jk ni rais ambaye anaondoka madarakani bila kuacha kumbukumbu chanya yenye kurithiwa na kuendelezwa. Ni kweli kwamba ccm imekiri kupitia kwa katibu mkuu wake kinana kuwa hali ya wananchi bado ni masikini sana, hivyo maisha bora kwa kila mtanzania ni ndoto za mchana. Jk ameshindwa kutekeleza mradi muhimu wa national identity, mradi huu umeishia kusikojulikana. Jk ameshindwa kuwaunganisha watanzania, amesababisha mitafaruku ya kidini kati ya viongozi wa dini kupitia hoja ya kadhi. Ni jk ambaye ameshindwa kusimamia mchakato wa katiba na hivyo kupata katiba feki inayopingwa na watu makini.. Jk ameshindwa hata zoezi la kuandikisha watanzania kwa wakati ili waweze kupiga kura ya maoni. Lakini pia jk amefeli kutekeleza agizo lake la kufanyika kwa kura ya maoni tar 30 april. Na kibaya zaidi jk atashindwa kutoka madarakani kwa muda kwa kikatiba kutokana na kushindwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu oct 2015. Huyu ndio jk.