Serikali, Wizara, Halmashauri, Agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC) mkiendelea na kazi kwa mazoea mtaendelea kuwa wahujumu uchumi namba 1

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,294
2,000
Nchi yetu imepita kwenye mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka sita.

Kumekua na mageuzi makubwa sana kiutawala na kiuchumi tangu 2015.

Kukataa kwamba mfumo uliokuwepo kabla ya 2015 ulishavunjwa na hauwezi kurudishwa ni kujidanganya, kinachotakiwa ni sasa ni kutembea na mabadiliko kwa serikali na idara zake kufanya kazi na sekta binafsi ili kuhakikisha ndani ya awamu hii kunakua na uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni ili kuongeza pato la taifa

Ninachosikitika ni kwamba Serikali yetu kupitia vyombo vyake ikiwa ni pamoja Wizara, Halmashauri zetu, agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS) mmekua kikwazo kikubwa kwa uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi hii. Kwa maneno mengine ni kwamba Vyombo vya serikali vimegeuka kuwa wahujumu uchumi namba1 wa juhudi za Rais kwenye kukuza uchumi wa nchi

Wawekezaji wengi sana wa nje na ndani wana mitaji yao na wamekua wakifuatilia vibali kwenye vyombo husika kwa zaidi hata ya mwaka MaWizara, Halmashauri zetu, Agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS).

TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS vimejawa usumbufu mkubwa na huduma mbovu sana kwa wateja na vikwazo vinavyochochea wawekezaji kuchoka, kukata tamaa na hata kughairi kuendelea na taratibu za uwekezaji kwenye nchi yetu.

Kuna wakati huwa najiuliza hivi wahusika ambao ni watendaji wa umma wanajua wanajua zinakotoka stahiki zao, ikiwa ni pamoja office, mahitaji ya office, mishahara yao na posho?

Hivi hawa wanajua bila kuwasaidia wawekezaji kwa kuwapa vibali na support wanakwamisha hata uendeshaji wa serikali?

Enyi TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS.. kwanini mnahujumu juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan?

Kwanini mnahujumu ukuaji wa uchumi wa nchi yetu?

Au mnataka kila siku tuwe tunakuja kulalamikia matendo yenu huku mitandaoni?

Hivi mnapokua humo maofisini mwenu mnafikiri nyie tuu ndio mnastahili kuwepo humo? Mlishawahi kujiuliza ni watu wangapi humu mtaani hawana ajira na wana uwezo wa kufanya hayo majukumu yenu kwa ubora zaidi ya mnachokifanya?

Rais wetu Samia Suluhu Hassan amesema mwaka huu watumishi wa umma hawawezi kuongezwa mshahara na kuahidi mwakani atajitahidi kufanya hivyo. Je, mna nia ya dhati kuhakikisha mnamsaidia Rais kutimiza ahadi yake?

Rais wetu anapambana kutekeleza miradi mikubwa, huduma za kijamii na mambo mengine mengi ikiwa ni pamoja kuhakikisha mna mazingira mazuri kwenu na ya kuhudumia wateja wenu. Basi kuwenu na shukrani walau kwa kufanya kazi kwa uhakika na kwa wakati.

Utopolo mmoja yupo pale Brela Anaitwa Nyaisa sijui hapa mama anategemea Nini!! Ondoa hizo takataka weka watu wanaoijua biashara na maana yake sio huyo boharia wa magereza unampeleka Brela kuweni serious kidogo basi
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,147
2,000
Hilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia 💯! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,953
2,000
Mama D, hii nchi ni kama kuna laana kubwa ambayo sijui tutatoka vipi maana tunachokilalamikia ndicho tunachokijenga.

Kinachofanyika kwenye hivyo vyombo ni copy and paste ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi.

Mahali ambapo tumekuwepo kwa miongo mingi ni:

Rais na vyombo vyake anadhibiti wakosoaji wa Rais na Serikali yake.

Msajili wa vyama vya siasa, anadhibiti vyama vya upinzani.

Polisi wanadhibiti wananchi wasioishangilia Serikali.

TRA, BOT, TBS, wanadhibiti wawekezaji na wafanya biashara.

Unachokiongelea hapa ni taswira ya Serikali nzima. Viongozi wetu na Serikali, siyo wawezeshaji bali ni wadhibiti na wapinzani wa chochote unachotaka kufanya mwananchi, isipokuwa tu kusifu. Kama unasifia, hata kama sifa unazozitoa ni za uwongo kama vile alivyokuwa akifanya Majaliwa na Chalamila kuwa Hayati Rais Mzalendo Magufuli anachapa kazi, wakati yupo mahtuti, wewe utawezeshwa na Serikali na vyombo vyake vyote.

Matendo yote hayo ya hovyo yanayofanywa na hivyo vyombo ulivyovitaja, na taswira ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi. Na hivyo vyote havitabadilika kamwe, mpaka mfumo wa uendeshaji nchi ubadilike, na hilo halitawezekana bila ya kuwa na Katiba Mpya iliyo bora inayotoa mwongozo mpya ulio bora wa kuendesha nchi. Vinginevyo tuendelee tu kuvumilia tukijua kuwa sisi ni wa kushuhudia maendeleo ya mataifa mengine, lakini siyo ya Taifa letu.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,923
2,000
Nchi yetu imepita kwenye mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka sita.

Kumekua na mageuzi makubwa sana kiutawala na kiuchumi tangu 2015...
Tukisema maza hawezi mnasema kazi iendelee. Leo Lita moja ya petrol Tsh 2,700
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,294
2,000
Mama D, hii nchi ni kama kuna laana kubwa ambayo sijui tutatoka vipi maana tunachokilalamikia ndicho tunachokijenga.

Kinachofanyika kwenye hivyo vyombo ni copy and paste ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi....
Hakuna kisichowezekana Bams . Tunapokuja kwenye swala la maslahi ya nchi lazima tukubali kwamba makosa yapo kwenye baadhi ya maeneo na nini kifanyike kuyaondoa.

Walioko kwenye hizo nafasi sio wageni, ni watanzania wenye mapenzi mema kwa nchi hii.
Inawezekana kabisa policy ziko vizuri na process za utendaji zipo sawa ila matumizi ya commonsense na usimamizi makini.

Tusisusie haya mambo maana kama likiharibika hawaumii wao wanaoharibu peke yao, ila tunaumia wote kama watanzania
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,294
2,000
Hilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia 💯! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!

Unaweza kusema hili ni tatizo la CCM lakini nitakuuliza swali, Je ni chama gani kina uwezo wa kufanya haya mambo yakawa sawasawa?? Huoni wananchi waligoma kuwapa kina Tundu nchi wafanye majaribio?
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
2,153
2,000
Hilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia ! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!
Umesahau na osha
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,147
2,000
Unaweza kusema hili ni tatizo la CCM lakini nitakuuliza swali, Je ni chama gani kina uwezo wa kufanya haya mambo yakawa sawasawa?? Huoni wananchi waligoma kuwapa kina Tundu nchi wafanye majaribio?
Hukuwepo Tanzania 2020? Ule uchafuzi unasema wananchi waliwanyima kina Lisu nchi?! Usitake kujidanganya, ili utete chama chako mfu!
Ccm Ina uozo wote ulioainisha kwenye bandiko lako, na mda wake wa kuzikwa umefika!
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,294
2,000
Hukuwepo Tanzania 2020? Ule uchafuzi unasema wananchi waliwanyima kina Lisu nchi?! Usitake kujidanganya, ili utete chama chako mfu!
Ccm Ina uozo wote ulioainisha kwenye bandiko lako, na mda wake wa kuzikwa umefika!

Uchafuzi unaweza kuwepo kwenye sehemu yoyote ile. Uchafuzi unafanywa na mtu mmojammoja na sio chama.....kama ulivyokua kwenye kumchagua Mbowe kuwa mwenyekiti wa Chadema.

Na zaidi ya hilo Chadema hawakuwa wamejipanga kuchukua nchi. Kushika dola hakuji kwa posts za twita na Jf bali kwa wananchi kukusikia na kukuelewa.
Huwezi ishi ulaya ukaja kwenye kampeni, ukakosa, halafu ukarudi ulaya, unasubiri tena kampeni zianze ndio uje halafu upate. Sahauuuu

Tunahitaji sana upinzani na tunahitaji zaidi upinzani wenye tija
 
Ni rahisi sana kuongea hizo propaganda matangopori mliyo aminishwa kama hujawai kutishwa hata na kile kisu cha kukunja! Harakati za mzalendo wenu Sir baya, ni ushahidi kwamba wanao pambana kufanya siasa kwenye jukwaa la upinzani ni mashujaa!
Ni aibu sana kwa hayo mambo yote mfanyayo, kubambikia wapinzani kesi, kuua, kutesa, kupiga risasi, kuminya uhuru wa kujeleza, kuzuia haki Ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa, kwa hoja za hovyo, eti kunyoosha nchi, sijui kujenga uchumi!
Uoga wa ccm unarudisha nchi yetu nyuma, kwa mfano mwendazake angesimamia katiba mpya, ingekuwepo hata baada ya kifo chake! Angalia sasa kaondoka na kila kitu! Nchi hii ni kubwa na muhimu kuliko utopolo ccm, mnayoabudu!
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Hilo ndo tatizo la ccm, hata bungeni! Unataja madudu yote ambayo yapo kila mahali kwenye serikali yenu ya ccm, alafu mwisho unaunga mkono bajeti kwa asilimia 💯! Hizo wizara, sijui na manini nini, ni viungo mbali mbali vinavyo unda serikali na utawala kwa jumla, ubovu wake ndo uozo wa serikali! Dawa ya yote, kwanza ni katiba mpya na pili, chama cha mapinduzi kuzikwa
Rasimi!
CCM imetufikisha hapa tulipo
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Ni rahisi sana kuongea hizo propaganda matangopori mliyo aminishwa kama hujawai kutishwa hata na kile kisu cha kukunja! Harakati za mzalendo wenu Sir baya, ni ushahidi kwamba wanao pambana kufanya siasa kwenye jukwaa la upinzani ni mashujaa!
Ni aibu sana kwa hayo mambo yote mfanyayo, kubambikia wapinzani kesi, kuua, kutesa, kupiga risasi, kuminya uhuru wa kujeleza, kuzuia haki Ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa, kwa hoja za hovyo, eti kunyoosha nchi, sijui kujenga uchumi!
Uoga wa ccm unarudisha nchi yetu nyuma, kwa mfano mwendazake angesimamia katiba mpya, ingekuwepo hata baada ya kifo chake! Angalia sasa kaondoka na kila kitu! Nchi hii ni kubwa na muhimu kuliko utopolo ccm, mnayoabudu!
Hakuna mwenye nia njema na hii nchi hata mmoja
 
Tuongee kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, vyama ni majina tuu. Tukibadilika sisi wanachama nchi yetu itakua sehemu salama sana
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,147
2,000
Tuongee kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, vyama ni majina tuu. Tukibadilika sisi wanachama nchi yetu itakua sehemu salama sana
Mama D,
Kunatakiwa maamuzi ya makusudi ya kudai katiba mpya! Katiba ni engen ya kuendesha nchi, ni hitaji la nchi, na siyo matakwa ya wachache! Nchi yetu Ina matatizo haya yote kwa sababu ya mwingozo (katiba) mbovu!
 
Scaramanga

Member
Aug 19, 2020
55
125
Nchi yetu imepita kwenye mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka sita.

Kumekua na mageuzi makubwa sana kiutawala na kiuchumi tangu 2015.

Kukataa kwamba mfumo uliokuwepo kabla ya 2015 ulishavunjwa na hauwezi kurudishwa ni kujidanganya, kinachotakiwa ni sasa ni kutembea na mabadiliko kwa serikali na idara zake kufanya kazi na sekta binafsi ili kuhakikisha ndani ya awamu hii kunakua na uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni ili kuongeza pato la taifa

Ninachosikitika ni kwamba Serikali yetu kupitia vyombo vyake ikiwa ni pamoja Wizara, Halmashauri zetu, agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS) mmekua kikwazo kikubwa kwa uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi hii. Kwa maneno mengine ni kwamba Vyombo vya serikali vimegeuka kuwa wahujumu uchumi namba1 wa juhudi za Rais kwenye kukuza uchumi wa nchi

Wawekezaji wengi sana wa nje na ndani wana mitaji yao na wamekua wakifuatilia vibali kwenye vyombo husika kwa zaidi hata ya mwaka MaWizara, Halmashauri zetu, Agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS).

TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS vimejawa usumbufu mkubwa na huduma mbovu sana kwa wateja na vikwazo vinavyochochea wawekezaji kuchoka, kukata tamaa na hata kughairi kuendelea na taratibu za uwekezaji kwenye nchi yetu.

Kuna wakati huwa najiuliza hivi wahusika ambao ni watendaji wa umma wanajua wanajua zinakotoka stahiki zao, ikiwa ni pamoja office, mahitaji ya office, mishahara yao na posho?

Hivi hawa wanajua bila kuwasaidia wawekezaji kwa kuwapa vibali na support wanakwamisha hata uendeshaji wa serikali?

Enyi TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS.. kwanini mnahujumu juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan?

Kwanini mnahujumu ukuaji wa uchumi wa nchi yetu?

Au mnataka kila siku tuwe tunakuja kulalamikia matendo yenu huku mitandaoni?

Hivi mnapokua humo maofisini mwenu mnafikiri nyie tuu ndio mnastahili kuwepo humo? Mlishawahi kujiuliza ni watu wangapi humu mtaani hawana ajira na wana uwezo wa kufanya hayo majukumu yenu kwa ubora zaidi ya mnachokifanya?

Rais wetu Samia Suluhu Hassan amesema mwaka huu watumishi wa umma hawawezi kuongezwa mshahara na kuahidi mwakani atajitahidi kufanya hivyo. Je, mna nia ya dhati kuhakikisha mnamsaidia Rais kutimiza ahadi yake?

Rais wetu anapambana kutekeleza miradi mikubwa, huduma za kijamii na mambo mengine mengi ikiwa ni pamoja kuhakikisha mna mazingira mazuri kwenu na ya kuhudumia wateja wenu. Basi kuwenu na shukrani walau kwa kufanya kazi kwa uhakika na kwa wakati.
Mama D.

Ili kuweka maelezo vizuri ingefaa zaidi kila taasisi ungeweka wapi walipokwamisha maana ukiangalia kila taasisi hapo tajwa zina majukumu tofauti hata kama ukisema uwekezaji kuna wengine watoa vibali,wengine wathibiti pesa,wengine wanajihusisha na uthibiti wa ubora na wengine wasajili wa biashara na wapo pia wakusanya kodi.
 
sirmweli

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
1,471
1,500
We mtoa mada umeanza lini kuikosoa serikali?

Au hujalipwa 7000 yako kutoka hapo Lumumba?
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
662
1,000
Mama D, hii nchi ni kama kuna laana kubwa ambayo sijui tutatoka vipi maana tunachokilalamikia ndicho tunachokijenga.

Kinachofanyika kwenye hivyo vyombo ni copy and paste ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi.

Mahali ambapo tumekuwepo kwa miongo mingi ni:

Rais na vyombo vyake anadhibiti wakosoaji wa Rais na Serikali yake.

Msajili wa vyama vya siasa, anadhibiti vyama vya upinzani.

Polisi wanadhibiti wananchi wasioishangilia Serikali.

TRA, BOT, TBS, wanadhibiti wawekezaji na wafanya biashara.

Unachokiongelea hapa ni taswira ya Serikali nzima. Viongozi wetu na Serikali, siyo wawezeshaji bali ni wadhibiti na wapinzani wa chochote unachotaka kufanya mwananchi, isipokuwa tu kusifu. Kama unasifia, hata kama sifa unazozitoa ni za uwongo kama vile alivyokuwa akifanya Majaliwa na Chalamila kuwa Hayati Rais Mzalendo Magufuli anachapa kazi, wakati yupo mahtuti, wewe utawezeshwa na Serikali na vyombo vyake vyote.

Matendo yote hayo ya hovyo yanayofanywa na hivyo vyombo ulivyovitaja, na taswira ya mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi. Na hivyo vyote havitabadilika kamwe, mpaka mfumo wa uendeshaji nchi ubadilike, na hilo halitawezekana bila ya kuwa na Katiba Mpya iliyo bora inayotoa mwongozo mpya ulio bora wa kuendesha nchi. Vinginevyo tuendelee tu kuvumilia tukijua kuwa sisi ni wa kushuhudia maendeleo ya mataifa mengine, lakini siyo ya Taifa letu.
Badala ya kufanya kazi kwa weledi na ufasaha wanageuka kuwa wazuiaji wa maendeleo na wavugaji wa nchi.
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
662
1,000
Hakuna kisichowezekana Bams . Tunapokuja kwenye swala la maslahi ya nchi lazima tukubali kwamba makosa yapo kwenye baadhi ya maeneo na nini kifanyike kuyaondoa.

Walioko kwenye hizo nafasi sio wageni, ni watanzania wenye mapenzi mema kwa nchi hii.
Inawezekana kabisa policy ziko vizuri na process za utendaji zipo sawa ila matumizi ya commonsense na usimamizi makini.

Tusisusie haya mambo maana kama likiharibika hawaumii wao wanaoharibu peke yao, ila tunaumia wote kama watanzania
Hizo ni porojo fika kwenye field uone,halafu je sheria zinazingatiwa barabara au ni kutekeleza amri za wakubwa ili kulinda vibarua vyao?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom