Serikali yaagiza Mtoto Charles Mathias arushwe Darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada

Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza baada ya kuonyesha kipaji kikubwa kwenye somo la Hisabati.

Afisa tawala wa mkoa bwana Kobehelo amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale ameahidi kugharamia elimu ya mtoto huyo hapo kijijini.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Mwanangu ana miaka 6 na yupo darasa la pili
Baasi na yeye namuweka kundi moja na mtoto mwenye kipaji .
This world isn't fair. Nahisi alitakiwa kurushwa labda mpaka la tatu huko
 
Babu Tale agharamie nini tena wakati elimu ni bure?
Jaribu kuficha ujinga wako mkuu.
Kama aufuatilii habari kuwa kimyaa.
Babu tale alishasema tangu Awali atamsomesha St mary morogoro au nayo ni Bure?
 
Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza baada ya kuonyesha kipaji kikubwa kwenye somo la Hisabati.

Afisa tawala wa mkoa bwana Kobehelo amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale ameahidi kugharamia elimu ya mtoto huyo hapo kijijini.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Tale nae aache sifa sasa ada gani kwa shule ile? Yeye akajenge madarasa tu
 
Mwanangu ana miaka 6 na yupo darasa la pili
Baasi na yeye namuweka kundi moja na mtoto mwenye kipaji .
This world isn't fair. Nahisi alitakiwa kurushwa labda mpaka la tatu huko
Hajui kusoma wala kuandika anapelekwa vipi darasa la tatu mkuu?
 
Mwalimu wake wa darasa alinukuliwa akisema pamoja na dogo kuwa fiti hesabu ila hajui kuandika. Badala ya kumrusha rusha dogo na kumtoa mazingira aliyozoea ingekuwa busara kama hiyo hiyo shule iboreshwe. Anawezwa pelekwa shule nyingine mazingira tofauti akawa wa kawaida sana. Mazingira is everything!
 
Back
Top Bottom