Serikali na Hatima ya ATCL

Serikali na Hatima ya ATCL

Rais Kikwete awashutumu watendaji ATCL kwauzembe
*Waziri Kawambwa atoa muda wa siku saba wajieleze

Na Waandishi Wetu

WAKATI Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa kufungiwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kumetokana na uzembe wa watendaji wa shirika hilo, Waziri wa Miundombinu, Shukuru Kawambwa ameipa bodi ya shirika hilo siku saba kueleza chanzo cha kudorora kwake.

ATCL imefungiwa kurusha ndege zake ndani na nje ya nchi baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA), kuipokonya cheti cha usalama wa anga (AOB) kutokana na uzembe katika kujaza nyaraka za usalama wa anga kulingana na sheria za mamlaka hiyo.

Hatua ya TCAA ilifuatiwa na uamuzi wa Umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani (IATA) kuizuia kufanya shughuli zozote za biashara ya usafiri wa anga.


Kikwete, ambaye yuko nchini Msumbiji kwa ziara ya siku tatu ya kikazi, alisema katika utaratibu wa kawaida shirika hilo na mengine hufanyiwa ukaguzi na TCAA na kwamba, katika kipindi hicho ATCL ilipewa notisi ya miezi mitatu na muda wa ziada kuwasilisha nyaraka zake kwa ukaguzi.

Lakini akaongeza kuwa pamoja na kuongezewa muda, shirika hilo lilishindwa kufanya hivyo na badala yake ATCL ikawasilisha TCAA nyaraka zenye mapungufu na kusababisha kufungiwa.

Rais Kikwete aliyekaririwa na kituo cha televisheni cha TBC1 kutoka Msumbiji juzi usiku na jana, amemtaka Waziri wa Miundombinu kukutana na bodi ya ATCL haraka, kuhakikisha bodi hiyo na menejimenti inatoa maelezo kuhusu uzembe huo pamoja na kuchukua hatua kuiwezesha ATCL kuanza kazi ndani ya siku 10.

Kwa mujibu wa TBC1, sambamba na hatua hiyo, serikali pia ipo mbioni kuiongezea mtaji ATCL kwa lengo la kuiwezesha kuboresha huduma zake na kujiendesha kibiashara.

Katika miezi ya karibuni ATCL imekumbwa na wimbi la matatizo mbalimbali, ikiwemo hali mbaya kifedha iliyosababisha wafanyakazi wake kulipwa kwa mafungu mshahara wao wa mwezi Novemba.

Hata hivyo, bodi ya ATCL imesisitiza kuwa serikali isipolipa deni la Sh20 bilioni na kuongeza mtaji wa Sh70 bilioni, itakuwa ndoto kufanikisha mipango ya kuliunda upya shirika hilo, anaripoti Leon Bahati.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Mustapha Nyang'anyi alisema dawa ya ATCL ni kulipa deni hilo na kuongeza mtaji kwa dola 67 milioni za Kimarekani.

Alikanusha madai kuwa kuyumba kwa ATCL kumetokana na uzembe wa watendaji, akisema tatizo kuu ni serikali kutotekeleza ahadi za kulifufua shirika mara baada ya kuvunja mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) Machi, 2007.

"Hata tukirudishiwa leseni bado hatuwezi kutatua matatizo hayo. Kama serikali ingelipa deni, angalau tungeweza kukopa benki. Lakini katika mazingira ya deni hili hatuwezi kukopeshwa," alisema waziri huyo wa zamani wa mawasiliano na uchukuzi.

"Udhaifu wote unaoonekana sasa tuliuona tangu awali na ndio maana tuliiambia serikali watupe fedha hizo za kulisuka upya shirika. Uzuri, wao (serikali) ndio waliotuomba tufanye tathmini na Aprili 30 mwaka 2007 tukaikabidhi Wizara ya Miundombinu mpango wa biashara wa miaka mitano pamoja na kiwango cha fedha kinachohitajika. Hadi leo hatujapewa chochote," alilalamika Balozi Nyang'anyi.


Katika hatua nyingine, serikali imempa siku saba mwenyekiti wa bodi ya ATCL kutoa maelezo ya kina yaliyosababisha shirika hilo kupoteza mwelekeo na kusimamishiwa leseni ya kuruka angani- siku zinazoisha Desemba 22, anaripoti Peter Edson.

Serikali pia imesema ili ATCL iweze kurudishiwa leseni yake na kuanza kufanya kazi kama ilivyokuwa mwanzo ikizingatia taratibu zote za Mamlaka ya anga duniani, inahitaji kiasi cha Dola 273 milioni za Kimarekani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alisema serikali imesikitishwa sana na kitendo cha ATCL kusimamishiwa leseni, akisema suala hilo linaathiri uchumi wa nchi.

"Hatuwezi kuoneana aibu mambo ya nchi yanapoharibika, tumempa mwenyekiti wa bodi siku saba kutoa maelezo ya kina, ili waliohusika kuliangamiza shirika waweze kuwajibishwa," alisema Dk. Kawambwa.

Alisema fedha ambazo zinatakiwa ili kuirudisha ATCL katika shughuli zake za kawaida ni nyingi, ikizingatiwa kuwa hazikuwa kwenye bajeti yoyote ile.

Alisema serikali kwa kushirikiana na bodi ya wakurugenzi tayari imeshazipata fedha hizo na tayari juhudi za kupitia upya kanuni na sheria za uendeshaji wa ndege zimeanza kufanyika ili kulinusuru shirika hilo.

Dk. Kawambwa alisema utekelezaji wa mpango huo wa kuboresha shughuli za shirika, kwa lengo la kukidhi kanuni na sheria stahili za mamlaka ya anga ulishaanza tangu Desemba 11 na unategemewa kuisha Desemba 24 wakati ndege za ATCL zitakaporejea angani.

Aliongeza kuwa mkurugenzi huyo akishapeleka maelezo ya kina kuhusu sakata hilo, watendaji wote watakaobainika kuwa kwa namna moja au nyingine walihusika kulihujumu shirika hilo watawajibishwa kwa kanuni na sheria.

"Katika jambo hili hatuna masihara hata kidogo, tutahakikisha tunapata ufafanuzi wa kutosha na kuchukua hatua kwa masilahi ya taifa," alisema Dk. Kawambwa

Alisema haitawezekana watu wachache kuharibu kazi na uchumi wa taifa wakati serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kuliboresha shirika hilo ili liweze kumudu shughuli zake.

Alisema kusimamishwa kwa ATCL kuruka angani ni changamoto kwa nchi, kwani athari zake ni kubwa kutokana na ukweli kuwa litakuwa haliingizi fedha yoyote.

"Watumishi wa ATCL wataendelea kudai mishahara yao kwa mujibu wa taratibu, lakini shirika halizalishi, fedha za mishahara zitatoka wapi?" Dk. Kawambwa alihoji.

Alisema pamoja na changamoto hiyo, bodi ya wakurugenzi pamoja na shirika hilo wanawajibika kutafuta fedha za mishahara ya wafanyakazi wao katika kipindi hiki ambacho huduma zimesitishwa.

"Tumewaeleza kuwa serikali haitapenda kusikia wafanyakazi wanakosa mishahara "

Alisema nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa ATCL inarudia kazi zake mapema iwezekanavyo na kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo ya taifa badala ya kuwanufaisha watu wachache.

Hatua ya TCAA kuipokonya cheti cha usalama wa anga ilichukuliwa baada ya Kitengo cha Ukaguzi cha Umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani (IOSA) kulikagua shirika hilo mwaka jana na kubaini mapungufu 482, lakini ATCL haikurekebisha makosa hayo.

Novemba mwaka huu, Mamlaka ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO) iliikagua TCAA na kubaini kuwa nyaraka zilizojazwa na ATCL zilikuwa haziendani na sheria za mamlaka hiyo ya Tanzania na hivyo kuishauri iipokonye cheti hicho cha usafiri wa anga.


Tayari ATCL imeshasema kuwa imerekebisha mapungufu hayo na kuziwasilisha nyaraka hizo TCAA, ambayo iliahidi kuzishughulikia katika muda wa siku 10 za kikazi.

Mwandishi wetu, Salim Said anaripoti kuwa baadhi ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, ambazo ni kati ya waathirika wa matatizo ya usafiri ya ATCL, zimepongeza uamuzi wa IATA wa kulifungia shirika hilo la ndege.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, makatibu Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wamesema hatua hiyo ni stahili ya ATCL na wala si uonevu.

Katibu mkuu wa Bakwata, Sheikh Ally Juma Mzee alisema kutokana na utendaji mbovu wa ATCL, Waislamu 1,500 walipata usumbufu wa kulala Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa zaidi ya siku 11 mwaka jana wakati wakielekea Maka kwenye ibada ya Hija.

Licha ya Usumbufu huo lakini Waislamu/mahujaji hao hawakulipwa fidia pamoja na serikali kuwaahidi kifuta jasho, jambo lililozipelekea baadhi ya Taasisi za Kiislamu kuingilia kati na kuahidi kuwa wataliburuza mahakamani shirika hilo.

"Waislamu nchini ndio waathirika wakuu wa uzembe wa viongozi wa ATCL, hatua ya kuifungia si uonevu bali ni stahili yao kutokana na uzembe unaofanywa na uongozi wa shirika hilo," alisema Sheikh Mzee.

"Hili ni fundisho kwanza kwa uongozi wa ATCL na ni aibu kwa shirika linaloongozwa na wasomi na watu ambao walishashika nafasi kubwa serikalini kufanya uzembe wa hali ya juu katika utendaji wao," alisema.

Naye katibu mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam Tanzania, Sheikh Ramadhan Sanze alisema hatua hiyo ni sahihi na kulaumu kuwa imechelewa kwa kuwa ilistahili kuchukuliwa tangu mwaka jana wakati shirika hilo lilipokwamisha safari za mahujaji.

"Hii ilikuwa ichukuliwe tangu mwaka jana imechelewa sana, lakini tatizo si ATCL bali tatizo ni viongozi wake ambao ni wazembe na hawana historia nzuri ya utendaji katika sehemu zote wanazoongoza," alisema Sheikh Sanze.

Sheikh Sanze alisema mwenyekiti wa bodi ya ATCL, Mustapha Nyang'anyi ana kashfa ya kununua kivuko kibovu cha Kigamboni katika miaka ya tisini wakati huo akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.

Source: Mwananchi Online

Neno moja: UZEMBE
 
Siku saba za nini tena wakati watu wameshashindwa kazi na kuliua shirika!!!? 😕
Fukuza kazi management yote na Board of Directors mara moja!!!
 
Let ATCL collapse. Enough is enough. No need to pump over 100million dollars for what?? hizo hela kama zipo zisaidie wakulima kwenye mbolea, pembejeo na mbegu bora.

Kwani bongo ukitaka ticket ya ndege si unakata Precision au???

It is good to have ATCL, lakini the cost is too much.
 
Kama kweli wanataka kuisafisha ATCL inabidi wawatimue manungayembe ya akili yote ambayo yapo kwenye uongozi hivi sasa, watoe hata matangazo ya kazi sehemu mbalimbali ili watu wenye uwezo waje kufanyiwa interviews kwenye positions zote na sio kuchagua some stupid fat cats ambao genes za akili zao zimeshakuwa mutated to stupidness. Moja ya requirements ambayo mtu atakiwa kuja nayo kwenye kuomba kazi hasa ya CEO ni kuja na overhauling plan na aweze kui-defend vilivyo.
 
Kama kweli wanataka kuisafisha ATCL inabidi wawatimue manungayembe ya akili yote ambayo yapo kwenye uongozi hivi sasa, watoe hata matangazo ya kazi sehemu mbalimbali ili watu wenye uwezo waje kufanyiwa interviews kwenye positions zote na sio kuchagua some stupid fat cats ambao genes za akili zao zimeshakuwa mutated to stupidness. Moja ya requirements ambayo mtu atakiwa kuja nayo ni kwenye kuomba kazi hasa ya CEO ni kuja na overhauling plan na aweze kui-defend vilivyo.

Duh! mazee wewe ukiwa interviewer nitakuogopa....sitakuja kwenye hiyo interview....lol
 
Duh! mazee wewe ukiwa interviewer nitakuogopa....sitakuja kwenye hiyo interview....lol

hahahahahah Mazee unajua inabidi waajiriwe watu ambao wana uwezo wa kuweza ku-think outside the box na kuwa na innovative ideas. Tumeshazoea kuteua watu kwenye nafasi hizo kiushikaji kisa tu mtu unakunywa nae beer na hapo kunakuwa hakuna accountability, kwa sababu tusipoukuwa makini hii meli yetu ndio inaendelea kuzama.
 
Yap, niliyasema kabla ya habari.. Haya sasa tumefikia ukingoni kuua ATCL...
Hivi hao viongozi wa ATCL wanaposema serikali haikuwapa kitu toka wajitenge na South hiyo mitumba ya ndege walinunua kwa fedha toka wapi?...

Again, Ufisadi wakuu zangu upo ktk kila taasisi ya serikali na binafsi siafiki kifo cha ATCL kuna great risk ya kupoteza kiungo muhimu ktk uchumi wa nchi..Ndege wakuu zangu ni sawa na chunvi ktk mboga sio lazima iwe ndio kinachotupa shibe kiuchumi lakini ni kiungo muhimu sana ktk Usafiri na hasa dunia ya leo.. Ikiwa serikali inaweza jenga mabarabara, madaraja na kadhalika iweje swala la usafiri wa anga liwe dogo kiasi hicho!..
Ni kutokana na kukosekana kwa usafiri Barricks, Mwadui Diamonds na mashirika mengine ndege zao zikitua na kuruka kama vile wapo kwao, na kibaya zaidi hatufahamu huwa wanaondoka na vitu gani kwa sababu ukiondoa tofali moja ktk mjengo basi kila kitu huporomoka!
 
Du, Mkuu Mkandara naona hapa umekosea sana.

ATCL wanataka over 200 million USD, sasa kweli unaweza kuniambia faida gani itapatikana wakipewa hizo pesa??? Kweli 200 million USD zikipelekwa kwa wakulima si tutaona maajabu na hizo hela zitakuwepo kila mwaka kwani mbolea, matractor na dawa zitatolewa kwa mikopo.

Na tukifanya hata worst case scenario, hizo hela wakulima wakizipoteza kama ambavyo ATCL BLACK HOLE will guarantee kupoteza, si ni afadhali wakulima wengi watafaidika??

Sasa kama airlines ni muhimu sana mbona US govt wao hawaown hata hiyo airline yenye govt name US Airways au hata American airlines???

Hapana mkuu ATCL imeshakufa, tukiamua kupoteza hizo hela sio tena humu ndani muanze kusema ooh serikali imechemsha. Hakuna cha uongozi wala nini, ATCL is dead na bila Capital infusion there is no way out. Na hiyo Capital infusion pia sio kwamba italeta faida, ila itaprolong date ya kuzikwa.
Kwani jamani airline business ni profitable hivyo mpaka watu mnakazania ATCL itufilisi nchi??? Biashara yenyewe kichaa part from Emirates, airlines nyingi ni losses tu.
 
Siku saba za nini tena wakati watu wameshashindwa kazi na kuliua shirika!!!? 😕
Fukuza kazi management yote na Board of Directors mara moja!!!

Nina shangaa!!
Wanpewa siku 7 za nini wakati hata wakipewa Muongo mmoja hawatatekeleza jambo?

Tanzania watu hawafukuzwi kazi wanasubiriwa wafe wenyewe na hata wakifa wanaendele kulipwa mishahara na malupulupu ya safari, sjui safari ipi?

Fukuza Mkurugrnzi na MWenyekiti wa Bodi.
Piga panga Bodi nzima.
Timua kila aliye na mkono kwenye kifo cha ATCL.
Kisha unda Upya.

Tatizo analo MH Kikwete, ambaye hana masikio wala moyo wa kujenga nchi, siyo ATCL
 
Sina shaka kabisa kuwa katika ATCL kuna ufisadi uliokubuhu unaotakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Hivi ilikuwaje hawa jamaa wakaanza kutumia ndege za aina ya AIRBUS badala ya BOEING, ndege ambazo hawakuwa na marubani wala maengineer wa kuzihudumia? Hapa nadhani kuna umuhimu wa kufahamu nani alikuwa kinara wa hoja au alishinikiza kampuni ikodishe AIRBUS na kwasababu zipi? Hii ndege ndio imeiletea dhahama kubwa ATCL; inasemekana viongozi wa shirika kwa kupitia kwa wakala wa kampuni iliyokodisha ndege wanapata mgao wao wa 10% kila mwezi malipo ya $ 360,000 yanapofanyika; ndio maana viongozi hao wako radhi wafanyakazi wasilipwe mshahara lakini kampuni ya wallis ililpwe hata kama ndege haingizi mapato yoyote!! Kulaleki walahi kuna watu wanajua kuila nchi.
 
JAMANI PAMOJA NA LAWAMA ZOTE NI KAIWAIDA YA SERIKALI KUFICHA UKWELI. NAOMBA MSOME HII ARTICLA ILITOKA KENYE TRAVEL NEWS MAGAZINE. TATIZO LA WAANDISHI WETU HAPA HAWAFANYI UCHUNGUZI WA KINA KUJUA TATIZO NINI. HUYO MWANDISHI KAELEZA CHIMBUKO LA YOTE HAYA. HAPPY READING!


By Wolfgang H. Thome, eTN Africa | Dec 15, 2008


The CEO and managing director of Air Tanzania, David Mattaka, has reacted promptly to reports that the Tanzanian Civil Aviation Authority (TCAA) had suspended their AOC (Air Operator Certificate) and effectively grounded the airline on December 9.

Mr. Mattaka explained that the suspension did not arise from safety, training or maintenance issues but over discrepancies in documentation as required by global aviation bodies. During the International Air Transport Association (IATA) Operational Safety Audit reportedly some irregularities in documentation were discovered, but the airline has said most of the items pointed out at the time had been rectified and resolved, but that the deadline set was probably too tight to achieve a 100 percent compliance.

The CEO also left no doubt that the government’s failure of meeting their financial obligations towards the airline had substantially contributed as a key factor to the woes of Air Tanzania. This in fact has been reported repeatedly in this column in the past.

TCAA was tightlipped over the prospects of the Air Tanzania Company Limited (ATCL) to resume flights within a fortnight as indicated by airline sources and the only available comment was that all submitted documentation by ATCL would be studied and evaluated before returning their operating permits, or else keep the airline grounded.

However, there is also indication from usually reliable aviation sources in Dar es Salaam, that a recent the International Civil Aviation Organization (ICAO) audit of TCAA in November has raised alarm bells at the global body as it put the regulators on the spot themselves and left them little if any chance but to jump into (re)action mode to avoid being sanctioned by ICAO, as had happened in previous years to Sierra Leone and the Democratic Republic of Congo. It is speculated that Air Tanzania was probably an “easy target” to show some action towards the ICAO demands, but this saga is certainly not ending here or now, irrespective of the outcome of the ATCL suspension.

Intriguing were also comments from TCAA staff that all ATCL aircraft were “airworthy,” adding further suspicion of an ulterior motive by sections of the regulatory staff.

Meanwhile, the unions too waded into the argument with complaints over unpaid wages, but as usual their way over the top demands, made probably by simply not understanding a thing about aviation, are bound to be thrown out by the company and the political oversight with the contempt they deserve.
 
Ni jambo la kushangaza kwamba waziri anasema katoa siku saba jana wakati hizo siku saba zimetolewa tangu na jumatatu wiki hii! Wakati anazungumza jana majibu alikuwa nayo kwa nini hakusema nini kimejibiwa ili umma ujue? Ni siasa "tupu"!
 
Yap, niliyasema kabla ya habari.. Haya sasa tumefikia ukingoni kuua ATCL...
Hivi hao viongozi wa ATCL wanaposema serikali haikuwapa kitu toka wajitenge na South hiyo mitumba ya ndege walinunua kwa fedha toka wapi?...
Again, Ufisadi wakuu zangu upo ktk kila taasisi ya serikali na binafsi siafiki kifo cha ATCL kuna great risk ya kupoteza kiungo muhimu ktk uchumi wa nchi..Ndege wakuu zangu ni sawa na chunvi ktk mboga sio lazima iwe ndio kinachotupa shibe kiuchumi lakini ni kiungo muhimu sana ktk Usafiri na hasa dunia ya leo.. Ikiwa serikali inaweza jenga mabarabara, madaraja na kadhalika iweje swala la usafiri wa anga liwe dogo kiasi hicho!..
Ni kutokana na kukosekana kwa usafiri Barricks, Mwadui Diamonds na mashirika mengine ndege zao zikitua na kuruka kama vile wapo kwao, na kibaya zaidi hatufahamu huwa wanaondoka na vitu gani kwa sababu ukiondoa tofali moja ktk mjengo basi kila kitu huporomoka HII [/SIZE]!



FEDHA ZILITOKA KWA MCHINA ANAYETAKA KUWEKEZA KWENYE SHIRIKI, MITUMBA AU MPYA SINA UHAKIKA

SIO KWELI, BARRICK ANA UHURU WA KUTUMIA NDEGE YOYOTE, ATCL HAWANA NA HAWAJAWHI KUWA NA NDEGE ZA MIZINGO

Let SAY Serikali iliyoahidi kujitoa muhanga kuendeleza shirika hili na ikaunda board na kuteua CEO, ikaomba ipewe strategic/business plan, ikapewa na kuambiwa kama inatataka kulifufua iongeze mtaji. Haikuongeza mtaji ikaruhusu waendelee HIVYO HIVYO kwa kujikongoja, WHAT DO YOU EXPECT jamani watanzania wenzangu?

Kama iliona hiyo plan haitekelezeki kwanini haikuwaondoa hao watu?
Hamuoni kuwa ni chanzo cha AIBU HII?
 
Sina shaka kabisa kuwa katika ATCL kuna ufisadi uliokubuhu unaotakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Hivi ilikuwaje hawa jamaa wakaanza kutumia ndege za aina ya AIRBUS badala ya BOEING, ndege ambazo hawakuwa na marubani wala maengineer wa kuzihudumia? Hapa nadhani kuna umuhimu wa kufahamu nani alikuwa kinara wa hoja au alishinikiza kampuni ikodishe AIRBUS na kwasababu zipi? Hii ndege ndio imeiletea dhahama kubwa ATCL; inasemekana viongozi wa shirika kwa kupitia kwa wakala wa kampuni iliyokodisha ndege wanapata mgao wao wa 10% kila mwezi malipo ya $ 360,000 yanapofanyika; ndio maana viongozi hao wako radhi wafanyakazi wasilipwe mshahara lakini kampuni ya wallis ililpwe hata kama ndege haingizi mapato yoyote!! Kulaleki walahi kuna watu wanajua kuila nchi.

I agree we would like to know who was behind that ridiculous decision. Their needs to be an investigation and someone needs to end up in Jail one way or another. I refuse to believe that this is just pure incompetence and laziness. Nobody can possibly be that stupid.
 


It was just a matter of time 'kabla bomu halijalipuka!'

...hivi, watendaji hao hao wanaokuwa "recycled" miaka nenda rudi mlitegemea wangefanya miujiza gani kuliokoa shirika hilo? au kwakuwa shirika lilikuwa linarusha ndege angani?

Serikali inakemea, wakati serikali ya nchi hii ilifumbia macho vifo vya mashirika mengine ya umma?

wapi KAMATA, NASACO, TRC? ...kama serikali ilishindwa kuokoa mashirika yake ya Umma huko nyuma, hizi kelele za siku saba ni funika kombe mwanaharamu apite

...kwa kifupi, Serikali "haiwezi" kuendesha mashirika yake ya umma!
 
Ni jambo la kushangaza kwamba waziri anasema katoa siku saba jana wakati hizo siku saba zimetolewa tangu na jumatatu wiki hii! Wakati anazungumza jana majibu alikuwa nayo kwa nini hakusema nini kimejibiwa ili umma ujue? Ni siasa "tupu"!

I have got a feeling five years term haitoshi kuongoza nchi bora tufanye term moja miaka 10, Yaani kitu hakiitaji hata darasa la saba unampa siku saba wakaji jibu unalo wameshindwa kazi
Mpaka sasa hizi hakuna hata kimaoja kilicha fanywa kutoka kwenye ahadi za uchaguzi
 
FEDHA ZILITOKA KWA MCHINA ANAYETAKA KUWEKEZA KWENYE SHIRIKI, MITUMBA AU MPYA SINA UHAKIKA

SIO KWELI, BARRICK ANA UHURU WA KUTUMIA NDEGE YOYOTE, ATCL HAWANA NA HAWAJAWHI KUWA NA NDEGE ZA MIZINGO

Let SAY Serikali iliyoahidi kujitoa muhanga kuendeleza shirika hili na ikaunda board na kuteua CEO, ikaomba ipewe strategic/business plan, ikapewa na kuambiwa kama inatataka kulifufua iongeze mtaji. Haikuongeza mtaji ikaruhusu waendelee HIVYO HIVYO kwa kujikongoja, WHAT DO YOU EXPECT jamani watanzania wenzangu?

Kama iliona hiyo plan haitekelezeki kwanini haikuwaondoa hao watu?
Hamuoni kuwa ni chanzo cha AIBU HII?


Mkuu heshima mbele hapa tatizo si pesa hata kidogo tatizo ni kwanini hiyo AOC imenyanganywa na walipewa muda tangu mwaka jana kurekebisha hanma kilichofanyika.
Sijui hizo crisis meeting za kila siku walikuwa wanajadili nini
 
Nifahamvyo mimi ni Board na wakurugenzi wake hukutana angalau mara tatu kwa mwaka na sitting allowance kibao. Kukutana kufanya nini, kutathimini maendeleo ya kampuni. Haya sasa hawa mwenyekiti na baraza lake wamekuwa wakikutana kufanya nini, kujadili wapewe safari ngapi za bure??? inanikumbusha wakati wabunge walikuwa wanabishana bungeni eti waitweje, Mh au Mtukufu au ndugu, he,
Hapa ni kuondoa Mkiti na baraza lake, MD na timu yake anayepewa kampuni apewe na "Performance contract" mshahara upimwe kwa faida atakayotoa.
Siku hizi hata mtu anayekuandikia business plan unampa yeye kuimplement na ajilipe kutokana na faida, hapo ndio utashangaa visingizio vya kukataa kama ulikuwa hujamwambia kabla.
 
Nimehabarishwa kuwa Waziri wa MiundoMbinu baada ya kukutana na Waziri Mkuu amesema kuwa anatarajia kukutana na Viongozi wa wafanyakazi wa ATCL. Huu mkutano nadhani ni muhimu sana kwa wafanyakazi kutoa msimamo wao juu ya hali ilivyosasa. Tayari Waziri Shukuru anaielekeza Bodi na Menejimenti zitafute fedha za kulipa mishahara ya wafanyakazi. Kwa kweli ndugu zangu wafanyakazi hima-hima mkutane na Mheshimiwa Waziri kwani ile ligi ya kudai mafao inayoendelea kati ya wafanyakazi wa Ex-EAC na serikali soon itahamia kwenu.
Inajulikana wazi kuwa ATCL haina fedha, iweje waziri aamrishe itafute fedha za kulipa mishahara? Jipangeni vizuri kabisa kuzungumza na serikali juu ya mustakabali wenu. Ni vema baada ya mazungumzo yenu mkubaliane na serikali mambo gani yatafanyika na kwa muda gani. Ikiwezekana, Waziri ateue afisa wa wizara yake ambaye atakuwa desk officer wa ATCL kwa muda huu.
 
nDUGU WANANCHI,KUMEKUWA NA MAWAZO YA WATU MBALIMBALI AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE WANAPEWA MADARAKA YA KUONGOZA NCHI MAKAMPUNI AMA MASHIRIA MBALIMBALI KWA KUPEANA AMA KUJUANA KINDUGU,,SASA BASI IMEFIKA SASA WANANCHI WAMEONA BASI INATOSHA NA YOYOTE ALIETUMIA MADARAKA YAKE VIBAYA LAZIMA AFIKISHWE KWENYE MKONDO WA SHERIA,,JF KAMA SEHEMU YA KUFUNDISHANA NA KUMSHAURI RAISI NINI AFANYE NANAI AMTEUE...TUMEONA MAWAZIRI MBALI MBALI MRH MRAMBA NA MH YONA WAKIKWAA GARI LA KIJANI KUELEKEA KEKO KUJIBU TUHUMA ZA UBADHIRFU WA MALI YA UMMA KWA KUTOA MISAADA YA AJABU AJABU..SASA BASI HIVI SASA TUSIKIMBILIE TU SIMBA WAKUBWA WAKUBWA TWENDE KUWAONYESHA ADABU WALE WANAOPEWA HAKI YA KUONGOZA MASHIRIKA YA UMMA KAMA ,,BOT.TANESCO.TRLA,TTCL.ATCL NA MENGINEYO....MAJUZI NIMESOMA KIJARIDA KIMOJA KUTOKA HAPA JF KINAONYESHA JINSI BAADHI YA VIONGOZI WA ATCL WALIVYOLITAFUNA SHIRIKA LA AIRTANZANIA BILA AIBU...NA KILICHONIUMA ZAIDI NILIPOONA KUNA BAADHI YA WANABODI WAMEGAWANA DOLLER 11,000 NDANI YA WIKI MBILI HUKU KUKIWA NA WAFANYAKAZI AMBAO HAWAJALIPWA MISHAHARA YAO MPAKA LEO HII....NADHANI KUNA TATIZO KUBWA SANA KAMA KIONEKANAVYO HAPO CHINI...MH RAISI HIVI SASA TUANZE KUWAFUNDISHA ADABU HAWA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA WANAOIBA WAKIJUA UMEWACHAGUA NA HIVYO HAKUNA MKONDO WA SHERIA UTAKAOWAFWATA
NA KATIKA KUANZA NA HILI TUNAOMBA

MH MUSTAFA NYANGANYI NA MKURUGENZI WAKE BWANA DAVID MATTAKA WAWE FUNDISHO KWA WALE WOTE WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA MASHIRIK YA UMMA KUANZA KUYAHESHIMU KWA KUWAFIKISHA KWENYE MKONDO WA SHERIA(MAHAKAMANI),HARAKA IWEZEKANAVYO
NINA UHAKIKA KAMA MH UJUAVYO BWA DAVID ALIONDOLEWA KWA UBADHIRIFU PALE PPF NA KWA USWAHIBA WAKO UKAAMUA KUWASAKAZIA MASIKINI WAFANYAKAZI WA ATCL..NAAMINI KAMA ALIPOONDONDOLEWA
ANGEFIKISHWA KWENYE MKONDO WA SHERIA LEO HII ASINGE FANYA UBADHIRIFU WA HALI YA JUU KAMA UNAVYOSOMA HAPO CHINI.....

LENGO LETU SI TU WAJIUZULU MANAGEMENET NA BODI YAKE ,LA HASHA KUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KATIKA YALIOANDIKWA HAPO CHINI KUHUSU WIZI WA MALIZ A KAMPUNI HIVYO NI LAZIMA WARUDOSHE MALI ZA WATANZANIA.....HAIWEZEKANI GARI USED INANUNULIWA DUBAI KWA MILLION 25,000 MTU KWA MOYO WAKE WOTE NA KWA ROHO YAKE YOTE NA NAFSI YAKE ANAANDIKA GARI IMENUNULIWA KWA DOLLER 72,000.....
MFANO MDOGO NI HIZO NDEGENDOGO SOKO LA DUNIA KILA SEHEMU NI USD MILL4.5 LAKINI UNAAMBIWA WAMENUNUA KWA USD MILLION7.5....MFANO MWINGINE NI UNUNUZI WA AIRBUS...SOKO LA DUNIA NI 260,000USD LAKINI WAKANUNUA 360,000USD LEO HII WANGEKUWA WAPI KWA DIFF YA 100,000USD AMA 3MILLION USD KWA KILA NDEGE NDOGO WALIONUNUA...JE SWALI LANGU UKIACHA PESA WANAZOPATA KUTOKA KWA MARUBANI KAMA KAMISHENI DOLLER 3000USD INAINGIA MIFUKONI MWAO MOJA KWA MOJA NA USHAHIDI UPO....KUNA HAJA GANI YA WAO WAJIUZULU TU..

TUNAOMBA MRAISI WOTE WALIOSHIRIKI KUIUA ATCL WAFIKISHWE MAHAKAMANI MARA MOJA
WAKO SWEETBABY
UKIPENDA MALOVE
 
Back
Top Bottom