Juzi nilikuwa Posta, Mwendokasi mida ya jioni ni kisanga. Serikali hamwoni? Nusura nipate kilema

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
JUZI NILIKUWA POSTA, ASEEH! MWENDOKASI MIDA YA JIONI NI KISANGA. SERIKALI HAMWONI? NUSURA NIPATE KILEMA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Baada ya kumaliza kilichonipeleka, jua lilikuwa limeshapunga mkono wa Buriani. Kigiza cha usoni kilikuwa kimetawala usoni pa Nchi. Ni saa moja hiyo.

Nikaenda kituo cha Mwendokasi Posta ya Zamani pale. Nikakuta umati mkubwa wa Watu ndani ya kituo. Hilo halikunishangaza sana. Wingi sio hoja. Nilijua kama yangekuja magari matano hivi basi Lundo lile la Watu lingekuwa limepata huduma.

Lakini haikuwa hivyo. Subiri magari! Subiri wee! Wapi! Ikapita nusu saa, sasa ilikuwa inakaribia saa mbili hivi.
Gari mojamoja likawa linapita lakini halisimami. Kituoni Watu wanazidi kufurika.

Kuuliza uliza maana mimi sio mtumiaji wa mara kwa mara wa haya magari. Kwanza wale abiria wenzangu walionyesha kunishangaa, wao kwao hiyo haikuwa habari. Wameshazoea. Ingawaje wapo Wachache ambao walikuwa wakilalamika. Wanasema hiyo mbona ni kawaida, wao kila mara hali hiyo hutokea. Mmmh!

Nikapata wazo nipande gari zinazorudi Kivukoni ambazo muda huwa zinakuwa hazina Watu wengi. Kufika tena Kituo cha Kivukoni huko kidogo nipige Yowee! Jamani! Jamani! Jamani! Ule umati ulikuwa ni mkubwa, misururu mirefu ya Watu waliokaa kwenye mistari ilinikatisha tamaa. Hiyo ni saa mbili usiku sasa.

Magari yanakuja lakini ni machache sana. Yaani Watu ni wengi mno kuliko watu.

Nisingeweza kupanga Foleni kwa namna ile. Nikaenda upande ambao ulikuwa ni kwaajili ya wasiotaka kupanga foleni. Tunaita Wapiga mipira ya Kona Watu wagombanie. Hapo gari ikija na kusimama, vita huzuka, fujo hutokota, ghasia na purukushani ya vuta ni kuvute, sukuma niingie. Prakatatumba ngungurungangari!
Hapo nikaona mzee mmoja akimenyeka, kwa macho yangu nikamuona akijitutumua huku akiminywa na kuminywa, nikamuona akiingizwa polepole kutokana na kani ya msuguano wa watu.

Nikapiga kelele. "Mnamuua! Mnamuua mzee wa Watu" Lakini haikusaidia kitu. Hakuna aliyekuwa anajali zaidi ya kung'ang'ania kuingia ndani ya gari. Nilipiga kelele kwa sababu nilimuoma yule mzee akitoa jicho kama anakataa roho huku ulimi ukitoa nje kama mtu aliyekabwa na mwiba wa Samaki Kibua. Wachache wakafanikiwa kuingia wakituacha wengine nje.

Hapo nikashusha pumzi nzito. Nikiwa nimesogea katika ukingo wa kupandia gari wanaposimamia abiria.
"Kiatu! Kiatu! Kuna aliyeacha kiatu" kuna kijana mmoja wa makamo aliongea huku akiangalia chini. Basi macho yetu wote kwenye kile kiatu.

Kilikuwa kiatu cheusi nafikiri cha mguu wa kushoto chenye kamba. Soli ya kiatu kile ilikuwa imesiginwa upande hivi. Nikazidi kukaza macho yangu na bila shaka sikuwa pekee yangu niliyefanya hivyo. Huku mijadala ya lawama, manung'uniko na maombi yasiyo na msikilizaji yakiendelea kuzonga masikio yangu kutoka kwa Watu.

Nikajua kitakuwa ni kiatu cha yule Mwanaume niliyemuona akihangaishwa nusura afie kwa kugombania Mwendokasi. Niliwahi sikia mtu akiwa anakata roho basi ati roho huanzia kutokea kwenye miguu, unyayoni. Huenda kama kile kiatu kisingetoka mguuni mwake yule mwanaume basi angeshakuwa ameaga mashindano. Hayo yalikuwa mawazo yangu tuu ambayo yalikatishwa na Gari jingine lililokuwa limefika ambalo lilikuwa linapakazia Watu walioko kwenye foleni kabla ya kuja kwetu sisi wapiga Kona. Mimi niliomba kimoyomoyo niwe mpiga kona wa mguu wa kushoto nikiwa nimevaa kile kiatu cha yule mwanaume. Ili nimlipie kisasi.

Hapo hofu ikiwa imeniingia, picha za kukatikakatika za yule mwanaume jinsi alivyokuwa anatoa macho huku ulimi nje kama mbwa wa askari wa magendo. Nilihitaji kujiandaa kwa pambano la kuingia mwendokasi.

Gari lilipofika, nikavuta pumzi ndefu kama mpuliza baragumi ndilo tarumbeta. Kisha gari lilipo simama nami nikajirusha lakini kabla sijaufikia mlango nikakamatwa kwa nyuma. Sikujua aliyenikamata na wala sikuwa na muda wa kugeuka nyuma kuangalia aliyenikamata. Macho yangu mbele, nikazidi kuzikusanya nguvu zangu nikijivuta mbele kuukabili mlango wa Mwendokasi.

Jamani! Jamani! Mlango ulikuwa nusu hatua tuu lakini kuukaribia ulikuwa ni kisanga. Kwenda siendi! Na kama nikijilegeza kidogo narudishwa nyuma huku tayari nikiona baadhi ya Watu wakiingia. Kudadadeki!

Pai D kipeo cha pili H sijui ilikuwa ni kanuni ya umbo gani lakini nikajikuta nimesema kimoyomoyo. Niliamini kanuni hiyo ingenisaidia kupenya katika kipenyo cha mlango wa Mwendokasi.

Nikajitutumua, hapo nikasogea mbele nikaushika ule mlango. Dadeki! Vuta n'kuvute. Nikapigwa kipepsi ya mdomo. Nikasikia Kwaa! Jino au kitu gani? Nikasema hapa lazima kurudishwa, nami nikarudisha paa nikamtwanga yule kijana. Sasa kila mmoja atatibu alipoumizwa mambo ya bahati mbaya sikuyapa nafasi. Nisingeruhusu asi-score kirahisi vile. Ndani! Nikajikuta nipo Ndani katikati ya viti.

Hapo nikiwa na maumivu ya mbavu na kile kisukusuku nilichopigwa karibu na taya. Yule jamaa aliyenipigq kisukusuku nikamwona ameshika jicho lake limevia, ni kama alikuwa anataka fujo. Si amenikadiria na kuniona Mdogomdogo.

Nikamwambia tusisumbue abiria kama vipi tushuke tumalizane anavyotaka yeye. Watu wakawa wanashangaa, gari likaondoka buuuuuu! Saa mbili na dakika arobaini hiyo. Kutokea saa moja kasorobo.

Raha ya Mwendokasi hainichukui dakika ishirini nitakuwa nimefika nyumbani. Lakini sio kwa ule mbanano. Ndani ya gari yule jamaa kila mara nilimwona akifikicha jicho lake. Na kama tungegongana macho alikuwa kama anataka kunifuatafuata lakini asingefika kwangu pasipo kupangua safu ya Watu waliotutenganisha kutokana na mbanano mkali.

Mpaka ninafika oxygen yangu sijui ilikuwa ngapi mwilini. Na maumivu makali ya mbavu na taya.

Sasa serikali, tuachane na stori yangu hiyo. Hivi nini kinashindikana kuongeza magari hasa muda ya asubuhi na jioni. Kwa sababu Posta na Kariakoo kuanzia saa kumi na mbili Watu wanapata tabu mno. Wanapoteza muda mwingi njiani.

Ninyi viongozi mkipita barabarani mnataka mpishwe na mnaenda kwa haraka kusema mnashughuli za kitaifa. Ni nini kinawafanya msiwarahisishie maisha Watu mpaka tunataka kutoana roho kisa kugombea Magari?

Serikali, tazameni jambo hili.

Mimi nimemaliza, acha nipumzike nikakande taya langu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Tatizo sio serikali,tatizo ni wabongo washazoea shida na kakubali kila kitu. Tunaona shida ni muhimu hivo hata serikali inaenda hivo hivo wabongo wanavopenda. Toka niwe na pikipiki yangu nimesahau kabisa kupanda mwendokasi Wala kuwaza mateso yake na Mimi ni maskini tu sasa imagine kiongozi au watu wengine wakubwa wapo mbali kabisa na reality sababu haiwagusi.

Wabongo siku tukiamua kuanzisha chaos, watu kadhaa wafe, wapigwe na wengine jela at least serikali itapata awareness, we are so docile.
 
Watu warudi Mikoani. Mjini wako wachoma mihogo, mahindi, na biashara kibao. Huku Mikoani kutupu hakuna watu wote wamekimbilia Dar kutafuta Maisha. Makonda angeendelea kuwa Mkuu WA Mkoa Dar kungenyooka. Mji gani kila MTU mchuuzi.
 
Tatizo sio serikali,tatizo ni wabongo washazoea shida na kakubali kila kitu. Tunaona shida ni muhimu hivo hata serikali inaenda hivo hivo wabongo wanavopenda. Toka niwe na pikipiki yangu nimesahau kabisa kupanda mwendokasi Wala kuwaza mateso yake na Mimi ni maskini tu sasa imagine kiongozi au watu wengine wakubwa wapo mbali kabisa na reality sababu haiwagusi.

Wabongo siku tukiamua kuanzisha chaos,watu kadhaa wafe,wapigwe na wengine jela at least serikali itapata awareness,we are soo docile.
Ngumu sana kuanzisha hiyo chaos ..sababu tunaishi kinafiki na kibinafsi ..
 
JUZI NILIKUWA POSTA, ASEEH! MWENDOKASI MIDA YA JIONI NI KISANGA. SERIKALI HAMWONI? NUSURA NIPATE KILEMA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Baada ya kumaliza kilichonipeleka, jua lilikuwa limeshapunga mkono wa Buriani. Kigiza cha usoni kilikuwa kimetawala usoni pa Nchi. Ni saa moja hiyo.

Nikaenda kituo cha Mwendokasi Posta ya Zamani pale. Nikakuta umati mkubwa wa Watu ndani ya kituo. Hilo halikunishangaza sana. Wingi sio hoja. Nilijua kama yangekuja magari matano hivi basi Lundo lile la Watu lingekuwa limepata huduma.

Lakini haikuwa hivyo. Subiri magari! Subiri wee! Wapi! Ikapita nusu saa, sasa ilikuwa inakaribia saa mbili hivi.
Gari mojamoja likawa linapita lakini halisimami. Kituoni Watu wanazidi kufurika.

Kuuliza uliza maana mimi sio mtumiaji wa mara kwa mara wa haya magari.
Kwanza wale abiria wenzangu walionyesha kunishangaa, wao kwao hiyo haikuwa habari. Wameshazoea. Ingawaje wapo Wachache ambao walikuwa wakilalamika.
Wanasema hiyo mbona ni kawaida, wao kila mara hali hiyo hutokea. Mmmh!

Nikapata wazo nipande gari zinazorudi Kivukoni ambazo muda huwa zinakuwa hazina Watu wengi. Kufika tena Kituo cha Kivukoni huko kidogo nipige Yowee! Jamani! Jamani! Jamani! Ule umati ulikuwa ni mkubwa, misururu mirefu ya Watu waliokaa kwenye mistari ilinikatisha tamaa. Hiyo ni saa mbili usiku sasa.

Magari yanakuja lakini ni machache sana. Yaani Watu ni wengi mno kuliko watu.

Nisingeweza kupanga Foleni kwa namna ile. Nikaenda upande ambao ulikuwa ni kwaajili ya wasiotaka kupanga foleni. Tunaita Wapiga mipira ya Kona Watu wagombanie.
Hapo gari ikija na kusimama, vita huzuka, fujo hutokota, ghasia na purukushani ya vuta ni kuvute, sukuma niingie. Prakatatumba ngungurungangari!
Hapo nikaona mzee mmoja akimenyeka, kwa macho yangu nikamuona akijitutumua huku akiminywa na kuminywa, nikamuona akiingizwa polepole kutokana na kani ya msuguano wa watu.

Nikapiga kelele. "Mnamuua! Mnamuua mzee wa Watu" Lakini haikusaidia kitu. Hakuna aliyekuwa anajali zaidi ya kung'ang'ania kuingia ndani ya gari. Nilipiga kelele kwa sababu nilimuoma yule mzee akitoa jicho kama anakataa roho huku ulimi ukitoa nje kama mtu aliyekabwa na mwiba wa Samaki Kibua.
Wachache wakafanikiwa kuingia wakituacha wengine nje.

Hapo nikashusha pumzi nzito. Nikiwa nimesogea katika ukingo wa kupandia gari wanaposimamia abiria.
"Kiatu! Kiatu! Kuna aliyeacha kiatu" kuna kijana mmoja wa makamo aliongea huku akiangalia chini. Basi macho yetu wote kwenye kile kiatu.

Kilikuwa kiatu cheusi nafikiri cha mguu wa kushoto chenye kamba. Soli ya kiatu kile ilikuwa imesiginwa upande hivi. Nikazidi kukaza macho yangu na bila shaka sikuwa pekee yangu niliyefanya hivyo. Huku mijadala ya lawama, manung'uniko na maombi yasiyo na msikilizaji yakiendelea kuzonga masikio yangu kutoka kwa Watu.

Nikajua kitakuwa ni kiatu cha yule Mwanaume niliyemuona akihangaishwa nusura afie kwa kugombania Mwendokasi. Niliwahi sikia mtu akiwa anakata roho basi ati roho huanzia kutokea kwenye miguu, unyayoni. Huenda kama kile kiatu kisingetoka mguuni mwake yule mwanaume basi angeshakuwa ameaga mashindano. Hayo yalikuwa mawazo yangu tuu ambayo yalikatishwa na Gari jingine lililokuwa limefika ambalo lilikuwa linapakazia Watu walioko kwenye foleni kabla ya kuja kwetu sisi wapiga Kona.
Mimi niliomba kimoyomoyo niwe mpiga kona wa mguu wa kushoto nikiwa nimevaa kile kiatu cha yule mwanaume. Ili nimlipie kisasi.

Hapo hofu ikiwa imeniingia, picha za kukatikakatika za yule mwanaume jinsi alivyokuwa anatoa macho huku ulimi nje kama mbwa wa askari wa magendo. Nilihitaji kujiandaa kwa pambano la kuingia mwendokasi.

Gari lilipofika, nikavuta pumzi ndefu kama mpuliza baragumi ndilo tarumbeta. Kisha gari lilipo simama nami nikajirusha lakini kabla sijaufikia mlango nikakamatwa kwa nyuma. Sikujua aliyenikamata na wala sikuwa na muda wa kugeuka nyuma kuangalia aliyenikamata. Macho yangu mbele, nikazidi kuzikusanya nguvu zangu nikijivuta mbele kuukabili mlango wa Mwendokasi.

Jamani! Jamani! Mlango ulikuwa nusu hatua tuu lakini kuukaribia ulikuwa ni kisanga.
Kwenda siendi! Na kama nikijilegeza kidogo narudishwa nyuma huku tayari nikiona baadhi ya Watu wakiingia. Kudadadeki!

Pai D kipeo cha pili H sijui ilikuwa ni kanuni ya umbo gani lakini nikajikuta nimesema kimoyomoyo. Niliamini kanuni hiyo ingenisaidia kupenya katika kipenyo cha mlango wa Mwendokasi.

Nikajitutumua, hapo nikasogea mbele nikaushika ule mlango. Dadeki! Vuta n'kuvute. Nikapigwa kipepsi ya mdomo. Nikasikia Kwaa! Jino au kitu gani? Nikasema hapa lazima kurudishwa, nami nikarudisha paa nikamtwanga yule kijana. Sasa kila mmoja atatibu alipoumizwa mambo ya bahati mbaya sikuyapa nafasi. Nisingeruhusu asi-score kirahisi vile.
Ndani! Nikajikuta nipo Ndani katikati ya viti.

Hapo nikiwa na maumivu ya mbavu na kile kisukusuku nilichopigwa karibu na taya. Yule jamaa aliyenipigq kisukusuku nikamwona ameshika jicho lake limevia, ni kama alikuwa anataka fujo. Si amenikadiria na kuniona Mdogomdogo.

Nikamwambia tusisumbue abiria kama vipi tushuke tumalizane anavyotaka yeye. Watu wakawa wanashangaa, gari likaondoka buuuuuu! Saa mbili na dakika arobaini hiyo. Kutokea saa moja kasorobo.

Raha ya Mwendokasi hainichukui dakika ishirini nitakuwa nimefika nyumbani. Lakini sio kwa ule mbanano. Ndani ya gari yule jamaa kila mara nilimwona akifikicha jicho lake. Na kama tungegongana macho alikuwa kama anataka kunifuatafuata lakini asingefika kwangu pasipo kupangua safu ya Watu waliotutenganisha kutokana na mbanano mkali.

Mpaka ninafika oxygen yangu sijui ilikuwa ngapi mwilini. Na maumivu makali ya mbavu na taya.

Sasa serikali, tuachane na stori yangu hiyo. Hivi nini kinashindikana kuongeza magari hasa muda ya asubuhi na jioni.
Kwa sababu Posta na Kariakoo kuanzia saa kumi na mbili Watu wanapata tabu mno. Wanapoteza muda mwingi njiani.

Ninyi viongozi mkipita barabarani mnataka mpishwe na mnaenda kwa haraka kusema mnashughuli za kitaifa. Ni nini kinawafanya msiwarahisishie maisha Watu mpaka tunataka kutoana roho kisa kugombea Magari?

Serikali, tazameni jambo hili.
Mimi nimemaliza, acha nipumzike nikakande taya langu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ungevunjika hata hilo gumba ili mabandiko yako yafupike kidogo.
 
Back
Top Bottom