Utopolo mmoja yupo pale Brela Anaitwa Nyaisa sijui hapa mama anategemea Nini!! Ondoa hizo takataka weka watu wanaoijua biashara na maana yake sio huyo boharia wa magereza unampeleka Brela kuweni serious kidogo basi
Tukisema maza hawezi mnasema kazi iendelee. Leo Lita moja ya petrol Tsh 2,700Nchi yetu imepita kwenye mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka sita.
Kumekua na mageuzi makubwa sana kiutawala na kiuchumi tangu 2015...
Hakuna kisichowezekana Bams . Tunapokuja kwenye swala la maslahi ya nchi lazima tukubali kwamba makosa yapo kwenye baadhi ya maeneo na nini kifanyike kuyaondoa.Mama D, hii nchi ni kama kuna laana kubwa ambayo sijui tutatoka vipi maana tunachokilalamikia ndicho tunachokijenga.
Kinachofanyika kwenye hivyo vyombo ni copy and paste ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi....
Hilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia 💯! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!
Umesahau na oshaHilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!
Hukuwepo Tanzania 2020? Ule uchafuzi unasema wananchi waliwanyima kina Lisu nchi?! Usitake kujidanganya, ili utete chama chako mfu!Unaweza kusema hili ni tatizo la CCM lakini nitakuuliza swali, Je ni chama gani kina uwezo wa kufanya haya mambo yakawa sawasawa?? Huoni wananchi waligoma kuwapa kina Tundu nchi wafanye majaribio?
Hukuwepo Tanzania 2020? Ule uchafuzi unasema wananchi waliwanyima kina Lisu nchi?! Usitake kujidanganya, ili utete chama chako mfu!
Ccm Ina uozo wote ulioainisha kwenye bandiko lako, na mda wake wa kuzikwa umefika!
Ni rahisi sana kuongea hizo propaganda matangopori mliyo aminishwa kama hujawai kutishwa hata na kile kisu cha kukunja! Harakati za mzalendo wenu Sir baya, ni ushahidi kwamba wanao pambana kufanya siasa kwenye jukwaa la upinzani ni mashujaa!Uchafuzi unaweza kuwepo kwenye sehemu yoyote ile. Uchafuzi unafanywa na mtu mmojammoja na sio chama.....kama ulivyokua kwenye kumchagua Mbowe kuwa mwenyekiti wa Chadema.
Na zaidi ya hilo Chadema hawakuwa wamejipanga kuchukua nchi. Kushika dola hakuji kwa posts za twita na Jf bali kwa wananchi kukusikia na kukuelewa.
Huwezi ishi ulaya ukaja kwenye kampeni, ukakosa, halafu ukarudi ulaya, unasubiri tena kampeni zianze ndio uje halafu upate. Sahauuuu
Tunahitaji sana upinzani na tunahitaji zaidi upinzani wenye tija
CCM imetufikisha hapa tulipoHilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia 💯! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!
Hakuna mwenye nia njema na hii nchi hata mmojaNi rahisi sana kuongea hizo propaganda matangopori mliyo aminishwa kama hujawai kutishwa hata na kile kisu cha kukunja! Harakati za mzalendo wenu Sir baya, ni ushahidi kwamba wanao pambana kufanya siasa kwenye jukwaa la upinzani ni mashujaa!
Ni aibu sana kwa hayo mambo yote mfanyayo, kubambikia wapinzani kesi, kuua, kutesa, kupiga risasi, kuminya uhuru wa kujeleza, kuzuia haki Ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa, kwa hoja za hovyo, eti kunyoosha nchi, sijui kujenga uchumi!
Uoga wa ccm unarudisha nchi yetu nyuma, kwa mfano mwendazake angesimamia katiba mpya, ingekuwepo hata baada ya kifo chake! Angalia sasa kaondoka na kila kitu! Nchi hii ni kubwa na muhimu kuliko utopolo ccm, mnayoabudu!
Ni rahisi sana kuongea hizo propaganda matangopori mliyo aminishwa kama hujawai kutishwa hata na kile kisu cha kukunja! Harakati za mzalendo wenu Sir baya, ni ushahidi kwamba wanao pambana kufanya siasa kwenye jukwaa la upinzani ni mashujaa!
Ni aibu sana kwa hayo mambo yote mfanyayo, kubambikia wapinzani kesi, kuua, kutesa, kupiga risasi, kuminya uhuru wa kujeleza, kuzuia haki Ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa, kwa hoja za hovyo, eti kunyoosha nchi, sijui kujenga uchumi!
Uoga wa ccm unarudisha nchi yetu nyuma, kwa mfano mwendazake angesimamia katiba mpya, ingekuwepo hata baada ya kifo chake! Angalia sasa kaondoka na kila kitu! Nchi hii ni kubwa na muhimu kuliko utopolo ccm, mnayoabudu!
Ni mali halali ya Rais wengine wote ni wapangaji tuTanzania ni ya watanzania sio ya chama cha siasa
Mama D,Tuongee kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, vyama ni majina tuu. Tukibadilika sisi wanachama nchi yetu itakua sehemu salama sana
Mama D.Nchi yetu imepita kwenye mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka sita.
Kumekua na mageuzi makubwa sana kiutawala na kiuchumi tangu 2015.
Kukataa kwamba mfumo uliokuwepo kabla ya 2015 ulishavunjwa na hauwezi kurudishwa ni kujidanganya, kinachotakiwa ni sasa ni kutembea na mabadiliko kwa serikali na idara zake kufanya kazi na sekta binafsi ili kuhakikisha ndani ya awamu hii kunakua na uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni ili kuongeza pato la taifa
Ninachosikitika ni kwamba Serikali yetu kupitia vyombo vyake ikiwa ni pamoja Wizara, Halmashauri zetu, agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS) mmekua kikwazo kikubwa kwa uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi hii. Kwa maneno mengine ni kwamba Vyombo vya serikali vimegeuka kuwa wahujumu uchumi namba1 wa juhudi za Rais kwenye kukuza uchumi wa nchi
Wawekezaji wengi sana wa nje na ndani wana mitaji yao na wamekua wakifuatilia vibali kwenye vyombo husika kwa zaidi hata ya mwaka MaWizara, Halmashauri zetu, Agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS).
TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS vimejawa usumbufu mkubwa na huduma mbovu sana kwa wateja na vikwazo vinavyochochea wawekezaji kuchoka, kukata tamaa na hata kughairi kuendelea na taratibu za uwekezaji kwenye nchi yetu.
Kuna wakati huwa najiuliza hivi wahusika ambao ni watendaji wa umma wanajua wanajua zinakotoka stahiki zao, ikiwa ni pamoja office, mahitaji ya office, mishahara yao na posho?
Hivi hawa wanajua bila kuwasaidia wawekezaji kwa kuwapa vibali na support wanakwamisha hata uendeshaji wa serikali?
Enyi TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS.. kwanini mnahujumu juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan?
Kwanini mnahujumu ukuaji wa uchumi wa nchi yetu?
Au mnataka kila siku tuwe tunakuja kulalamikia matendo yenu huku mitandaoni?
Hivi mnapokua humo maofisini mwenu mnafikiri nyie tuu ndio mnastahili kuwepo humo? Mlishawahi kujiuliza ni watu wangapi humu mtaani hawana ajira na wana uwezo wa kufanya hayo majukumu yenu kwa ubora zaidi ya mnachokifanya?
Rais wetu Samia Suluhu Hassan amesema mwaka huu watumishi wa umma hawawezi kuongezwa mshahara na kuahidi mwakani atajitahidi kufanya hivyo. Je, mna nia ya dhati kuhakikisha mnamsaidia Rais kutimiza ahadi yake?
Rais wetu anapambana kutekeleza miradi mikubwa, huduma za kijamii na mambo mengine mengi ikiwa ni pamoja kuhakikisha mna mazingira mazuri kwenu na ya kuhudumia wateja wenu. Basi kuwenu na shukrani walau kwa kufanya kazi kwa uhakika na kwa wakati.
Badala ya kufanya kazi kwa weledi na ufasaha wanageuka kuwa wazuiaji wa maendeleo na wavugaji wa nchi.Mama D, hii nchi ni kama kuna laana kubwa ambayo sijui tutatoka vipi maana tunachokilalamikia ndicho tunachokijenga.
Kinachofanyika kwenye hivyo vyombo ni copy and paste ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi.
Mahali ambapo tumekuwepo kwa miongo mingi ni:
Rais na vyombo vyake anadhibiti wakosoaji wa Rais na Serikali yake.
Msajili wa vyama vya siasa, anadhibiti vyama vya upinzani.
Polisi wanadhibiti wananchi wasioishangilia Serikali.
TRA, BOT, TBS, wanadhibiti wawekezaji na wafanya biashara.
Unachokiongelea hapa ni taswira ya Serikali nzima. Viongozi wetu na Serikali, siyo wawezeshaji bali ni wadhibiti na wapinzani wa chochote unachotaka kufanya mwananchi, isipokuwa tu kusifu. Kama unasifia, hata kama sifa unazozitoa ni za uwongo kama vile alivyokuwa akifanya Majaliwa na Chalamila kuwa Hayati Rais Mzalendo Magufuli anachapa kazi, wakati yupo mahtuti, wewe utawezeshwa na Serikali na vyombo vyake vyote.
Matendo yote hayo ya hovyo yanayofanywa na hivyo vyombo ulivyovitaja, na taswira ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi. Na hivyo vyote havitabadilika kamwe, mpaka mfumo wa uendeshaji nchi ubadilike, na hilo halitawezekana bila ya kuwa na Katiba Mpya iliyo bora inayotoa mwongozo mpya ulio bora wa kuendesha nchi. Vinginevyo tuendelee tu kuvumilia tukijua kuwa sisi ni wa kushuhudia maendeleo ya mataifa mengine, lakini siyo ya Taifa letu.
Hizo ni porojo fika kwenye field uone,halafu je sheria zinazingatiwa barabara au ni kutekeleza amri za wakubwa ili kulinda vibarua vyao?Hakuna kisichowezekana Bams . Tunapokuja kwenye swala la maslahi ya nchi lazima tukubali kwamba makosa yapo kwenye baadhi ya maeneo na nini kifanyike kuyaondoa.
Walioko kwenye hizo nafasi sio wageni, ni watanzania wenye mapenzi mema kwa nchi hii.
Inawezekana kabisa policy ziko vizuri na process za utendaji zipo sawa ila matumizi ya commonsense na usimamizi makini.
Tusisusie haya mambo maana kama likiharibika hawaumii wao wanaoharibu peke yao, ila tunaumia wote kama watanzania