Mbeya: Watu 9 Wafariki katika ajali baada ya gari la abiria kuongwa nan Lori katika Mteremko wa Iwambi-Mbalizi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,046
49,730
Mteremko wa Iwambi- Mbalizi umeanza kufyonza tena Damu za watu baada ya kimya Cha mda mrefu.

Kwa mujibu wa Polisi na mashuhida Lori lililofeli breki liligonga daladala aina ya Mitsubishi na kusababisha kutumbukia korongoni na kusababisha vifo na majeruhi wengi.

My Take
Pole sana Kwa ndugu wafiwa Kwa vifo vya wapendwa wenu,Mungu azipokee roho zenu na awajaalie kupona majeruhi wote.😭😭😭😭😭

Pili watu wa Mbeya badala ya kutumia mda mwingi kubishana na Serikali ni vyema mkashirikiana Ili Kumaliza ajali eneo Hilo kama kule Shimwenga(Mteremko wa Nsalaga-Uyole).

================

Mnamo 22/09/2023 majira ya saa 11:40 jioni huko eneo mteremko wa Iwambi Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya kuelekea Tunduma, Gari yenye namba za usajili BCE 9384/ABX 8675 aina ya Howo mali ya kampuni ya Horn Afric Motors ltd ya nchini Zambia ikitokea Mbeya kuelekea Tunduma likiendeshwa na dereva MOHAMED ABILAH [47] Msomali, Mkazi wa Zambia iliigonga kwa nyuma Gariyenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubish Rosa ikitokea Mbeya mjini kuelekea mbalizi ikiendeshwa na Dereva ELLY ELIA MWAKALINDILE [41] Mkazi wa Iyunga na kusababisha vifo kwa watu 9 kati yao wanaume 5 wanawake 4.

Aidha katika ajali hiyo watu 23 wamajeruhiwa kati yao wanaume 13 na wanawake 10. Majeruhi wanaendelea kutibiwa Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi ambapo miili ya marehemu 07 imetambuliwa huku miili ya watu 02 bado haijatambuliwa.

Chanzo cha ajali hii ni Dereva wa lori kushindwa kulimudu gari lake kwenye mteremko mkali na kwenda kuigonga kwa nyuma Gari ya abiria. Dereva wa lori amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva ambao wanapita katika Mkoa wa Mbeya kwenye milima na miteremko mikali kuhakikisha wanakagua magari yao kabla ya kuanza safari na wamiliki wa magari wasiruhusu magari yao kuendeshwa na madereva hao ili kuepusha ajali.

Imetolewa na:
BENJAMIN KUZAGA - ACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
 
View: https://www.instagram.com/p/CxgznbCtgEy/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

My Take
Pole sana Kwa ndugu wafiwa Kwa vifo vya wapendwa wenu,Mungu azipokee roho zenu na awajaalie kupona majeruhi wote.

Pili watu wa Mbeya badala ya kutumia mda mwingi kubishana na Serikali ni vyema mkashirikiana Ili Kumaliza ajali eneo Hilo kama kule Shimwenga(Mteremko wa Nsalaga-Uyole).

Rip Ila nadhani wewe ni kijana au mzee wa hovyo ajali na wizi wa Ccm vinahusiana vipi watu waache muuze bandari kisa ajali?
 
Acheni ujuaji wankindezi mtatelekezwa jumla, Bandari iuzwe Ili Serikali itoe wapi pesa?

Kwanza shukuruni yupo Spika vinginevyo mngeula wa chuya
 
Hilo eneo haupiti muda mrefu, utasikia habari ya lori limefeli breki na kuparamia magari mengine; na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa!!

Na wakati huo huo hatusikii hatua zozote zile za madhubuti zikichukuliwa na serikali ili kukomesha hizo ajali!! Hivi kuna sababu za msingi kweli za kushindwa kuzitanua na kuziboresha hizo barabara za Mbeya kweli!!
 
Ujenzi wa njia 4 umeanza ,hata hivyo Kuna trafiki pale wanasubirisha magari ndio maana Kwa mda mrefu hakujatokea ajali sema Kwa usiku Huwa hawapo ndio maana Hawa wamepatwa na hiyo shida.

View: https://youtu.be/krIb-lTS0qU?si=Aiewod_voSgOyjRD
 
Mteremko wa Iwambi- Mbalizi umeanza kufyonza tena Damu za watu baada ya kimya Cha mda mrefu.

Kwa mujibu wa Polisi na mashuhida Lori lililofeli breki liligonga daladala aina ya Mitsubishi na kusababisha kutumbukia korongoni na kusababisha vifo na majeruhi wengi.

My Take
Pole sana Kwa ndugu wafiwa Kwa vifo vya wapendwa wenu,Mungu azipokee roho zenu na awajaalie kupona majeruhi wote.😭😭😭😭😭

Pili watu wa Mbeya badala ya kutumia mda mwingi kubishana na Serikali ni vyema mkashirikiana Ili Kumaliza ajali eneo Hilo kama kule Shimwenga(Mteremko wa Nsalaga-Uyole).

================

Mnamo 22/09/2023 majira ya saa 11:40 jioni huko eneo mteremko wa Iwambi Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya kuelekea Tunduma, Gari yenye namba za usajili BCE 9384/ABX 8675 aina ya Howo mali ya kampuni ya Horn Afric Motors ltd ya nchini Zambia ikitokea Mbeya kuelekea Tunduma likiendeshwa na dereva MOHAMED ABILAH [47] Msomali, Mkazi wa Zambia iliigonga kwa nyuma Gariyenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubish Rosa ikitokea Mbeya mjini kuelekea mbalizi ikiendeshwa na Dereva ELLY ELIA MWAKALINDILE [41] Mkazi wa Iyunga na kusababisha vifo kwa watu 9 kati yao wanaume 5 wanawake 4.

Aidha katika ajali hiyo watu 23 wamajeruhiwa kati yao wanaume 13 na wanawake 10. Majeruhi wanaendelea kutibiwa Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi ambapo miili ya marehemu 07 imetambuliwa huku miili ya watu 02 bado haijatambuliwa.

Chanzo cha ajali hii ni Dereva wa lori kushindwa kulimudu gari lake kwenye mteremko mkali na kwenda kuigonga kwa nyuma Gari ya abiria. Dereva wa lori amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva ambao wanapita katika Mkoa wa Mbeya kwenye milima na miteremko mikali kuhakikisha wanakagua magari yao kabla ya kuanza safari na wamiliki wa magari wasiruhusu magari yao kuendeshwa na madereva hao ili kuepusha ajali.

Imetolewa na:
BENJAMIN KUZAGA - ACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Ile bypass road ya kupita nyuma ya MUST iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom