Serikali ifanye udhibiti wa uuzaji wa spare za magari ya Serikali na Mafuta; Tunaomiliki garage tunaumia sana mfanyacho

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Naomba kutoa Rai kwa Serikali kujiwekea utaratibu mzuri wa kuwadhibiti madereva. Hali ya sasa siyo nzuri sana mtaani na kwenye vijiwe. Yawezekana kweli uchumi siyo mzuri na maslahi ya madereva siyo mazuri kivile kutokana na elimu zao. Lakini pamoja na umaskini walionao haileti maana kufungua spear za magari mapya na kuziuza kisha kufunga spear zilizokufa. Haileti maana kufungua matairi mazuri yenye TBS na kufunga tairi zilizopitwa na wakati . Ni hatari sana kwao, kwa wanaowabeba na hata familia zao.

Lakini haya yote yanatokana na ukweli kwamba hakuna usimamizi wala anayefuatilia ufanisi wa vyombo vya usafiri vya Serikali. Nikifuatilia sana aliyepewa dhamana ya kuwasimamia madereva ana masters na wakati mwingine hata Phd. Analipwa fedha nyingi lakini pia kwa ubosi wake siyo mtu wa kwenda garage kufuatilia. Baadhi hata vifaa vyamagari hawavifahamu hivyo kujua kibovu na kizima kwao kizungumkuti. Baadhi wamepewa dhamana hiyo kama adhabu huku baadhi wakiwa na mgongano wa maslahi kwa kushirikiana na madereva kuhujumu Serikali kwenye matengenezo na mafuta.

Hali hii ya wizi wa mafuta na vipuri imekuwepo muda mrefu ila kwa sasa imezidi. Dereva anakuja na gari garage anawapa vijana wafungue vifaa na kufunga vibovu hadharani bila hata kificho. Naandika kwa uchungu kwani magari mengi haya yananunuliwa kwa kodi zetu huku machache tukipewa msaada.

Kwa upande mwingine wapo madereva wanafungua vifaa hasa tyre za gari za umma na kufunga kwenye magari yao. Unajiuliza huyu Dereva akipata ajali na tyre mbovu nani atakayekuwa? Udhibiti wa kodi zetu upo wapi?

Nadhani Serikali inaweza ikawa imelifumbia macho ila sisi tuliopo mtaani kwenye vijiwe na wamiliki wa garage tunaona. Hata kesho serikali ikitoa namba za whatsapp special watu watume picha za uhalifu huu watu watatuma. Siyo Busara magari ya kodi zetu yakafa kwa sababu ya watu wachache wanaonenepesha familia zao.

Leo tembelea ofisi za Serikali uone magari yaliyopaki, ni mapya kabisa ila wameyakwapua vifaa vya ndani na kuuza kisha wameyaweka juu ya mawe. Kila ofisi ukienda magari ya Serikali mapya yamepaki lakini huku mtaani hakuna bosi yeyote ambaye amepaki gari means watumishi wa umma wana pesa za kutunza magari kuliko Serikali? Hapana, wanayaua makusudi kwa kuuza spear na kunenepesha miili yao.

Last time tuliona Mtanda akiwa huko Kaskazini anaenda ofisi ya mkurugenzi magari yamepaki kwa kifaa cha milioni moja; yakikaa baada ya muda wanaanza kuiba kifaa na kwenda kuuza......huu ndio uhujumu uchumi.

Ni yapi maoni yangu kwa Serikali na jamii?
1. Maafisa usafirishaji Serikalini wawe wataalamu wa fani ya usafirishaji waweze kusimamia vyema mali za umma ikiwemo pikipiki na magari.

2. Dereva atakayebainika ameiba au kuuza kifaa cha Serikali afukuzwe kazi kulinda uhai wa anaowabeba akiwemo bosi wao

3. Magari yote mapya yaliyopaki kwenye ofisi za umma viongozi wa hizo taasisi wawajibishwe ikiwemo kufukuzwa kazi kwa kuhujumu uchumi wa wananchi. Gari ya milioni mia mbili inapaki hadi kufa kwa kukosa huduma ya milioni moja au mbili?

4. Garage itakayobainika ina spear zilizotolewa kwenye gari za Serikali mmiliki awajibishwe ikiwemo kuthibitisha alipotoa spear husika.

5. Serikali ipige marufuku gari za Serikali kuingia garage zisizo rasmi na pale zinapopaki au kuingia pawepo na kibali maalum cha kufanya hivyo.

6. Serkali itoe namba maalumu kwa umma ya kusaidia kuripoti matukio ya hujuma kwa mali za umma.

7. Utaratibu wa kuwauzia watumishi hasa viongozi wa umma magari uangaliwe upya kwani unachangia wao kuua magari kwa lengo la kujiuzia.

Zidumu fikra za watu wazalendo, zidumu hoja zenye tija, lidumu jukwaa la great thinkers.
 
Naomba kutoa Raia kwa serikali kujiwekea utaratibu mzuri wa kuwadhibiti madereva. Hali ya sasa siyo nzuri sana mtaani na kwenye vijiwe. Yawezekana kweli uchumi siyo mzuri na maslahi ya madereva siyo mazuri kivile kutokana na elimu zao. Lakini pamoja na umaskini walionao haileti maana kufungua spear za magari mapya nakuziuza kisha kufunga spear u hoja zenye tija, lidumu jukwaa la great thinkers
Kauli za Hangaya kumnanga Simba wa Yuda na kumdhalilisha marehemu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM ilikuwa ndo mlango wa haya yote.

Nchi imewashinda, kilichosalia ni kusaka na kuua watu wanaowapinga waziwazi.

Tuendelee kula nyama mtori upo chini
 
Naomba kutoa Raia kwa serikali kujiwekea utaratibu mzuri wa kuwadhibiti madereva. Hali ya sasa siyo nzuri sana mtaani na kwenye vijiwe. Yawezekana kweli uchumi siyo mzuri na maslahi ya madereva siyo mazuri kivile kutokana na elimu zao. Lakini pamoja na umaskini walionao haileti maana kufungua spear za magari mapya nakuziuza kisha kufunga spear zilizokufa. Haileti maana kufungua matairi mazuri yenye TBS na kufunga tairi zilizopitwa na wakati . Ni hatari sana kwao,

Zidumu fikra za watu wazalendo, zidumu hoja zenye tija, lidumu jukwaa la great thinkers
Mkuu, hapa umetoa ushauri mzuri sana, ila naomba urekebishe kidogo hapo, ni spare parts, au kwa lugha yetu ya Kiswahili ni vipuri.

Rekebisha tu hiyo ili hoja yako ikae vizuri, kwani neno spear ulilotumia hapa lina maana tofauti kabisa na muktadha wako.

Ova
 
Ila serikalini. People are getting away with murders! It's hurting. Honestly...
 
Ni kweli.....

Takukuru wapo tu..

Mie nasema tena nikija kuwa Waziri wa Mambo ya ndani kuna sehem mbili za kudili nazo.

Takukuru na Zimamoto.
 
Mabosi nao wanalilia kununuliwa gari la she. 400,000,000 magari ya kifahari kwa fedha za kodi za wananchi.

Ugonjwa huu wa kutothamini fedha za kodi ya wananchi siyo tu upo kwa madereva bali mabosi pia ngazi ya wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara na taasisi za serikali, wizara , mikoa na wilaya.

Fedha zinazopotea ni nyingi sana na inabidi watumishi wote wa serikali na taasisi zake wadhibitiwe ili hela hiyo iendee kununua vifaa tiba vya hospitali, kujena majengo ya shule hospitali na kujenga barabara n.k kwa matumizi ya walio wengi badala ya hela kubwa kwa matumizi ya kifahari kwenda kugharamia ofisa mmoja bosi wa taasisi ya umma na serikali.

TOKA MAKTABA :

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma amesema hajaridhishwa na manunuzi ya gari la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita aina ya V8 lenye thamani ya mil.400

1700732417634.png

Mbunge Joseph Musukuma (kushoto) ahoji mkurugenzi Mhandisi Modest Apolinary (kulia) wa Geita kununua gari la thamani ya Tshs.400 milioni kwa matumizi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Geita.
 
Naomba kutoa Rai kwa serikali kujiwekea utaratibu mzuri wa kuwadhibiti madereva. Hali ya sasa siyo nzuri sana mtaani na kwenye vijiwe. Yawezekana kweli uchumi siyo mzuri na maslahi ya madereva siyo mazuri kivile kutokana na elimu zao. Lakini pamoja na umaskini walionao haileti maana kufungua spear za magari mapya nakuziuza kisha kufunga spear zilizokufa. Haileti maana kufungua matairi mazuri yenye TBS na kufunga tairi zilizopitwa na wakati . Ni hatari sana kwao, kwa wanaowabeba na hata familia zao.

Lakini haya yote yanatokana na ukweli kwamba hakuna usimamizi wala anayefuatilia ufanisi wa vyombo vya usafiri vya serikali. Nikifuatilia sana aliyepewa dhamana ya kuwasimamia madereva ana masters na wakati mwingine hata Phd. Analipwa fedha nyingi lakini pia kwa ubosi wake siyo mtu wakwenda garage kufuatilia. Baadhi hata vifaa vyamagari awavifahamu hivyo kujua kibovu nakizima kwao kizungumkuti. Baadhi wamepewa dhamana hiyo kama adhabu huku baadhi wakiwa na mgongano wa maslahi kwa kushirikiana na madereva kuhujumu serikali kwenye matengenezo na mafuta.

Hali hii ya wizi wa mafuta na vipuri imekuwepo muda mrefu ila kwa sasa imezidi. Dreva anakuja na gari garage anawapa vijana wafungue vifaa na kufunga vibovu adharani bila hata kificho. Naandika kwa uchungu kwani magari mengi haya yananunuliwa kwa kodi zetu huku machache tukipewa msaada.

Kwa upande mwingine wapo madereva wanafungua vifaa hasa tyre za gari za umma nakufunga kwenye magari yao. Unajiuliza huyu Dreva akipata ajali na tyre mbovu nani atakayekuwa? Udhibiti wa kodi zetu upo wapi?

Nadhani serikali inaweza ikawa imelifumbia macho ila sisi tuliopo mtaani kwenye vijiwe na wamiliki wa garage tunaona. Hata kesho serikali ikitoa namba za whatsapp special watu watume picha za uhalifu huu watu watatuma. Siyo Busara magari ya kodi zetu yakafa kwa sababu ya watu wachache wanaonenepesha familia zao.

Leo tembelea ofisi za serikali uone magari yaliyopaki, ni mapya kabisa ila wameyakwapua vifaa vya ndani na kuuza kisha wameyaweka juu ya mawe. Kila ofisi ukienda magari ya serikali mapya yamepaki lakini huku mtaani hakuna bosi yeyote ambaye amepaki gari means watumishi wa umma wana pesa zakutunza magari kuliko serikali? Hapana, wanayaua makusudi kwa kuuza spear na kunenepesha miili yao.

Last time tuliona Mtanda akiwa huko Kaskazini anaenda ofisi ya mkurugenzi magari yamepaki kwa kifaa cha milioni moja; yakikaa baada ya muda wanaanza kuiba kifaa na kwenda kuuza......huu ndio uhujumu uchumi.

Ni yapi maoni yangu kwa serikali na jamii?
1. Maafisa usafirishaji serikalini wawe wataalamu wa fani ya usafirishaji waweze kusimamia vyema mali za umma ikiwemo pikipiki na magari..

2. Dreva atakayebainika ameiba au kuuza kifaa cha serikali afukuzwe kazi kulinda uhai wa anaowabeba akiwemo bosi wao

3. Magari yote mapya yaliyopaki kwenye ofisi za umma viongozi wa hizo taasisi wawajibishwe ikiwemo kufukuzwa kazi kwa kuhujumu uchumi wa wananchi . Gari ya milioni mia mbili inapaki hadi kufa kwa kukosa huduma ya milioni moja au mbili?

4. Garage itakayobainika ina spear zilizotolewa kwenye gari za serikali mmiliki awajibishwe ikiwemo kuthibitisha alipotoa spear husika.

5. Serikali ipige marufuku gari za serikali kuingia garage zisizo rasmi na pale zinapopaki au kuingia pawepo na kibali maalum cha kufanya hivyo.

6. Serkali itoe namba maalumu kwa umma ya kusaidia kuripoti matukio ya uhujuma kwa mali za umma.

7. Utaratibu wa kuwauzia watumishi hasa viongozi wa umma magari uangaliwe upya kwani unachangia wao kuua magari kwa lengo la kujiuzia.

Zidumu fikra za watu wazalendo, zidumu hoja zenye tija, lidumu jukwaa la great thinkers
Hekaya za Abunwasi
 
Nchi hii Ina madudu mengi kwenye kila idara.....yaani unaweza kupasuka kichwa kwa kuwaza na kuwa mzalendo.....

Madudu na uchafu vinaanzia ngazi ya juu kabisa....huko ndio kinatoka funza.......kila siku tunasikia hapa wizi wa mabilioni kama sio matrilioni kwenda ripoti za mkaguzi mkuu..... lakini hatujawahi kuona hata mmoja akiwajibishwa......

Hakuna wa kumnyooshea mtu kidole kwani wote ni wezi na wamejiwekea utaratibu wa kuiba bila kuingiliana mfano wa mbuzi waliofungwa kamba kula nyasi.......

Sasa kama huko juu kumeoza huko chini kutakuwa na hali gani.........??

Kwa kweli ili nchi hii irudi kwenye mstari labda kupigwe bomu tuangamizwe wote na waje watu waaanze upya......ila sio sisi tuliopo maana tayar wizi na ubadhilifu upo kwenye vinasaba vyetu kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa........
 
Back
Top Bottom