DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwani ungepeleka hizo details police ndio wangekuja kuwafanya Nini hao jamaa?Kuwatishia/kuwafunga au?

Mpakistani hakupi 1mil kizembe namna hio.
Polisi wangeweza kutowafanya kitu, ila kumpora mtu simu yake akipata mwanasheria mzuri akiunganisha na vingine ulimpora, kutumua ofisi yako kama tegesheo la kupora watu vitu basi ingekuwa kesi kubwa au anehonga sana zaid ya hiyo 1m
 
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan 🗾 asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Ninachojuwa Mimi gari used kitu muhimu sana ni engine na body, jitahidi kumlipa Fundi mkweli uende naye kununuwa gari kuna technical kadhaa za kuangalia.

Kuna kitu kinaitwa kuvunja, mfano una Rav4 unataka tako la nyani unampa mwenye yard Rav4 unamuongeza na pesa kisha anakupa tako la nyani.

Affricaries ni kampuni kubwa ya kuuza magari ya Fidahussein lakini wanarudia Rangi magari.

Kama kuna mtu anawaza kwenda Polisi asipoteze muda wake, Mimi ni ushahidi nimeshakamatwa na Interpol nikiwa na gari ya wizi iliibiwq Japan lakini tulinunuwa Kwa Fidahussein alichofanya alinipa gari ya kutumia Kwa muda then akaenda kutowa ile gari ya wizi nikarudishiwa.

Kuna kipindi Interpol huwa wana kuja Tanzania kuendesha oparesheni ya magari ya wizi, wale wenye magari ya kijanja ya bei mbaya huwa wanapewa taarifa wanayafungia.

Utajifanya unakwenda kutowa taarifa Polisi wakati huyo mkuu wa kituo kapewa gari bure atumie na haohao unaodhani eti unawalipuwa.
 
Back
Top Bottom