Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Mtoto Charles Mathias Mbena(6) mkazi wa Kibungo Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ameonesha kipaji cha hesabu ambapo anaweza kujumlisha na kutoa hesabu za makumi na malaki bila kutumia karatasi.
Mtoto huyo anayesoma darasa la awali katika Shule ya Msingi Nyigwa ametakiwa kufanyiwa majaribio ili kumpeleka katika Shule na darasa analostahili.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuele Kalobelo amesema wamegundua ana kipaji hivyo watamfanyia majaribio.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala ameelezea azma yao ya kuboresha mazingira ya Shule ya Msingi Nyigwa kwa kuijengea madarasa manne mbali na mawili ambayo yanamaliziwa na Mkurugenzi.
Pia soma: Serikali yaagiza mtoto Charles Mathias arushwe darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada