Makampuni ya michezo ya kubahatisha yameendelea kuongezeka kwa kasi sana nchini Tanzania kuliko nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki.
Ongezeko hili linachagizwa na ukweli usiopingika kuwa kumiliki kampuni ya michezo ya kubahatisha ndio njia rahisi zaidi ya kuvuna pesa kutoka kwa watu wa rika mbalimbali.
Kilichonisukuma kuandika andiko hili sio kuhoji uhalali wa makampuni haya ya michezo ya kubahatisha bali namna yalivyopewa uhuru na serikali kuchota pesa za wavuja jasho bila kufuatiliwa kwa huduma zao.
Kinachoendelea kwenye makampuni haya ni zaidi ya utapeli wa kawaida. Leo nitapenda nijikite zaidi kwenye michezo ya kasino (online casino) inayotolewa kwenye makampuni haya mbalimbali hususani game ya AVIATOR na ZEPPELIN.
Michezo hii imekuwa ni hatari sana kwa taifa letu kiuchumi, kiafya na kiakili kwa ujumla. There's no fairness hata kidogo kwenye michezo hii na zaidi ipo kuwaibia watumiaji wa huduma hizo.
Sina uhakika kama serikali huwa inajiridhisha kwenye huduma zinazotolewa na makampuni haya kwa watumiaji. Na kama huwa inafanya hivyo na imeamua kukaa kimya badi ni dhahiri kuwa imebariki taifa lake liendelee kunyonywa na kuharibiwa kiakili.
Serikali ndio mlezi mkuu wa taifa lake na haipaswi kuruhusu na kuhalalisha wizi wa wazi kwa raia wake. Michezo tajwa haiongozwi na bahati kama watu wanavyofikiria bali ni mitambo inayoongozwa na mmiliki wa mitambo husika.
Mmiliki anaamua atakalo kwenye pesa za watumiaji wa huduma na hakuna mechanisms za kufuatilia fairness katika matokeo yanayochakatwa na mtambo.
Jambo baya zaidi ni kuwa michezo hii ina nguvu kubwa sana ya kutengeneza uraibu (addiction) kwa watumiaji wake. Na kutambua hilo ndio maana hata baadhi ya makampuni wameondoa option ya kumruhusu mtumiaji wa huduma kujitoa (permanent self-exclusion) katika tovuti zao na hata ikitokea unamjulisha mtoa huduma juu ya nia ya kujiondoa kwa kufungwa account yako bado sio rahisi kusikilizwa.
Hawaruhusu account yako kufutwa kwa sababu wanaamini you're addicted already na sio rahisi kukaa bila kuifungua account yako.
Kila anayecheza michezo ya online casino ana chance kubwa ya kukumbwa na magongwa ya moyo na yale yanayohusiana na mfumo wa akili. Hivyo, vijana kwa wazee chukueni tahadhali kubwa juu ya michezo ya kubahatisha. Sio kweli kuwa kuna pesa huko za kuchukua kilaini tu.
Hata hao washindi wanaotangazwa kuwa wameshinda pesa nyingi sio issue ya ukweli na most of them are ghost winners na lengo ni kukuaminisha kuwa one day utakuwa wewe.
Serikali ifanye tafiti za kina kujua faida za kodi inayozikusanya kutoka kwa makampuni haya inaendana na madhara yatokanayo na huduma zinazotolewa kwa watumiaji.
Michezo hii hairuhusu vijana kuwa chanzo cha ujenzi wa taifa kiuchumi na mbaya zaidi athari zake zinagusa mpaka nyanja nyingine muhimu kwa maendeleo ya taifa kama vile elimu.
Vijana wa Sekondari, vyuo vya kati mpaka huko university wanaharibika kupitia michezo hii ya kubashiri.
Mwisho niwahimize wazazi tuwe na mfumo mzuri wa malezi ili kuwaepusha watoto wetu kujiingiza kwenye wizi huu ambao unavuna pesa likuki kwa manufaa ya watu wachache.