Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Matukio ya kimataifa nchini

Sullivan_1212447272.jpg
 
Kazi ya Rais siyo kugawa maendeleo kama BIG ndugu yangu .Soma unielewe ninacho kimaanisha hili si suala la Kichama ni suala la Maslahi ya nchi kama ambavyo wamarekani wanaweza kuhalalisha kuvamia nchi nyingine kwakisingizio cha kueneza Demokrasia na kupinga Ugaidi (lakini ndani wakiwa na nia ya kukidhi kiu yao isiyo kwisha ya kukamata mafuta na gesi kulisha viwanda vyao) kwa Tanzania suala la Kukuza uchumi huku ukisahau Kilimo haina tofauti na kuvaa suti mpya huku ukitembea peku bila viatu. Lazima Taifa liwe na vipau mbele ambapo kwa Tanzania ilitakiwa iwe AFYA, ELIMU, MIUNDOMBINU NA KILIMO.

Wengi tunakimbilia kwenye miundo mbinu hasa barabara kwasababu tunadhani ni jambo linaloonekana kiurahisi na kwa haraka.Tunasahau kwamba Miundo Mbinu hii iliiwe na Manufaa lazima mipango izingatie nyanja nyingine ilikukamilisha ukuaji wa Uchumi kutoka kwenye makaratasi hadi kwa watu (jamii). Tunapokazania uwekezaji katika Miundo mbinu na uwekezaji Mkubwa (madini na Gesi) na wakati huo huo kusahau/kupuuza kilimo ambacho kinaajiri asilimia 80 ya wananchi tutaishia kuwa na maendeleo ya vitu na siyo watu.

Nakubaliana na wewe kwamba kupanga ni kuchagua lakini lazima unapokuwa na madaraka ya kuongoza Nchi ufanye Uchaguzi ulio Bora (an informed Decision) hii nchi ni yetu sote na tunaishi leo hatutakiwi kuishi leo as if tuna jiandaa kwa ajili ya kuishi leo .Lazima mipango na sera itafsiri na kuharakisha maendeleo sasa. Chama chochote kitakachoshindwa kuharakisha maendeleo kiondolewe kwa kura full stop.

Fursa zilizopo kwa nchi yetu ni nyingi sana ila kinachokwamisha ni Uzembe,Wizi.Ufisadi,kutowajibishana na Ubinafsi uliokithiri ambapo kila Mtu anapopata madaraka hafikirii kulitumikia Taifa bali kujitafutia madaraka ya juu zaidi na kudhibiti kama siyo kuwamaliza kabisa wenzake badala ya kukazana kuumaliza umasikini unaolinyonga Taifa hili lililobarikiwa raslimali za kila aina.

Nami nakubaliana na wewe kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, lakini ebu leo hii tujiulize sote mimi na wewe tukafanikiwa kuboresha kilimo 100% kule vijijini lakini chakula kile ambacho wakulima wale wamekipata hawawezi kusafilisha kwenda sokoni kwa sababu ya barabara,bado kilimo kile hakina tija kwa sababu mazoa yataoza .mf mimi naishi mikoa hi ya Rukwa ,tunazalisha chakula kwa wingi sana lakini barabara zetu hazifikiki kwa msimu wote wa mwaka kwa hiyo tunashindwa kuuza mazoa ya ziada.kwetu sisi barabara ndio kipaumbele as longo bado tunauwezo wa kuzalisha chakula cha kutoshelezea mahitaji yetu ya mwaka.
 
Annael umejitahidi. Umetimiza kazi ambayo jk ameipigia kelele siku nyingi ' tangazeni mazuri tunayoyafanya'.

Wekeni pia picha za mauaji ya Mwandishi Mwangosi, Babu Seya kifungoni, waliofukiwa na vifusi vya madini, waliathirika na maji sumu kutoka migodini, jk akianguka jukwaani, magari yakikwsma barabara kutopitika, misululu mirefu akina mama wakutafuta maji kahama, shinyanga, mabomu ya gongo la mboto...uchunguzi ukiendekea, vijana waathirka madawa ya kulevya. this will balance your story, itaonesha uzalendo wako pia.

Mbona hata china watu wanafukiwa na vifusi ndugu yangu pamoja na maendeleo ya technology yote waliyonayo, USA kuna watu wanakufa kwa kupigwa risasi ovyo ovyo tu je hivyo vyote vinakanusha maendeleo yaliyofikiwa katika mataoifa hayo? kwa taarifa yako hata rais akiwa Mh Mbowe hayo yatatokea tu, lakini hayo yasitufanye tuwe vipofu wa kuona ukweli wa hatua zinapigwa na serikali,huu utamaduni wa kupinga kila kitu ukijengeka hata nyie mkiingia madarakani wapinzani wenu pia watajifanya vipofu na viziwi wa kuona jitihada mtakazozifanya .upinzani wa kweli sio kupinga kila kitu jamani !
 
index.jpg UPATIKANAJI WA ARV NCHI NZIMA
Serikali ya JK imejitahidi kupigania haki ya Mtanzania kuishi, Wenye VVU wameweza kuendelea kuishi muda mrefu na kwa matumaini zaidi
 
ie.jpg SCHOLARSHIPS KWA WANAFUNZI WA TANZANIA
Serikali ya JK imewekeana Mkataba wa Serikali ya China kusomesha Watanzania 1000 elimu ya juu nchini china kila mwaka, huku serikali ya TZ ikisomesha wachina 10 nchini Tanzania kila mwaka
 
index3.jpg UBUNIFU WA AJIRA
Serikali ya JK imewezesha Maelfu ya Vijana kupata ajira kupitia bodaboda na bajaji, Vijana hawa wameweza kukuza kipato chao na hivyo kusaidia hata familia zao
 
images4.jpg Kukuza Uzalendo na Kuwa na Taifa Kakamavu
Serikali ya JK baada ya kuona vijana wameanza kuwa "soft soft" , "visharobaro sharobaro", ikaamua kurejesha busara za Muasisi wa Taifa hili JK Nyerere, na kurudisha tena JKT, sasa hivi vijana hawa wana discipline wako focused na ni hazina ya Taifa
 
Safi sana, Tunapojua kulaumu tujue na kushukuru, tunapojua kukandia tujue na kusifia Hata Mungu anahimiza haya. JK amefanya mengi sana pamoja na nguvu kubwa ya waliotaka sifanye llote. Lete mapichaaaaaaa. Wapi kiwanda cha chuma Liganga sjui Mchuchuma huko Annael
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom