameongeza kuwa jambo hilo ameshalipiga marufuku.
Waziri Silaa amezidi kusema kwakuwa mahakama inasikiliza kila mtu, hivyo wapo watu ambao hutumia mwanya huo kuchelewesha haki za wengine au kuwasumbua watu wengine hasa ambao hawajui sheria au hawana nguvu ya kupambana kimahakama. Hivyo suala hilo ni misuse of court process.
Amemalizia kwa kusema kuwa Wizara ya Ardhi itamsikiliza mwananchi yeyote na maadam atakuwa na vielelezo vyote na pale penye haki za watu watazitoa.