Serikali, Wizara, Halmashauri, Agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC) mkiendelea na kazi kwa mazoea mtaendelea kuwa wahujumu uchumi namba 1

Utopolo mmoja yupo pale Brela Anaitwa Nyaisa sijui hapa mama anategemea Nini!! Ondoa hizo takataka weka watu wanaoijua biashara na maana yake sio huyo boharia wa magereza unampeleka Brela kuweni serious kidogo basi
 
Utopolo mmoja yupo pale Brela Anaitwa Nyaisa sijui hapa mama anategemea Nini!! Ondoa hizo takataka weka watu wanaoijua biashara na maana yake sio huyo boharia wa magereza unampeleka Brela kuweni serious kidogo basi

Nyaisa🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Nchi yetu imepita kwenye mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka sita.

Kumekua na mageuzi makubwa sana kiutawala na kiuchumi tangu 2015.

Kukataa kwamba mfumo uliokuwepo kabla ya 2015 ulishavunjwa na hauwezi kurudishwa ni kujidanganya, kinachotakiwa ni sasa ni kutembea na mabadiliko kwa serikali na idara zake kufanya kazi na sekta binafsi ili kuhakikisha ndani ya awamu hii kunakua na uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni ili kuongeza pato la taifa

Ninachosikitika ni kwamba Serikali yetu kupitia vyombo vyake ikiwa ni pamoja Wizara, Halmashauri zetu, agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS) mmekua kikwazo kikubwa kwa uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi hii. Kwa maneno mengine ni kwamba Vyombo vya serikali vimegeuka kuwa wahujumu uchumi namba1 wa juhudi za Rais kwenye kukuza uchumi wa nchi

Wawekezaji wengi sana wa nje na ndani wana mitaji yao na wamekua wakifuatilia vibali kwenye vyombo husika kwa zaidi hata ya mwaka MaWizara, Halmashauri zetu, Agencies za umma (TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS).

TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS vimejawa usumbufu mkubwa na huduma mbovu sana kwa wateja na vikwazo vinavyochochea wawekezaji kuchoka, kukata tamaa na hata kughairi kuendelea na taratibu za uwekezaji kwenye nchi yetu.

Kuna wakati huwa najiuliza hivi wahusika ambao ni watendaji wa umma wanajua wanajua zinakotoka stahiki zao, ikiwa ni pamoja office, mahitaji ya office, mishahara yao na posho?

Hivi hawa wanajua bila kuwasaidia wawekezaji kwa kuwapa vibali na support wanakwamisha hata uendeshaji wa serikali?

Enyi TRA, BRELA, BOT, TRA, TIC, TBS.. kwanini mnahujumu juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan?

Kwanini mnahujumu ukuaji wa uchumi wa nchi yetu?

Au mnataka kila siku tuwe tunakuja kulalamikia matendo yenu huku mitandaoni?

Hivi mnapokua humo maofisini mwenu mnafikiri nyie tuu ndio mnastahili kuwepo humo? Mlishawahi kujiuliza ni watu wangapi humu mtaani hawana ajira na wana uwezo wa kufanya hayo majukumu yenu kwa ubora zaidi ya mnachokifanya?

Rais wetu Samia Suluhu Hassan amesema mwaka huu watumishi wa umma hawawezi kuongezwa mshahara na kuahidi mwakani atajitahidi kufanya hivyo. Je, mna nia ya dhati kuhakikisha mnamsaidia Rais kutimiza ahadi yake?

Rais wetu anapambana kutekeleza miradi mikubwa, huduma za kijamii na mambo mengine mengi ikiwa ni pamoja kuhakikisha mna mazingira mazuri kwenu na ya kuhudumia wateja wenu. Basi kuwenu na shukrani walau kwa kufanya kazi kwa uhakika na kwa wakati.
Good analysis

Beautiful with brain

Ushauri wako ni wakufanyiwa kazi

Naomba wapitie hapo juu kwa makini!
 
Hakuna kisichowezekana Bams . Tunapokuja kwenye swala la maslahi ya nchi lazima tukubali kwamba makosa yapo kwenye baadhi ya maeneo na nini kifanyike kuyaondoa.

Walioko kwenye hizo nafasi sio wageni, ni watanzania wenye mapenzi mema kwa nchi hii.
Inawezekana kabisa policy ziko vizuri na process za utendaji zipo sawa ila matumizi ya commonsense na usimamizi makini.

Tusisusie haya mambo maana kama likiharibika hawaumii wao wanaoharibu peke yao, ila tunaumia wote kama watanzania

Hapo kwenye "mapenzi mema" ndipo ulipokosea. Sehemu zote ziko sawa. Mimi nashauri hizo idara, ziende sekata binafsi, ili pengine viongozi wetu ni wageni kwenye uchapakazi ulioko huko.
 
Hapo kwenye "mapenzi mema" ndipo ulipokosea. Sehemu zote ziko sawa. Mimi nashauri hizo idara, ziende sekata binafsi, ili pengine viongozi wetu ni wageni kwenye uchapakazi ulioko huko.

Criterion🤣🤣🤣🤣
 
Utopolo mmoja yupo pale Brela Anaitwa Nyaisa sijui hapa mama anategemea Nini!! Ondoa hizo takataka weka watu wanaoijua biashara na maana yake sio huyo boharia wa magereza unampeleka Brela kuweni serious kidogo basi


Kwakweli afadhali tuendelee kuwataja hadharani kama hivi

Vipi kule TANESCO NA MAJI siku hizi wameacha ukiritimba?
 
Back
Top Bottom