DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Jul 19, 2021
2,791
8,005
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimepiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari yanauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika.
 
Noma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.

Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
 
Mkuu, kama ulikua hujui hii michezo sasa ndo uje kwamba yard zetu ni majanga...wanaouza gari na odo zake ni janmotors... hata kama gari ina km 200,000 utaikuta hivohivo...na utapewa na auction rating/details zake ..na hapa kwenye auction rating ni hivi gari yeyote yenye rating below 3 maana yake haifai..

Sasa ukiwa unanunua gari bongo kwenye hizi yard mara nyingi hawakupi file lenye auction rating ukiwaomba wanapiga chenga.but auction documents zitakupa taarifa za gari kuanzia odo readings, condition ya gari ilivokua Japan..etc.
 
Aisee, mi sijui kwanini kuanzia enzi za JABA, baba alioouziwa gari bovu magari ya yard nayaogopa sana
 
Noma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.

Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
Mpakistani wa kutoa mil 1 hayupo,hio ni chai.

Odometer zitaendelea kuchezewa na Cha kufanya hakuna.
 
Tupeni somo basi tujue utajyaje odometer iliyochezeshwa mauno
Waombe file la Gari lilio tokanalo japan,Ukiona wanakupiga janjajanja sepa.

Option nyingine,chukua VIN(Vehicle Identification Number) ya Gari i-search mtandaoni possibility kubwa Ni kuikuta Gari hio na details zake zote(maana Gari hizo zinauzwa minadani hukk Japan) then linganisha Km za hii Gari hapo Yard vs Km ikiwa huko Mnadani.

Zamani Nilikua nalipia pesa kidogo ($10) kwny website flani,nawatumia VIN then wananitumia details zote za hio Gari,Ila hii sites iko shutdown siku hizi.
 
Back
Top Bottom