Serikali na Hatima ya ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na Hatima ya ATCL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundamilia07, Sep 12, 2008.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ATCL gets lease to fly again
  CHALES KIZIGHA
  Daily News; Friday,September 12, 2008 @00:04


  The financially troubled Air Tanzania Corporation Limited (ATCL) might soon get a loan amounting to some seven billion shillings from an international bank – all guaranteed by the government, it has been learnt. Impeccable sources close to the national flag carrier claimed yesterday that CITI Bank was looking into the airline’s request for a loan amounting to some 7.1bn/-.

  “Air Tanzania had approached several banks for such credit … the CITI Bank has agreed to look into its request and chances are things will work out positively,” the sources said. The sources also indicated that the airline needed the money to pay for staff salaries and administrative costs, among others. However, the sources claimed that the airline’s request for the money had since been rejected, and that the airline can no longer meet its mandatory operational costs such as fuel.

  The airline has been experiencing financial problems since 2004 when it incurred a loss of some 7.7bn/-, which improved somewhat when it broke its troubled marriage with the South African Airlines in late 2006. According to Treasury records, it held some 13bn/- by March last year. Some of the workers who did not want their names to be disclosed said the morale of the majority of the workforce has gone down because the company was nosing down.

  “The government has not kept its word on giving ATCL full support … it has not done so since we parted company with the South Africans,” they allege. ATCL, formerly known as Air Tanzania Corporation (ATC) was privatized on December 2, 2002 in a deal under which SAA acquired 49 per cent shares in the firm. SAA bought the 49 per cent shares for only $20m which largely went into shareholding – the rest going into capital and training accounts.


  Ndugu Wadau,
  Ndani ya wiki mbili hivi tumesikia serikali na ATC wakitoa taarifa mbalimbali na nyingine zikikinzana juu ya hali inavyoendelea ndani ya ATC.

  Sichelei kurudia tena na tena, maoni mengi mbayo yamekuwa yakitolewa kupitia kwa wadau mbalimbali na hata kwenye forum hii kwamba yasipuuzwe katu. Sehemu kubwa ya ushauri ambao umekwishatolewa, unatoka kwa watu ambao wako independent na maslahi yao kwa ATC ni chombo chao cha umma na walipa kodi tu.

  Hadi wakati huu sijasikia taarifa kamili toka kwa serikali ambayo tayari imekwishaelezea ni kiasi gani cha fedha ambacho imekwisha toa kwa ATC wakati wa mtafaruku na SAA na vilevile kiasi ambacho pia kimekwishatolewa baada ya SAA kujitoa. Nilimsoma Waziri Shukuru akiongea mbele ya bunge kuwa serikali haiwezi kuitupa ATC na zaidi ya hapo itahakikisha kuwa inaendelea kuwepo.

  Sawa, sina tatizo na kauli zake, lakini mambo ya kujiuliza hiyo ATC ambayo serikali inataka iwepo ni ATC gani? Ni ATC hii ambayo itakuwa inapewa mabilioni ya walipa kodi bila ya kupiga hatua? je ni kuwa serikali haioni tatizo la msingi liko wapi? Ni vema serikali nayo na watoa maamuzi wengine wakasema 'siasa sasa basi tufanye maamuzi kisayansi' na kwa haraka.
  Mabadiliko ya uongozi ndani ya ATC ni lazima ili kuweza kunusuru hali iliyopo na kufikia azma ya serikali ya kuona ATC inasimama yenyewe bila ya kudai pesa za walipa kodi.

  Fedha ambayo tayari ATC imekwishapatiwa nina hakika kuwa ni nyingi na ingeratibiwa vizuri kwa maana kungekuwa na uongozi madhubuti basi hali isingekuwa kama ambavyo ilivyo sasa.

  Niwahakikishia wasomaji wote hapa kuwa pesa ambazo serikali inatoa kwa ATC hazitaweza kulikwamua Shirika hilo hapo lilipo endapo hakuta kuwa na uongozi wenye uwezo wa kupanga mikakati mizuri ya kibiashara(Corporate Business Plan) inayotekelezeka na kuisimamia.

  Ninaishauri serikali kuwa ifanye mabadilko ya haraka ikiwezekana ikodishe menejimenti ambayo itapewa jukumu la kuindoa ATC hapo ilipo na kuiweka katika hali nzuri na inayoeleweka. Nina uhakika kabisa utaalamu na ari ya kufanya kazi waliyonayo wafanyakazi wa ATC itaunganishwa na kutumiwa vizuri na menejimenti ambayo inaelewa ni nini kinatakiwa kufanyika kwa wakati huu.

  Mwisho, ni vema Bodi ya ATC ikachapisha taarifa za Mahesabu ya Kampuni ambayo yamekwishakaguliwa ili wananchi na wadau wengine waweze kuona na kujua hali halisi jinsi ilivyo katika ATC. Taarifa za mahesabu siyo siri tena katika ulimwengu wa leo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2009
 2. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Punda...., umesema ambayo wakuu wengi wamekuwa wakiyasema - UONGOZI kwanza then UONGOZI tena, mwisho ni mambo ya MIPANGO na MIKAKATI!!!

  Natumaini wahusika wanayasoma haya manake ATCL imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu karibu miaka kumi sasa na tunaendelea kusema tunalipa pesa kulisaidia, tunalibinafsisha kulisaidia lakini mwishowe ni palepale, kudema dema!!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yaani hata fedha za kulipa mishahara hawana! Kweli ATCL imeshafariki, inasubiri kuzikwa tu
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi tatizo la ATCL ni fedha?
   
 5. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Poor Management, lack of efficiency na politiki zinazoingizwa humo!!!!
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hiki ni kisingizio cha Management ya ATCL. Hata wakimwagiwa mabilioni ya kutosha kama Management ni mbovu hawawezi kwenda mbali.

  Kwani yale mashangingi waliyokopeshana Management hela walizitoa wapi? Hilo ni dalili tosha kwamba management inaangalia maslahi binafsi zaidi kuliko maslahi ya kampuni/shirika. Utatoaje mikopo ya mashangingi kwa management wakati huna uhakika wa kulipa mishahara ama ku-meet administrative costs?

  Kuna elements za kifisadi pia. Kila deal wanalofanya lazima kuwe na ufisadi na matokeo yake kama kuna faida inayoweza kupatikana kutokana na kukodi ndege basi hapo lazima imezwe na kamisheni za ufisadi.
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni masikitiko kwamba waandishi was habari kama Charles Kizigha, ambaye tena aliwahi kufanya kazi ATC hawezi kuandika habari kuhusu ATCL ikaeleweka kwa wasomaji. UKweli ni huu.
  Hiyo 13 bilioni inayosemwa kwamba wamepewa ATCL imetolewa na Serikali wakati ATCL ikiwa chini ya uongozi wa South African Airways (SAA). Baada ya uongozi wa SAA kuondoka na kuchaguliwa bwana David Mataka serikali haijawahi kutoa hata senti moja kwa ATCL na Bodi mpya licha ya kuhaidi kufanya hivyo! Kumlaumu Mataka kwamba hafai ni kutoelewa hali halisi ya nini kinatokea. Serikali inatumia takwimu hizi (13 bilioni) kama kiini macho lakini haijatoa hata "ndururu" kwa uongozi wa kizalendo wa ATCL. Mataka amejitahidi kuendesha shirika hili katika mazingara magumu sana.
  Mwenye masikio na asikie.
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ..........mwaka 2010 wala si mbali...........nyie endeleeni kupigia kelele EPA....bao la kisigino latengenezwa.......Shukuru ni kiungo mchezeshaji
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mtu mwenye mfuko uliotoboka ukimuongezea fedha mfukoni zimsaidie, mfuko wake utajaa?
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  ....mfuko ulitobokaje vile............ hivi nani aliutoboa vile?
   
 11. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  WELCOME TO AIR TANZANIA
  Good morning, Ladies and Gentlemen. This is yr captain MAFURU. On behalf of Air Tanzania Ltd, I’m welcoming both seated and standing passengers on board of Air Tanzania Boeing 767. We apologize for the six-hour delay in taking off, it was due to bad weather and some bad traffic from Tegeta to the Airport, Dala Dala’s are all full in the morning hours and traffic not moving. This is flight 712 From Dar es Salaam to Mwanza. Landing there is not guaranteed, but we will end up somewhere in the Lake Zone. And, if luck is in our favor, we may even be landing on your village!
  Air Tanzania has an excellent safety-record. In fact, our safety standards are so high, that even pick-pockets, snatchers and bandits are afraid to fly with us!
  It is with pleasure; I announce that, starting this year, over 30% of our passengers have reached their destination If our engines are too noisy for you, on passenger request, we can arrange to turn them off! To make your free fall to earth pleasant and memorable, we serve complimentary KONYAGI and Our favorite local brew MNAZI, you can also get GONGO if you promise not to drink more than half a bottle. For our not-so-religious passengers, we are the only airline who can help you find out if there really is a God!
  We regret to inform you, that today's in-flight movie will not be shown as we could not record it from the ITV due to UEFA Champions League live broadcasting. However, we have bought 10 copies of SANI Magazines and 12 copies of NIPASHE to supplement the movie. There is no smoking allowed in this airplane. Any smoke U see in the
  cabin is only the early warning system on the engines telling us to slow down or our stewards might be making TEA for the cockpit crews including myself In order to catch important landmarks, we try to fly as close as possible for the best view. If however, we go a little too close, do let us know. Our enthusiastic co-pilot sometimes flies right through the landmark! Kindly be seated, keep your seat in an upright position for take-off and fasten your seat belt. For those of you who can't find a seat-belt, kindly fasten your own belt to the arm of your seat. And, for those of you who can't find a seat, do not hesitate to get in touch with a stewardess who will explain how to fasten yourself on the overhead lockers." "Thanking you all for choosing Air-Tanzania to fly for the first and probably the last time."
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  We Naima wewe! so funny
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi unakaribia sasa. Nahisi HARUFU ya UFISADI. Hela za Wapambe na Takrima inabidi zitoke sehemu sehemu. Haya, waandishi na wapinzani ingieni kazini.
   
 14. M

  Mkora JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu sasa kama umesema serikali haija wapa chochote hizo pesa za kununulia hizo Dash 8- 300 na kukodi Airbus zimetoka wapi ?
  hapa naona kuna harufu ya siasa
   
 15. M

  Mkora JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  WAKUU HESHIMA MBELE HII NDIYO FLEET YA MUWEKEZAJI WA ATC
  YAANI KICHEFUCHEFU KITUPU BORA HATA SAA
  Fleet
  As of December 2007 the Sonair fleet includes:

  1 Airbus A319 (registration VP-BEY)[1]
  6 Raytheon Beech 1900D
  2 Beechcraft King Air B350
  1 Boeing 727-100F (registration D2-ESU)
  3 Boeing 727-229C (registration D2-EVD, D2-EVG, D2-FSA)
  9 De Havilland Canada DHC-6 Twin Otter Series 300
  3 Falcon 900Ex (registration D2-BEE, D2-BEF, D2-BEG)
  1 Fokker F27 Mk500
  2 Fokker 50 (registration D2-ESR, D2-ESW)
  1 McDonnell Douglas MD-11 (operated by World Airways, registration N278WA)
  On order: 1 Boeing 737-700W (registration D2-EVW) [1], Boeing 737-700QC (registration D2-EVZ) [2], 2 Airbus A319CJ, 1 Airbus A340-500

  Offshore helicopters:

  7 Eurocopter Dauphin AS 365N3
  4 Eurocopter Super Puma
  6 Sikorsky S-76C+
  On order: 4 Eurocopter Super Puma 225

  NINGESHAURI BORA WATUUZIE SHARE WATANZANIA WENYEWE I BELIEVE WE CAN DO BETTER
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Byasel,
  Ahsante kwa mchango wako, lakini inaonekana maelezo yako hayana ukweli wowote.

  Je, unataka kutuambia kuwa zile ndege mbili za Dash 8 zimenunuliwa kwa pesa gani?

  Ninakukumbusha kuwa serikali ilitoa pesa kutoka TCRA kwa ajili ya mahujaji baada ya kufanyika kwa uzembe mkubwa, hizi pia hujaziona?

  Tufahamishe ni yapi mapato hali ya ATC tangu imejiondoa kwa SAA?

  Utueleze ni jinsi gani mapato hayo yalivyotumika?
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mipango ya kibiashara ya ATC ni tatizo kubwa. hakuna ambaye anaweza kutengeneza mpango wa kibiashara ambao una-reflect hali halisi na wenye kuweza kufanya kazi.

  Unapokosea kutengeneza Business Plan ya kweli, basi utatengeneza projections ambazo haziwezi kufanya kazi kabisa.
  Makisio ya idadi ya abiria na mizigo itakayobebwa yatakuwa ni ya kupotosha.
  Resources zako za kutekeleza Business plan yako zitakuwa-wasted.

  Matokeo yake ni kuwa

  Hutaweza kupata mapato yatakayoweza kukidhi mahitaji ya matumizi

  Cash flow yako itaathirika kwa kiwango kikubwa.

  Madeni yataongezeka.

  Kwa hali hiyo basi hata kama ukipewa mabilioni ya pesa yataishia kupotea kama huna mipango sahihi ya kufanya biashara.

  Kwa mtu ambaye si mtaalam, akioneshwa hayo madudu wanayotengeneza na kuambiwa mawili matatu bila ya kujua ni nini hasa kilichopo ndani yake, hawezi kujua kama ni uozo.
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  For information board member ameamua ku resign

  ami mpungwe kaona hili so lisije likampasukia
   
 19. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Does ATC has a financial discipline to repay the loan or the government will assume responsibility once the airline default the loan? The government should have stayed out of the deal, ATC will never learn to stand on its feet as long as the government acts as if it's got ATC back no matter what. My take would have been to do away with the current top executives of ATC.
   
 20. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Date::10/3/2008
  ATCL yakwamisha abiria Wacomoro kwa siku tano Dar
  Na Salim Said

  ABIRIA 15 waliokuwa wasafiri kwenda Comoro kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), wamekwama na kuhifadhiwa kwenye hoteli ya Travertine iliyo Magomeni jijini tangu Jumatatu, wakililalamikia shirika hilo kwa kuwakwamisha jijini Dar es salaam.


  Abiria hao raia wa Comoro, Japan, Canada, Tanzania na Uingereza wamesema kitendo walichofanyiwa na ATCL si cha kibinaadamu kwa kuwa tangu wapelekwe hapo Jumatatu, hajafika hata ofisa mmoja wa shirika hilo kuwapa taarifa za safari yao, ambayo imekwama kutokana na Comoro kutokuwa na mafuta ya kujaza kwenye ndege ambayo itawapeleka huko ili iweze kurudi jijini.


  Wakizungumza na Mwananchi hotelini hapo, abiria hao walisema maisha yao yamekuwa ya shida kwa sababu hawana hata nguo za kutokana na mizigo yao kubakia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa na hawajui iko katika mazingira gani.


  Msafiri mmoja, Dk. Moh'd Ridhwan alisema hawezi kusamehe kitendo walichofanyiwa na ATCL cha kuwadanganya kama watoto wadogo kwamba ndege ilishindwa kuruka kwa sababu Uwanja wa Ndege wa Comoro hauna mafuta ya ndege, jambo ambalo alisema si la kweli.


  "Wanatudaganya kwamba Comoro hakuna mafuta ya ndege lakini ni uongo kwa sababu mimi nimepiga simu kwa rafiki yangu ambaye anafanya kazi huko na ameniambia mafuta yako ila inasemekana ATCL inadaiwa zaidi ya Euro 30 milioni (Euro moja ni sawa na Sh1,480 za Tanzania) na kampuni ya mafuta," alisema Ridhwan.


  "Mimi ni mtu mzima lakini wananifanya kama si binaadamu... leo siku ya tano sijabadili nguo. Mimi ni mfanyakazi na siku zangu za mapumziko zimeisha... nikipoteza kazi ni jukumu la Air Tanzania na siwezi kusamehe," aliongeza Ali.


  Alifafanua kwamba wameishiwa fedha hawana hata ya kupigia simu au kwenda intanet kuwapasha habari ndugu na jamaa zao kutokana na hali iliyowapata na kuongeza kuwa pengine baadhi yao wameshafanyiwa matanga kwamba wameanguka na Ndege.


  "Sisi tuko jela, Idd hatujatoka, hatujasali swala ya Idd, ndugu zetu tuliwambia tutarudi kabla ya Idd lakini hadi leo hawatupati katika simu na sisi hatuna fedha ya kuwapigia wanaweza kudhani kwamba tumekufa kwa sababu hatuna mawasiliano yoyote na wao, hotli yenyewe haina hata intanet wala simu" alisem Ali.


  Alisema ramadhani walipikiwa Futari ya Mihogo ambayo haikuwa na hata samaki au nayma jambo ambalo ni kinyume na haki za binaadamu kwa kuwa mtu anapofunga hutarajia kupata futari nzuri.


  "ATCLwamatutelekeza hapa hawaji hata kutusalimia hatuna taarifa kamili kuhusu safari yetu, tunaambiwa tu na wahudumu mara tujiandae tutakuja kuchukuliwa saa 11 jioni mara sa 2:00 usiku ilimradi hatuna taarifa kamili" alisema Ali.


  Naye Khadija Juma alisema kwa sasa wanachoomba ni kuondoka lakini tukio hilo limewaathiri sana kwani miongoni mwao ni watumishi wa umma ambao wanahitajika kazini na kwamba kuna hatari ya kufukuzwa kwa sababu hawajaenda kazini tena bila ya taarifa.


  Akizungumzia tatizo hilo, mkurugenzi mtendaji wa ATCL, Alhajji Mataka alisema hana taarifa kamili kwa kuwa alikuwa likizo na kuelekeza apigiwe meneja operesheni, Mark Manji, ambaye alisema tatizo ni uwanja wa ndege wa Comoro kutokuwa na mafuta.


  "Sina taarifa kwamba ATCL inadaiwa na kampuni ya mafuta kiasi hicho cha fedha," alisema Manji. "Ndege ambayo ilikuwa iwapeleke ni ndogo kwa hiyo haina uwezo wa kubeba mafuta ya kwenda na kurudi.


  "Lakini abiria wasiwe na wasiwasi kwa kuwa tumefanya utaratibu ili waondoke usiku wa kuamkia kesho (leo) kwa ndege kubwa ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba mafuta ya kutosha kwa safari ya kwenda na kurudi."


  Desemba mwaka jana zaidi ya mahujaji 1000 walikwama kwa zaidi siku 12 kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam kutokana na ndege ya ATCLshirika la ndege la Tanzania (ATCL) kushindwa kuruka kutokana hitilafu za kiufundi.
   
Loading...