Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Miradi ya kuzalisha umeme

power project.jpg
 
Kimsingi nakubali kwamba amejitahidi kufanya kwa kiasi cha uwezo wake kwani hatuwezi kutarijia mark II kuburuta mabehewa ya treni.Ila kwa haya yanayooneshwa kwa vielelezo vya picha hapa ni maendeleo ya Vitu na siyo maendeleo ya Watu. Tunahitaji kuona maendeleo ya watu badala ya vitu .
1.Je Wakulima maisha yao ya mebadilika?
2.Vipi kuhusu wafugaji hali hii imechangia kuboresha maisha yao na kuondoa migogoro na Wakulima.
3.Je halii hii imepunguza vifo vinavyozuilika vya akina mama na watoto Tanzania.
4.Je raslimali za Taifa zimeshawekwa mikononi mwa wananchi kwa usawa na kwa kadri ya uwezo wa Mwananchi.

Kwa ujumla nadhani alichokifanya ni kumalizia mipango ya wenzake iliyokuwa tayari kwa uwekezaji na akasahau kwamba mipango hiyo ilitakiwa iende sambamba na kuboresha hali ya Maisha ya Mwananchi wa Kawaida.

Hata akingia Dr slaa madarakani leo huwezi kutuaminisha kwamba ataweza kumfanya kila mwanakijiji aweze kuwa na maisha bora hayo unayoyazungumza, kupanga ni kuchagua, hata wewe katika maisha yako binafsi una mengi ambayo hayajatimia, kumalizia mipango ya waliomtangulia pia kunahitaji determination na uwezo wa kifedha, mf vitambulisho vya Taifa mpango ulikuwepo muda mrefu Mzee Mkapa hakuweza kuumalizia lakini yeye amefanikiwa tuache,BIG UP JK.
 
Hapana ndugu yangu Annael akisha leta sinia la Ubwabwa nyumbani ndo ata haribu kabisa Mimi mbali na kazi yangu ni mkulima mdogo mdogo.Hali yetu ni mbaya mno tunalima mazao hakuna masoko,Kupeleka watoto shule ni ghali sana na hakuna anayejishughulisha kuboresha masoko na bei za pembejeo ambazo ni kubwa sana hazi randani kabisa na bei ya mazao sokoni.

Huko kijijini tunakotumia muda mrefu ukiugua na kwenda Hospitali ni majanga ndugu yangu mtu ukiumwa tumbo panadol,ukiumwa kichwa panadol na Ukiumwa Jino Panadol,typhod panadol na hata malaria ni hivyohivyo.

Tunachokitaka kukiona ni mazingira ya mkulima kuboreshwa halingumu inayomkabili Mkulima kwa mtu ambaye Muda Mrefu yuko mjini hawezi ifahamu.

Hali yetu kiuchumi(wastani wa mapato) ni mbaya kuliko hata wakati wabarabara mbovu ambapo hata ukiuza gunia moja la Mchele ungeweza kupata fedha ya kujikimu kwa sasa gunia hilo ukiliuza bei yake ni ndogo kuliko miaka mitatu iliyopita.Ungejaribu kulitazama jambo hili kwa upande huo ungenielewa nilikuwa na maanisha nini.

Tunahitaji mipango inayotafsiri sera na kubadilisha maisha yetu basi.Hatuhitaji hisani za takrima ya Sinia la Ubwabwa,Kofia Tshirt,Nyamapori wala Kanga.





 

FaizaFoxy haya ndo nilikuwa nikimueleza mleta uzi kwamba hizo pembejeo na zana za kilimo zinazopewa wakulima Bei yake ni ya juu mno ukilinganisha na Bei ya Mazao yao shambani mfano Mkungu Mmoja wa ndizi unanunuliwa kwa Mkulima kwa bei ya Shilingi 3000 tu na gunia la mchele kwa kati ya bei ya shilingi 60,000 na 70,000.

Haya Matrekta yanakuwa kwa matukio Muhimu na yasiyo endelevu wangefanya Monitoring and evaluation wangebaini kwamba mara nyingi wanajitahidi kuzima moto na siyo kudhibiti chanzo cha moto na ndiyo sabu hali yetu wakulima inakuwa mbaya siku hadi siku.Nakuhakikishia ni zaid ya asilimia sitini ya wakulima hawawezi kumudu kabisa hivyo vifaa unavyoviona hapo na ndo maake kule kwetu kijijini baadhi ya mashine hizi kwa wale wa chacvhe ambao kwa wilaya nzima wanaweza wasizidi watano au kumi badala yakuwa shambani na mashine hizi wakilima wamezigeuza vyombo vya usafiri kwani kilimo hakilipi kabisa Mfano Kuna nchi Duniani zinategemea zao landizi tu katika kujiendesha Kiuchumi lakini lakini hapa kwetu Changamoto ni kubwa bado .

Sibezi jitihada zinazofanyika lakini nivema chama Tawala kitumie watunga sera waliopo kwa umakini na kuhakikisha wanafanya na kuzitafsiri sera na mipango ya Maendeleo Hususan kwenye kilimo ambapo ndo ajira rahisi zaidi kwa wengi kwa kumgusa mtu wachini. Hali ilvyo sasa ni kweli tunaigiza tu uhalisia hali ni mbaya mno na nadhani Kinana Na Nape watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kulieleza hili iwapo wanapita humu.
 
Hata akingia Dr slaa madarakani leo huwezi kutuaminisha kwamba ataweza kumfanya kila mwanakijiji aweze kuwa na maisha bora hayo unayoyazungumza, kupanga ni kuchagua, hata wewe katika maisha yako binafsi una mengi ambayo hayajatimia, kumalizia mipango ya waliomtangulia pia kunahitaji determination na uwezo wa kifedha, mf vitambulisho vya Taifa mpango ulikuwepo muda mrefu Mzee Mkapa hakuweza kuumalizia lakini yeye amefanikiwa tuache,BIG UP JK.

Kazi ya Rais siyo kugawa maendeleo kama BIG ndugu yangu .Soma unielewe ninacho kimaanisha hili si suala la Kichama ni suala la Maslahi ya nchi kama ambavyo wamarekani wanaweza kuhalalisha kuvamia nchi nyingine kwakisingizio cha kueneza Demokrasia na kupinga Ugaidi (lakini ndani wakiwa na nia ya kukidhi kiu yao isiyo kwisha ya kukamata mafuta na gesi kulisha viwanda vyao) kwa Tanzania suala la Kukuza uchumi huku ukisahau Kilimo haina tofauti na kuvaa suti mpya huku ukitembea peku bila viatu. Lazima Taifa liwe na vipau mbele ambapo kwa Tanzania ilitakiwa iwe AFYA, ELIMU, MIUNDOMBINU NA KILIMO.

Wengi tunakimbilia kwenye miundo mbinu hasa barabara kwasababu tunadhani ni jambo linaloonekana kiurahisi na kwa haraka.Tunasahau kwamba Miundo Mbinu hii iliiwe na Manufaa lazima mipango izingatie nyanja nyingine ilikukamilisha ukuaji wa Uchumi kutoka kwenye makaratasi hadi kwa watu (jamii). Tunapokazania uwekezaji katika Miundo mbinu na uwekezaji Mkubwa (madini na Gesi) na wakati huo huo kusahau/kupuuza kilimo ambacho kinaajiri asilimia 80 ya wananchi tutaishia kuwa na maendeleo ya vitu na siyo watu.

Nakubaliana na wewe kwamba kupanga ni kuchagua lakini lazima unapokuwa na madaraka ya kuongoza Nchi ufanye Uchaguzi ulio Bora (an informed Decision) hii nchi ni yetu sote na tunaishi leo hatutakiwi kuishi leo as if tuna jiandaa kwa ajili ya kuishi leo .Lazima mipango na sera itafsiri na kuharakisha maendeleo sasa. Chama chochote kitakachoshindwa kuharakisha maendeleo kiondolewe kwa kura full stop.

Fursa zilizopo kwa nchi yetu ni nyingi sana ila kinachokwamisha ni Uzembe,Wizi.Ufisadi,kutowajibishana na Ubinafsi uliokithiri ambapo kila Mtu anapopata madaraka hafikirii kulitumikia Taifa bali kujitafutia madaraka ya juu zaidi na kudhibiti kama siyo kuwamaliza kabisa wenzake badala ya kukazana kuumaliza umasikini unaolinyonga Taifa hili lililobarikiwa raslimali za kila aina.
 
Nimefurahi wan jf wamekujibu japo kwa kifupi sana na yapo mengi ila mimi nataka ujiulize wewe umefanyanini na ndo uulize serikari imekufanyia nini.
 
Kuna watu wana njaa. Ukiwaonyesha mti wenye matunda wanauliza, nani atayachuma hayo matunda?

Ukiwachumia wanauliza, nani atayamenya?

Ukiwamenyea, watasema mbona hujamenya vizuri?

Watu hawa tunao hapa Tanzania pia. Mmoja wao ni Kajunjumele BA


Ndugu yangu ZeMarcopolo umenifurahisha kwa hii Comment yako ila yanabaki kuwa ni maoni yako tu ili nakuhakikishia kwamba "WITH A GOOD MAN ON SADDLE EVEN UNRULY HORSE CAN BE PUT UNDER CONTROL" (by LORD Denning) na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Mungu amrehemu alikuwa na Msimamo thabiti kuhusu maendeleo kwamba " ILI NCHI IENDELEE INAHITAJI ARDHI, WATU,SIASA SAFI NA UONGOZI BORA"

Kwa nchi yetu ARDHI na WATU vipo changamoto ni SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Nikweli pia kwamba kwamaoni yangu ninazungumzia "Maendeleo ya watu" sina maana ya ukwasi tu "PESA" kama wengi wanavyodhani bali upatikanaji wa kiujumla wa Mahitaji yote ya Msingi kwa Maisha ya Binadamu na Uwezo wa Binadamu hawa kumudu gharama za mahitaji hayo na wale wasiyo weza kumudu kwasabu ya umasikini uliopitiliza,uzee au ulemavu walionao kuwepo na utaratibu maalum wa upatikanaji wa huduma hizi hususan kwenye Afya na Elimu,haya ndiyo yanayoitwa maendeleo ya watu.

Na sina maana kwamba Masikini wote watakwisha hapana bado umasikini utakuwepo lakini kwa mazingira tofauti na hali ilivyo sasa.Kwani hata hizo Nchi zilizoendelea Masikini bado wapo.Tunachotaka nikuwepo kwa fursa sera na taratibu wazi zinazo fikika (accessible) kwa wananchi wote ndipo tuwalaumu kwa uzembe wa kushindwa kuzitumia fursa hizo.Kwa sasa ukimwambie mwanachi akalime atakuuliza tu atalimaje? ,mtaji wapembejeo atapata wapi? na hali ya masoko kwa mazao yake ikoje?
 
Nimefurahi wan jf wamekujibu japo kwa kifupi sana na yapo mengi ila mimi nataka ujiulize wewe umefanyanini na ndo uulize serikari imekufanyia nini.
 
Hivi ile wizara ya Chai na Vitafunwa inaanzishwa lini?
 
Twambie ni kwa kiwango gani ya watanzania zaidi ya 90% ambao wanaishi kwa kilimo ni kwa vipi JK amewaboreshea maisha yao. Nyingi ya nyumba zao bado ni mbavu za mbwa. Hospital nzuri kwao ni zile zilizojengwa na wamisionari kabla ya nchi kupata uhuru. Viwango vyake vilikuwa bora zaidi ya leo. Watu hawa ndio wanawafitini watoto wasifaulu darasa la 7 kwa kuchelea kushindwa karo ya 20,000. Maji safi na salama ni ndoto pamoja nakupatikana mbali na maskani yao. Watoto wanafeli kwa viwango vikubwa. Ukienda polisi au mahakamani unanua karatasi za kuandikia kesi yako huko vijijini. Zimejengwa zahanati zisizo na dawa. Reli zimehujumiwa ili mkopo uimarishe barabra ili magari ya mafisadi yaweze kudumu ktk kusafirisha mizigo na abiria kwa gharama kubwa, akinyonywa mkulima kwa kulipa gharama za usafirishaji na mkulima atalipa mkopo unaochukuliwa kila uchao. Nitaendelea.,.,.,.
ata
Unatokea mkoa gani ndugu ! hamna mbolea za ruzuku huko, ikumbukwe hata akingia huyu Dr Sala wenu mnayemwabudu never hawezi badili hii hali within a second even one term of 5 yrs period. Jambo la msingi ni kipaumbele gani kila utawala umejiwekea natarajia hata katika ngazi ya familia ndivyo ilivyo mnajinyima kwajili ya kupeleka watoto shule. hata kama katika kilimo bado kuna mapungufu ni kwa sababu ya kipaumblele.
 
ata
Unatokea mkoa gani ndugu ! hamna mbolea za ruzuku huko, ikumbukwe hata akingia huyu Dr Sala wenu mnayemwabudu never hawezi badili hii hali within a second even one term of 5 yrs period. Jambo la msingi ni kipaumbele gani kila utawala umejiwekea natarajia hata katika ngazi ya familia ndivyo ilivyo mnajinyima kwajili ya kupeleka watoto shule. hata kama katika kilimo bado kuna mapungufu ni kwa sababu ya kipaumblele.

Hao sio kama hawaoni, wanaona kila kitu ila wanaendekeza nafsi ndio maana wanashindwa kujizuia kusema vile vilivyojificha kwenye vifua vyao...
 
Back
Top Bottom