Serikali yaagiza Mtoto Charles Mathias arushwe Darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada

unaendeleaje hapo kitengo cha utafiti NIMR
NIMR tena? :D
Unanionea,

Mimi nipo napangisha vyumba na kuuza Viwanja huku Buza, kwaMnyamani,Salanga,Mavurunza,KwaTumbo,UwanjawaFisi karibia na Kilimahewa upande wa Boko Nemela ingawa natembeatembea hadi Mwasonga, Vianzi pia.

Hata sijui Function,Set,Circle wala Pai inanipatiaje Tonge usawa huu.
 
Kweli Nina mjukuu WA dada yangu miaka mitano anaandika makolokocho anaenda shule kucheza Tu hajui chochote muda wote analia Ile ya kudeka. Huyu WA miaka mitatu anaamka ananawa anaenda shule umbali mrefu. Alirudi anasema anabadili nguo, anakula anakaa. Malezi mazuri hakuna mfano. Yaani mtoto huyu na wazazi wake wamekosha.
 
Shule yenyewe anayosoma haina madarasa wanaosomea kwenye pagala, halina madawati wanakaa kwenye mawe.

Halafu mbunge wao anasema atamgharamia masomo wakati hata kuboresha shule ameshindwa.

Hebu jiulize kuna magenius wangapi wanapotelea kwenye hayo mapagala yanayoitwa shule huko mikoani ?
Aiseee......
 
Hapo ajaruka kuruka angetoka chekechea hadi la 2 na kuendelea ikiwa na maana karushwa drs la kwanza sasa kutoka chekechea kwenda la kwanza karuka darasa gani najaribu kuwaza.
nchi confusion tupu.Nchi za wenzetu ni kawaida kabisa mtoto wa miaka sita darasa la kwanza.Anahitimu chuo kikuu miaka 20 ,21.
 
Atachangia 300 za uji
..
giphy.gif
 
Babu Tale agharamie nini tena wakati elimu ni bure?
Elimu sio bure mkuu,hizo ni lugha za kisiasa, elimu ilikuwa bure zamani, ambapo mzazi alikuwa ananunua uniform tu. Kuna madaftari, kalamu na vifaa vingine vya shule, school uniforms, madawati, michango ya chakula cha mchana, michango ya ujenzi wa madarasa, michango ya ujenzi wa vyoo vya shule nk. nk.
 
Huyo mtoto kuandika hajui, wangemuacha kwanza ajue kuandika ndiyo wamrushe.
 
Hao wanavuta bangi Yaani chekechea to primary ndio kurushwa darasa

Kwa iq ya yule mtoto alipaswa kurushwa mpaka darasa la 3 huko
Hajui kuandika bado hata kusoma yeye ni kichwani sasa atasoma vipi vitabu my dear
 
Nakumbuka kuliwahi kuweko shule za watoto wenye vipaji. Ila ziliishia viongozi kujaza watoto wao wasio na vipaji.Tusirejee Zama hizo.
Tena watoto mbulula ndiyo waliwajaza hapo, mkuu umasikini mbaya sana wenye pesa wanawapeleka popote pale watoto wao, huyo mtoto angekuwa mtoto wa mwenye nazo miaka 6 si angekuwa mbali siku hizi miaka 5 yupo darasa 1
 
Dogo anaweza kuzibiwa riziki kizembe, akapelekwa elimu bure wakati kulikuwa na nafasi ya kupelekwa shule ya maana, hao wazazi wajiridhishe chap kwamba Babu tale atamsomesha wapi na kwa level ipi waandikishiane, kama ni magumashi wakatae ofa yake mapema wafadhili wa maana wapo wengi maana dogo anao uwezo
Siku akikosa ubunge na mtoto anapotea huko huko
 
Back
Top Bottom