Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hakuna kitu kinakera kama ahadi za uwongo wa wanasiasa. Na mbaya zaidi ni pale ambapo wanaahidi uongo kwa vitu ambavyo vinagharimu maisha ya watu. Kwa nini wanasiasa wanapenda kusema uongo?
Tuchukulie huu mteremko wa Mbalizi unapotoka Mbeya mjini kwenda Songwe airport, Mbozi Tunduma na hata Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afrika Kusini, Congo nk. Ni barabara muhimu sana hii, na sehemu hii imeua watu wengi kutia ndani viongozi wa serikali na kuharibu mali za mabilioni ya fedha.
Kila inapotokea ajali, viongozi wanakuja na maneno matamu sana ya ahadi kurekebisha sehemu hii, ambayo ni fupi sana, kama kilomita moja na nusu tu. Miaka nenda miaka rudi hakuna kilichofanyika.
Mnataka nani afe hapo ili mchukue hatua, Waziri Mkuu? Au mnataka Watanzania wangapi wafe kabla ya kuchukua hatua?
Hii barabara si kwa ajili ya watu wa Mbeya tu, na kumbukeni kunapotokea ajali hata wasafiri wanaokwenda airport Songwe wanaathirika. Kama serikali ya CCM iliweza kutoa ahadi za papo kwa hapo kujenga barabara za lami zisizo kwenye mipango ya serikali wakati wa kampeni, mnashindwaje kutenga fungu ili kuweka njia nne katika hii sehemu ya barabara kuu Tanzania?
Kwako wewe Tulia kama Mbunge wa Mbeya. Umuhimu wa kuweka njia nne katika hii barabara ya Mbeya, kuanzia Uyole hadi sehemu ya Airport Songwe, haupaswi kuwa jambo ambalo unatakiwa uambiwe. Msongamano wa magari na ajali zinazotokea maeneo ya Mwanjelwa ni jambo lililowazi hata kwa mtu asiye na PhD, sasa kwa nini kwako liwe gumu kuliona?
Wiki hii imetokea ajali nyingine tena ambapo loli la shaba limegonga magari matano hivi. Vifo ambavyo vingeweza kutokea hapa inatisha kuwazia.
Natoa wito kwa wakazi wa Mbeya kwamba mnapaswa kuja juu kudai haki yenu ya kuendelea kuishi ili sehemu hii ijengwe njia nne. Daini kwamba tozo za miamala za mwezi ujao lazima zipelekwe hapa Mbalizi kujenga njia nne kwa sababu kuna hatari za vifo, papewe kipao mbele kwenye kutumia fedha za tozo.
Na kwa nini watu wa Mbeya mnaridhika na msongamano uliopo Mwanjelwa wakati uwezo wa kudai hii barabara ipanuliwe sehemu hii kuwa njia nne toka Uyole hadi Songwe airport serikali inao ila inawapuuza? Nyie ndio mnalisha karibu asilimia 50% ya Tanzania lakini serikali inakosa kuonyesha shukurani kwenu kwa kitu kidogo kama kurekebisha hii sehemu ya Songwe ili watu wasiendelee kufa. Mnakubali mabilioni yakajenge international airport Chato na kufanyiwa matamasha ya ngoma. Si mliambiwa mkimtosa Sugu mambo yenu yatanyooshwa? Wake up!