Not_James_bond
Member
- Sep 10, 2023
- 20
- 65
Nimekuwa mkazi wa Mbeya kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne sasa, lakini kati ya majiji yote niliyowahi kutembea katika kipindi chote, sijawahi kuona jiji lenye barabara mbovu kama Mbeya. Kuna barabara za lami zimekuwa na mashimo makubwa kwa zaidi ya miaka miwili, na ni barabara zenye umuhimu sana, kama vile barabara za kuingia na kutoka soko la Soweto, barabara ya Isyesye, Ituha, Makunguru, Veta ya Machinjioni, Block T, barabara za Stand ya Nane, na barabara ya kuingia na kutoka Stand ya Dadadala Airport ya zamani. Zote hizi ni mbovu kwa kipindi kirefu, na hii inaleta changamoto kubwa kwa wakazi wa maeneo haya.
Kwa muda sasa, tumekuwa tukishuhudia hali ya barabara hizi ikizidi kudorora. Hali hiyo imesababisha matatizo mengi, ikiwa ni pamoja na:
1. Usalama wa Watumiaji wa Barabara: Barabara hizi zina mashimo na sehemu zilizoharibika, na hivyo kuongeza hatari ya ajali na majeruhi kwa watu wanaotumia barabara hizi.
2. Uharibifu wa Magari: Kutokana na ubovu wa barabara, magari mengi yameharibika na wamiliki wamekuwa wakilazimika kutumia gharama kubwa kwa ajili ya matengenezo.
3. Usafirishaji na Biashara: Barabara hizi zina jukumu muhimu katika usafirishaji wa bidhaa na shughuli za biashara katika eneo letu. Ubovu wa barabara umesababisha usumbufu mkubwa katika shughuli hizi za kiuchumi.
Kwa sasa, kwa baadhi ya maeneo, kama vile Isyesye, inawalazimu vijana wa maeneo hayo kufanya kazi ya kujaza kifusi kwenye mashimo ili kusaidia watumiaji wa barabara hizo.
Tunatambua kwamba kurekebisha barabara kunaweza kuwa na gharama kubwa, lakini serikali yetu ya eneo au mamlaka ya barabara inapaswa kutoa kipaumbele kwa suala hili na kuanzisha hatua za haraka kurekebisha barabara hizi. Pia, tunaomba kuwe na uwazi katika matumizi ya fedha za umma kwa miradi ya miundombinu ya barabara.