Serikali na Hatima ya ATCL

Serikali na Hatima ya ATCL

Ninashauri kwamba serekali iunde tume ya kujadili makosa yaliofanyika ATCL na kuwajibisha wale watendaji waliofanya makosa yaliosababisha mambo yote haya....hii ni aibu!
 
Ninashauri kwamba serekali iunde tume ya kujadili makosa yaliofanyika ATCL na kuwajibisha wale watendaji waliofanya makosa yaliosababisha mambo yote haya....hii ni aibu!

Tume haitakuja na jipya zaidi ya hili tunaloliona sasa.

Shida yetu ni kukosa moyo wa kuwajibika, kila mtu kwenye sehemu yake anaangalia maslahi yake.
Kifo cha ATCL kimetokana na mafaniko ya watu wachache na ambao wanaweza kushughulikiwa.

Masikini kodi yangu, hivi namlipa nani???????????
 
Kama ambavyo nilivyochangia katika thread nyingine iliyotangulia juu ya ATCL, ninawashauri viongozi wa wafanyakazi waitake serikali ikae nao ili waweze kujua hatima yao ikiwemo ni namna gani watalipwa haki zao. Kwa hali jinsi ilivyo kwa kuangalia mizania ya mahesabu ya ATCL ni kwamba haiwezi kuinuka na kurudia hali yake ya kawaida hata kama TCAA ikiiruhusu kurusha ndege zake. ATCL inasubiriwa itamkwe kuwa imekufa, sasa sijui wa kutamka hivyo ni nani?
 
Hali mbaya fedha inayoikabili ATCL inatosha kuiondoa katika ushiriki wake IATA. Kwa kawaida mashirika yote ya ndege yanatransact biashara zao baina ya shirika kwa shirika kupitia IATA na malipo kutoka shirika moja kwenda lingine hufanywa kwa mtindo wa Clearing House. Kwa hiyo IATA wana Clearing House kwa ajili ya kupitisha transactions za wanachama wao wanapofanya biashara.

Kwa mfano endapo abiria amekata Tiketi London-Mwanza na msafirishaji wa wake akawa British Airways katika njia ya Dar-London na ATCL katika njia ya Dar-Mwanza. Kwahiyo yule aliyepokea pesa kule London itabidi awasilishe sehemu ya nauli ya Dar-Mwanza kwenye Clearing House ya IATA ili ATCL aweze kulipwa. Sasa basi kama tiketi iliuzwa na ATCL basi hapo matatizo yana kuwa makubwa kwani ninaamini ATCL imekua haiwasilishi fedha za Airlines nyingine kule kwenye Clearing House na matokeo yake ni kusimamishwa uanachama, kwa kutotimiza wajibu wake.
 
Kamati siyo suluhuhisho la matatizo yote yanayotokea hapa nchini.suluhusisho ni kuhakiksha wale waliotufikisha hapa hawaendelei kubaki madarakani.

Either kwa kuweka watoto au vizazi vyao
 
Hapa pana maswali mengi ya kuwauliza wahusika. Unapopewa dhamana ya uongozi unakuwa umeaminiwa kuwa una uwezo wa kutimiza wajibu uliopewa na kuyafikia matumaini ya wale waliokupa dhamana hiyo. Ili uweze kuyafikia malengo ni lazima uyajue malengo na ujue namna ya kuyafikia.

Suali langu mimi ni kuwa hawa kina Nyang'anyi na Mataka waliyajua malengo na ATCL?

Walikuwa na Business Plan ya muda gani?

ILICHUKUWA MUDA GANI KWA WAO KUGUNDUA KUWA HAWAFIKII MALENGO?

Ni lini walijua wao pana tatizo katika hiyo biashara? Wakafanya nini?
Kwa hiyo waliona hasara inatokea, wakatulia, wakaendelea kama kawaida, halafu hasara ikaendelea, wakatulia, wakaendelea kama kawaida.

Huyu Mataka na Nyang'anyi walitegemea kitokee nini na lini ndio wachue hatua?

I think we are dealing with a serious Lack of vission, insensitiveness, lack of knowledge, incompetence, stupidity na ushenzi tuu!!

Lakini wakubwa niwaulize ni kwa nini tunategemea kuwa ni wajibu wa hawa wahujumu kujirekebisha na sio wajibu wetu sisi kuchukua hatua kali zaidi.

Mtu akipewa dhamana ya uongozi, akaleta madudu,ufisadi tunamnyonga. Maana ni wauaji kama wauaji wengine
 
Lakini wakubwa niwaulize ni kwa nini tunategemea kuwa ni wajibu wa hawa wahujumu kujirekebisha na sio wajibu wetu sisi kuchukua hatua kali zaidi.

Mtu akipewa dhamana ya uongozi, akaleta madudu,ufisadi tunamnyonga. Maana ni wauaji kama wauaji wengine

Mkuu unayo kila sababu kukasirika kama unavyoonesha kwenye bandiko lako.
Ila hiyo ya tunamnyonga ni way too far maana haipo kwenye taratibu zetu za utawala wa sheria.
Pia hiyo ya sisi kuchukua hatua kali zaidi laiti tungeweza haya tunayoyaona leo yasingetokea.Tatizo wenye mamlaka ya kuteua wanatuangusha kwa kutuwekea wasio na uwezo.Laiti kama teuzi hizi zingekuwa zinathibitishwa na Bunge au mamlaka huru basi tungepata faraja.
 
Pana tatizo tunapo mtegemea kikwete ndio awawajibishe hawa watu. Kwanza Nyang'anyi ana shida ya akili, mdhaifu mno, hajawaji kufanya jambo lolote linaloweza kufanywa kuwa ni la mfano, mimi sijui!

Mataka nae ana matatizo ya arrogance na ushenzi tu! Ni vigumu kumwelezea huyu mataka misimamo yake, imani yake, na pia anataka ni nini - ajira au anataka kuonyesha kipaji, au anataka nini hasa. Kwa nini hakuanzisha biashara yake alipotoka PPF ndio tukamchue huko baada ya kuoba performance yake.

Hawajaweza kufanya jambo lolote binafsi
 
...walisema kuwa Mattaka was so successful at PPF,na ATC would have been a piece of cake.Well,walisahau kitu kimoja,kuwa PPF alikuwa anakusanya michango ya wanachama,yeye kazi yale ni ku invest tu.Kapewa vyeo vikubwa...Managing Director&CEO. Akaanza kwa kujikopesha Mercedes Benz ML,na kununua ma Land Cruiser VX's toka Dubai.Its obvious kuwa aliingia na mentality ileile alikuwa nayo PPF.Alisahau kuwa ATC ilikuwa kwenye life support,yeye badala yake akaja kuingozea malaria juu! Hapa ndio huwa namkumbuka marehemu Sanare.

Umenena vema Mkuu!
Mzoea vya kunyonga vya kuchinja ataviweza wapi?
 
Kwa hiyo unakubaliana na jamaa wa Kenya wanaposema kuwa watanzania ni wajinga hawajui kutumia raslimali zao?

Kama kweli watanzania sisi siyo wajinga na wala hatukubaliani na upuuzi huo, je tutakubalina kuingia mitaani kuitaka serikali ituambie hela yetu ya kodi wanaitumiaje kama matokeo yenyewe ni haya. Huoni kuwa zoezi zima la ubinafshijai tangu lianze halijatusaidia watanzania ipasavyo ila faida zote zimekwenda mifukoni mwa viongozi. Pale Kenya wakati waziri alipotaka kujichukulia 2Gcent kwa kuuza hoteli akakabwa koo mpaka akatapika chengi zote? Lakini kwetu sisi jamaa anachukua 2Gcent na kutuficha nchi za nje na sote tunafahamu kabisa nchi nzima lakini bado tunamtetemekea, na hasa pale alipotuchinjia ngombe kila kijiji ndiyo tukasahau kabisa?


...teh teh, thank you for the 'akakabwa koo mpaka akatapika chenji zote!' I liked that. Time we did it too...!
 
Serikali itatoa tamko kuwa haihusiki na hasara na kuangamia kwa ATCL, lakiin Rais bado anamteua Mwenyekiti wa bodi na mkurugenzi mkuu wa shirika lililobinafsishwa!
 
Tena hawa Precision wamepata fursa ya kufanya watakavyo, labda Community AirLine wajiweke sawa mapema zaidi. Vinginevyo hali ya usafiri wa anga inazidi kuwa tete!
 
Historia itahukumu Waziri gani? ATCL ilfia mikononi mwake? Naamini Mashirika ya Umma si mbuzi asiye na Mchungaji, Namchungaji mwenyewe ni Waziri, hushiriki kuteua Wajumbe wa Bodi? Pia tukumbuke mzee Ruksa alijiuzuru uwaziri wa mambo ya ndani kwa vifo vya mahabusu shinyanga, wa si IGP kama sikosei?
 
Tena hawa Precision wamepata fursa ya kufanya watakavyo, labda Community AirLine wajiweke sawa mapema zaidi. Vinginevyo hali ya usafiri wa anga inazidi kuwa tete!

Walichotaka kitokee kimetokea. Hivi Mramba ameshaondoa hisa zake Precision?
 
Wameihujumu ATCL na kuifikisha pabaya hao hao waliotegemewa kuliokoa shirika!! Waliwayima mtaji ; sasa wawaondoe Nyan'ganyi na Mattaka wamlete mchina na wasimpe mtaji tuone kama ndege zitaruka na shirika litaendelea. Wadanganyika ndio tulivyo tumekwishasahau mambo ya NET GROUP ya Tanesco mara hii!!
 
"An inspection by IATA and TCAA jotted down more than 500 operational gaps" jamani hivi bado bodi ya ATCL haijatimuliwa tu? Wanasubiri nini? kikao cha mwisho wagawane posho?

Hivi hadi sasa bado management ya ATCL ipo kazini na wanalipwa na kodi ya mvuja jasho wa Tanzania?

DPP unasubiri nini kuwaburuza hawa mafedhuli mahakamani? 500 operational gaps ni criminal negligence...actually ni gross criminal negligence and dereliction of duty! wajumbe wa bodi pamoja na management nzima ya ATCL bado wako uraiani wanafanya nini? they belong in prison. hawa lazima walishwe dona na maharage wakati huu wa siku kuu.

DPP unasubiri hadi watu wafe ndio tuone uwajibikaji? JK uko wapi? ama kwa vile una ndege yako mwenyewe basi ya ATCL hayakuhusu? 500 operational gaps na bado watu wako uraiani wanatanua!!!

JK, DPP how many more operational gaps before you act? 600, 800, 1000, 2000?
 
..cha ajabu na uzembe wote huo na ufisadi wa hili shirika hakuna hata mbunge mmoja kwa kutumia kamati zao aombe uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika,hii kitu wanachezea maisha ya watu na pesa za walipa kodi!
 
Halafu baada ya Muda wabunge husika wanaanza kupiga kelele, kwanini ATC imeacha safari za kuleta Ndege kijijini kwetu, wakati shirika lina didimia wanakaa kama watazamaji?
Au ndege ikidondoka na akina sisi , hakuna kitakacho fanyika, lakini ikiwa ni wao wako tayari kuingia gharama za kwenda kutibiana SA, yaani uchumi wetu tunaua hivi hivi na heshima yetu huku tukipiga makofi, halafu tunajiuliza kwanini watu wanakosa ajira au tunauoa vichocheo vya uchumi
 
Back
Top Bottom