mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 893
- 707
Salaam
Dunia inapambana kutatua vikwazo vya biashara,uwekezaji na mitaji..Hapa kwetu kumekuwa na jitihada nyingi Za kukuza uchumi kupitia mikakati mbalimbali ya kuwezesha wafanya biashara na wenye viwanda sambamba na kuvutia uwekezaji.
Tatizo Kwa maoni yangu ni wingi wa taasisi zinazofanya majukumu yanayoshabihiana Kwa namna moja au nyingine.
Mathalani tuna Tanzania Investment Centre (TIC),Tanzania Trade Authority (TANTRADE),Export Processing Zone Authority (EPZA) na pia Business Registration and Licencing Agency (BRELA)..
Ukifanya upembuzi wa kina ni wazi majukumu na utendaji wa hizi taasisi unafanana na kuingiliana hivyo kuongeza urasimu usio na lazima.Lakini pia Kwa serikali yetu ambayo bado inapambana kutatua kero lukuki zihusuzo umaskini kwake ni gharama kubwa kuruhusu uwepo wa taasisi hizi.
Nini kifanyike,Nadhani kungeundwa taasisi moja yenye kusimamia majukumu yote ya Hizi taasisi Kwa kuweka Idara Za kimkakati (Biashara,Viwanda,Uwekezaji,Ujasiliamali)..
Faida ni nyingi na pana hasa kuondoa urasimu na mwingiliano wa majukumu.
Shukrani