Serikali: Michezo ya kubahatisha imezalisha Ajira 25,000/=

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,552
Nimeinukuu toka kwa Millard Ayo.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake July 01, 2003 ambapo imesema licha kufanikiwa kuchangia pato la Taifa kufikia Tsh. bilioni 170.43 kwa mwaka, ndani ya miaka hiyo pia imefanikiwa kuzalisha ajira 25,000.

“Tumefanikiwa kuongeza ajira kwa Vijana, mchango wa maendeleo wa jamii kutoka kwenye Sekta pia umeongezeka katika kipindi hicho kutoka fursa za ajira 600 kwa mwaka 2006/7 hadi 25,000 kwa mwaka huu 2022/23.

“GBT imechochea pia ongezeko la ubunifu katika aina hizi za michezo kutoka aina tatu ya michezo tu mwaka 2003 hadi kufikia zaidi ya aina saba za michezo ya kubahatisha mwaka 2023.

“Pia, GBT imefanikiwa kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji wa Sekta hii na kuvutia makampuni yaliyowekeza katika biashara ya michezo ya kubahatisha kutoka kampuni 9 mwaka 2003 hadi kampuni 67 mwaka 2023”

“Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imefanikiwa kulinda haki za wachezaji na kutatua migogoro baina ya wachezaji na waendeshaji wa kampuni za michezo ya kubahatisha, tangu kuanziswa kwake GBT imekuwa ikipata hati safi ya ukaguzi na imekua mfano kwa baadhi ya nchi za Afrika, hususani ukanda wa Mashariki,Kati na Kusini”
=======

Kumbe kubeti ni ajira rasmi? Ngoja nipambane na bandari zangu nikisema sana naweza kosa yote.
 
Hizo ndio ajira za awamu ya sita ya viongozi mizigo wasio na maono. Pongezi kwao
Michezo hii ilishamiri kuanzia awamu ya inne, awamu ya tano ilipamba moto zaidi na sasa imekuwa ni uteja, ila kuwepo ilianzia enzi ya awamu ya kwanza, wakati huo ikiitwa bahati nasibu ya taifa sasa hivi imekuwa upgraded, yaani kama ni toleo basi ni promax
 
Dini zote zina panga kubeti ni Kamari, eti zimeungiza hela. Kwaiyo madawa ya kulevywa na bangi haiingizi hela. Acheni kusifia ujinga
 
Dini zote zina panga kubeti ni Kamari, eti zimeungiza hela. Kwaiyo madawa ya kulevywa na bangi haiingizi hela. Acheni kusifia ujinga
Hv mchungaji akisema jumapili wote mje na Tshs 500 kwa ajili ya sadaka na asiye leta atalaaniwa je huo sio mkeka kama waumini wakileta wote Tshs 500 ina maana mkeka umetiki na lazm mchungaji afurahi tena sio kidogo.
 
Hii ndiyo ajira rasmi isiyohitaji longolongo za kuonana na Hr wala kutembea na mavyeti kwenye maofisi.!

.. Malipo unapata kila siku umekaa tu na simu yako!

Simu yako ... Ofisi yako!
 
Back
Top Bottom