Serikali na Hatima ya ATCL

Serikali na Hatima ya ATCL

Haya tena politiks kwenye utendaji...kazi kweli...nini tufanye kama abiria???naomba msaada wa mawazo.....maana kama wamefanya kisiasa...na kulindana....tutakaokuwa victims ni sisi kina kalagabhahoo.....
......Dawa kugomea kupanda midege yao mpaka hapo tutakapojiridhisha kuwa wametekeleza masharti yote ya IATA, wao wanaweza kulazimisha hayo madege yaruke wakijua wazi kuwa hata wao wenyewe hawatapanda siku likiporomoka wataishia kutoa pole tu wakati sisi tunapoteza watu wetu!!!!!!!!!!
 
......Dawa kugomea kupanda midege yao mpaka hapo tutakapojiridhisha kuwa wametekeleza masharti yote ya IATA, wao wanaweza kulazimisha hayo madege yaruke wakijua wazi kuwa hata wao wenyewe hawatapanda siku likiporomoka wataishia kutoa pole tu wakati sisi tunapoteza watu wetu!!!!!!!!!!

Laligeni,
Ushauri wako ni mzuri sana lakini wakati mwingine tunalazimika kupanda hizo ndege mbofumbofu za ATCL. Vinginevyo inabidi ukubali maumivu ya hawa jamaa zetu precision air.
Jamaa wanatukandamiza mno kibara!!!!kama unakumbuka wakati wa community airline(sijui walipotelea wapi), nauli zilishuka mno kiasi kwamba wamatumbi wengi waliweza kupanda ndege kama wanavyopanda mabasi ya Kilimanjaro exp, dar exp, mohamed trans, ally's clssic, buffallo coach n.k n.k.Nakumbuka nilikata tiketi ya precision air toka dar kwenda musoma kwa Tsh.211,500/- mwezi november 2007.Walipokuja hawa community air line, nilisafiri na ndege yao toka mwanza hadi dar kwa Tsh. 99,500/- mwezi january 2008!!!!Juzi juzi mwezi wa november 2008 nimekata tiketi precision air toka dar kwenda KIA, huwezi amini, nimelipa Tsh.169,000/-.Ndio sababu nahisi kuwa kama ni kufa basi ndege za ATCL zitatumaliza safari hii.!!!
Yaani sisi watanzania kila mwaka ni mwaka wa taabu tu, hakuna unafuu kwenye huduma zozote.
 
PIUS RUGONZIBWA
Daily News; Tuesday,December 30, 2008 @21:15


The Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) has given back an airline operating certificate it took away from Air Tanzania Corporation Limited (ATCL), saying the airline was broke and urgently needs at least 72 million US dollars (over 72bn/-) to keep it afloat.

Information obtained yesterday and confirmed by TCAA Director General, Mrs Magreth Munyagi, said the certificate was handed back yesterday, allowing the airline to start operating any time. ATCL was grounded following its suspension over ‘documentation problems’ by TCAA and another stop order by the International Air Transport Association (Iata) about two weeks ago.

However, the airline board chairman, Mr Mustapha Nyang’anyi, told the 'Daily News' yesterday that the airline needs at least $76 million to keep flying. Mr Nyang’anyi said the board had directed the management to hire a consultancy firm capable of putting in place new heads of all crucial departments. He cited the departments that urgently need new management as Operations, Commercial,Marketing, Sales, Public Relations, Engineering and Finance.

“These people are urgently needed to join the Chief Executive Officer to streamline the ATCL operations … and we believe there are a lot of Tanzanians who can fill these posts,”
Mr Nyang’anyi said. He pointed out that they had already approached PricewaterhouseCoopers for the job and that about 69m/- is needed for the recruitment.

He said yesterday the Board directed the management to look for funds from the government that would assist among others, paying various debts of the companies, including payment of December staff salaries. He also said they would request the government to pay salaries of the airline’s staff.

Over 300 workers of the bankrupt ATCL celebrated Christmas penniless last week and they clock in for work today demanding overdue December salaries amounting to some 400m/-. The pay demands include salaries and flying crew allowances. He confirmed that the airline’s five vehicles were held by Stanbic Bank, but saying the airline owes the bank only 40m/- and not 400/- as earlier claimed.

Five vehicles now held by the bank include Toyota Land Cruisers - SU 37079, SU 37081, SU 37082, SU 37083 and 37084 which were bought from Dubai and another three vehicles. But the only working vehicle is the Toyota Land Cruiser SU 37085 which is used by the Chief Executive Officer, Mr David Mattaka.



Ninaamini 'kukata tamaa ni dhambi', basi kama ni hivyo nisingependa kupata dhambi kwa kukaa kimya bila ya kuendelea kutoa ushauri wangu.
Ninafarijika kuona sehemu ya yale ambayo nimekuwa nikiyashauri yameanza kutekelezwa, nina imani kuwa ninahitaji kuendelea kushauri zaidi na zaidi ili nieleweke vizuri.
Hatua ya kulikwamua Shirika la Ndege la ATCL sasa hivi hazihitaji majaribio wala kubahatisha. Kama ambavyo niliwahi kushauri huko nyuma kuwa ni muhimu ATCL ikaongezewa nguvu kwenye kujenga menejimenti imara ya Airline. Kwa hivi sasa shughuli nyingi zinazofanywa na menejimenti iliyopo ziko chini ya viwango halisi vya uendeshaji shughuli za anga. Nilieleza kuwa menejimenti iliyopo haiwezi kubuni na kutengeneza mkakati wa kibiashara utakaoweza kutekelezeka. Nilisema hivyo siyo kwa sababu nina chuki na mtu yeyote katika menejimenti hiyo, la hasha, ni kutokana na ufahamu wangu juu ya uwezo binafsi wa kila mmoja wao katika aviation industry. Hata leo hii ATCL wakipewa maradufu ya pesa wanazoziomba haitasaidia kufanya ATCL iwe 'going concern', pesa zitakwenda halafu hali itajirudia ileile miaka nenda miaka rudi.
Nilishauri na nitaendelea kusimamia ushauri huu kuwa ATCL inahitaji wataalam waliobobea katika Aviation Management. Ni vema serikali ikakodisha a team toka kwenye moja ya makampuni makubwa yanayotoa huduma hizo ili utaalam ambao upo sasa hivi duniani katika uendeshaji wa shughuli za anga uweze kuwa pass over kwa watanzania ambao watawa-understudy wataalamu kwa kipindi maalum. Hii ni muhimu sana kwani kwa muda mrefu kumekuwa na gap kubwa ya kurithisha utaalam wa uendeshaji wa shughuli za anga kutoka kada moja kwenda nyingine kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ubia wa SAA na Serikali kwenye Shirika hilo, Sheria ya urekebishaji mashirika ya umma chini ya iliyokuwa PSRC nk. urithishaji wa wataalam haukufanyika kwa kasi iliyotakiwa. Wapo wataalam ambao ni wastaafu, lakini si rahisi kuwaingiza katika mazingira ya sasa hivi bila ya kuwa na exposure ya hali halisi ya shughuli za anga zinavyofanyika hivi sasa. Wataalam wastaafu wanaweza kushirikishwa kikamilifu katika maeneo mengine ya kiutelekezaji ambapo ATCL inawahitaji na kuna mapungufu.

Leo hii hakuna shughuli za utafiti ambazo zimeweza kufanywa na ATCL tangu uongozi wa Bw. David Mattaka umeanza
Leo hakuna mpango ambao umeandaliwa kitaalam wa kuiwezesha kuonyesha mwelekeo wa ATCL kibiashara na itakuwa wapi baada ya muda gani.
Leo hii hakuna bajeti ambayo imeweza kutayarishwa kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi wa Tanzania na ulimwengu kwa ujumla (japo nionaelewa kabisa kuwa hakukuwa na bajeti yeyote)
Leo hii Bodi inaomba pesa ilhali ikielewa kuwa hakuna mpango wowote wa kibiashara uliopo ATCL utakaokidhi mahitaji ya kulikwamua shirika kutoka hapo lilipo.

Mapungufu ambayo nimeyaelezea hapo juu yanahitaji angalizo la haraka kwani kama nilivyosema hapo awali kuwa hakuna muda wa majaribio kwa sasa, inahitajika team ya wataalam ambayo inazo tafiti tayari kwa kuzihuisha na hali hali ya ATCL. Ninaamini pia kuwa team ya wataalam itaonesha njia sahihi ya namna gani menejimenti inatakiwa kufanya kazi na wala sio ubabaishaji.

Juu ya kuikasimu PriceWaterHouse kufanya usaili wa nafasi za Menejimenti, mimi sioni umuhimu wowote wa ATCL kufanya hivyo kwa sasa. PWC kimsingi hawana wataalam kwenye aviation, watakachofanya ni kuchukua hiyo kazi and then wata-sub-contract team ya wataalam wa kuja kufanya kazi hiyo, na vilevile sioni kama kutakuwa na tija yeyote endapo zoezi hilo litafanyika. Ninasema hivyo kwa sababu, hata kama utaajiri menejimenti team mpya itachukua muda kwa team hiyo kuweza kufanya kazi kwa pamoja 'as a team' lakini ni rahisi kama tayari kuna team of expert ambayo ndiyo hao menejimenti team mpya inaweza kufanya kazi chini yao ili waweze kujipanga at least for 36 to 48 months. Vinginevyo sidhani kama kutakuwa na mabadiliko endelevu.
Mwisho sitakuwa nimetenda haki bila ya kuipongeza workforce ya ATCL ambayo ndiyo imekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa Shirika hilo mbali ya kukumbwa na matatizo makubwa kwa kipindi kirefu. Kada ya wafanyakazi wa kawaida wa ATCL ndiyo hazina kubwa na ya pekee iliyopo. Ninaamini kuwa kuwepo kwao na mapenzi yao na kutimiza wajibu wao ndiyo kumewajengea heshima kubwa sana mbele ya jamii. Ninawahimiza kuwa wafanyakazi wote waendelee kufanya kazi zao kwa moyo na uadilifu mkubwa kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa wakati wote, hakuna ambaye anafahamu matatizo ya ATCL kwa undani na jinsi ya kuyatatua isipokuwa ninyi wafanyakazi. Ni imani yangu kubwa kuwa kama menejimenti ingewashirikisha vema ipasavyo basi kazi ya kuliongoza shirika hilo ingelikuwa ni nyepesi sana. Nina watakia kila la kheri.
 
DAILY NEWS Reporter
Daily News; Wednesday,December 31, 2008 @20:16

Also in the News
Now two teams probe ATCL
NBAA records mass failures at exams
Dar businessman in court over bribery
Road carnage claimed thousands of lives last year
Govt move to develop TRC assets
Mwanga man held over fake notes
Rustlers kill two, steal 49 cattle in Tarime
St Mary's tops Standard Seven exams in Dar
Could I have 'a soda' please?
15 charged with leaving the country illegally

The government has formed two separate committees to probe the crisis-ridden Air Tanzania Company Limited (ATCL) and both teams have been charged with coming up with independent opinions on the future of the national carrier.

Mr Martin Ntemo, spokesman for the Ministry of Infrastructure Development, told the 'Daily News' yesterday that the committees are made up of experts appointed by the Minister, Dr Shukuru Kawambwa.

"All these committees are still working on the company's crisis and will soon submit their reports," Mr Ntemo said. If all goes as scheduled, the minister plans to hold a news conference tomorrow at which he will address ‘endless media queries' over the airline, following suspension of the airline's Air Operating Licence three weeks ago – and its return last week.

"There is so much pressure that the minister wants to address the press on Friday … let's hope this arrangement isn't interrupted," he said Meanwhile, the ATCL Board has allayed fears that the crisis could lead to retrenchment of company staff – fears generated by the workers themselves who argued that it was impossible for the company to maintain such a big number of workers without generating any income.

ATCL has more than 300 workers, with an estimated monthly pay cheque of more than 400m/-, including allowances. ATCL Board Chairman Mustapha Nyang'anyi maintained yesterday that according to the airline's strategic plans, it would in fact need more staff to meet its expanded operations – with plans to acquire more planes and spreading out to more destinations inside and outside the country.

"We are just finalizing details to restart operations and the rest will follow," Mr Nyang'anyi has been quoted to have reassured the public. He pointed out that all efforts were aimed at ensuring that three existing planes start operating once the government injects more capital.

"The five-year strategic plan projects that the company could increase its fleet of planes from five to (at least) nine, depending on the capital injection from the proprietor and the business performance. So the present workforce will be there to stay,"
he said. But he cautioned that the existing workforce could ‘be reviewed' if the government isn't now ready to put in more capital.

On Tuesday, Mr Nyang'anyi told this newspaper that the Board had directed the ATCL management to approach the government for a $76 million (92bn/-) booster fund – for the airline's survival and meet overdue December staff salaries. On December 8, TCAA suspended the airline's Operator's Certificate, in a precautionary measure it said was necessary in order to avoid possible compromise to its flight safety.

My Take:
Hivi kweli (ukiangalia maneno hayo ya bold) kweli Nyang'anyi ana uelewa wa hali halisi ya ATCL na jukumu lililoko mbele yake? Ina maana wakimpa tu bilioni 90 mpango wake ni kuongeza ndege!!
 
DAILY NEWS Reporter
Daily News; Wednesday,December 31, 2008 @20:16

Also in the News
Now two teams probe ATCL
NBAA records mass failures at exams
Dar businessman in court over bribery
Road carnage claimed thousands of lives last year
Govt move to develop TRC assets
Mwanga man held over fake notes
Rustlers kill two, steal 49 cattle in Tarime
St Mary's tops Standard Seven exams in Dar
Could I have 'a soda' please?
15 charged with leaving the country illegally

The government has formed two separate committees to probe the crisis-ridden Air Tanzania Company Limited (ATCL) and both teams have been charged with coming up with independent opinions on the future of the national carrier.

Mr Martin Ntemo, spokesman for the Ministry of Infrastructure Development, told the 'Daily News' yesterday that the committees are made up of experts appointed by the Minister, Dr Shukuru Kawambwa.

“All these committees are still working on the company’s crisis and will soon submit their reports,” Mr Ntemo said. If all goes as scheduled, the minister plans to hold a news conference tomorrow at which he will address ‘endless media queries’ over the airline, following suspension of the airline’s Air Operating Licence three weeks ago – and its return last week.

“There is so much pressure that the minister wants to address the press on Friday … let’s hope this arrangement isn’t interrupted,” he said Meanwhile, the ATCL Board has allayed fears that the crisis could lead to retrenchment of company staff – fears generated by the workers themselves who argued that it was impossible for the company to maintain such a big number of workers without generating any income.

ATCL has more than 300 workers, with an estimated monthly pay cheque of more than 400m/-, including allowances. ATCL Board Chairman Mustapha Nyang’anyi maintained yesterday that according to the airline’s strategic plans, it would in fact need more staff to meet its expanded operations – with plans to acquire more planes and spreading out to more destinations inside and outside the country.

“We are just finalizing details to restart operations and the rest will follow,” Mr Nyang’anyi has been quoted to have reassured the public. He pointed out that all efforts were aimed at ensuring that three existing planes start operating once the government injects more capital.

“The five-year strategic plan projects that the company could increase its fleet of planes from five to (at least) nine, depending on the capital injection from the proprietor and the business performance. So the present workforce will be there to stay,”
he said. But he cautioned that the existing workforce could ‘be reviewed’ if the government isn’t now ready to put in more capital.

On Tuesday, Mr Nyang’anyi told this newspaper that the Board had directed the ATCL management to approach the government for a $76 million (92bn/-) booster fund – for the airline’s survival and meet overdue December staff salaries. On December 8, TCAA suspended the airline’s Operator’s Certificate, in a precautionary measure it said was necessary in order to avoid possible compromise to its flight safety.

My Take:
Hivi kweli (ukiangalia maneno hayo ya bold) kweli Nyang'anyi ana uelewa wa hali halisi ya ATCL na jukumu lililoko mbele yake? Ina maana wakimpa tu bilioni 90 mpango wake ni kuongeza ndege!!

Inasikitisha na tena inatia simanzi kwani mazingira yanayoizunguka ATCL kwa maana ya mikakati ya kibiashara Mh Balozi hayuko kwenye picha kamili. Uendeshaji wa ATCL unahitaji watu wengine sasa hivi wenye vision tofauti. Inaniwia vigumu kuelewa hii statement ya Mwenyekiti imebeba nguvu gani ya kitaalam dhidi ya hali halisi ya ATCL leo.
 
Laligeni,
Ushauri wako ni mzuri sana lakini wakati mwingine tunalazimika kupanda hizo ndege mbofumbofu za ATCL. Vinginevyo inabidi ukubali maumivu ya hawa jamaa zetu precision air.
Jamaa wanatukandamiza mno kibara!!!!kama unakumbuka wakati wa community airline(sijui walipotelea wapi), nauli zilishuka mno kiasi kwamba wamatumbi wengi waliweza kupanda ndege kama wanavyopanda mabasi ya Kilimanjaro exp, dar exp, mohamed trans, ally's clssic, buffallo coach n.k n.k.Nakumbuka nilikata tiketi ya precision air toka dar kwenda musoma kwa Tsh.211,500/- mwezi november 2007.Walipokuja hawa community air line, nilisafiri na ndege yao toka mwanza hadi dar kwa Tsh. 99,500/- mwezi january 2008!!!!Juzi juzi mwezi wa november 2008 nimekata tiketi precision air toka dar kwenda KIA, huwezi amini, nimelipa Tsh.169,000/-.Ndio sababu nahisi kuwa kama ni kufa basi ndege za ATCL zitatumaliza safari hii.!!!
Yaani sisi watanzania kila mwaka ni mwaka wa taabu tu, hakuna unafuu kwenye huduma zozote.

Tayarisha lawyer wako tu ili kikitokea kitu chochote uweze kuwashtaki serikali, ATCL na TCA kwa kukuletea madhara kwa uzembe wao na ukaidi.
Na kuhakikisha mahakama inawafungia mpaka wameruhusiwa na vyombo vyote vilivyoifungia. Hao wanasiasa ni wangapi wanapanda ATCL?

Safety should be their TOP priority.
 
Laligeni,
Ushauri wako ni mzuri sana lakini wakati mwingine tunalazimika kupanda hizo ndege mbofumbofu za ATCL. Vinginevyo inabidi ukubali maumivu ya hawa jamaa zetu precision air.
Jamaa wanatukandamiza mno kibara!!!!kama unakumbuka wakati wa community airline(sijui walipotelea wapi), nauli zilishuka mno kiasi kwamba wamatumbi wengi waliweza kupanda ndege kama wanavyopanda mabasi ya Kilimanjaro exp, dar exp, mohamed trans, ally's clssic, buffallo coach n.k n.k.Nakumbuka nilikata tiketi ya precision air toka dar kwenda musoma kwa Tsh.211,500/- mwezi november 2007.Walipokuja hawa community air line, nilisafiri na ndege yao toka mwanza hadi dar kwa Tsh. 99,500/- mwezi january 2008!!!!Juzi juzi mwezi wa november 2008 nimekata tiketi precision air toka dar kwenda KIA, huwezi amini, nimelipa Tsh.169,000/-.Ndio sababu nahisi kuwa kama ni kufa basi ndege za ATCL zitatumaliza safari hii.!!!
Yaani sisi watanzania kila mwaka ni mwaka wa taabu tu, hakuna unafuu kwenye huduma zozote.

Kwani sasa hivi wamapanda ndege gani? Na bei zikoje?
 
......Dawa kugomea kupanda midege yao mpaka hapo tutakapojiridhisha kuwa wametekeleza masharti yote ya IATA, wao wanaweza kulazimisha hayo madege yaruke wakijua wazi kuwa hata wao wenyewe hawatapanda siku likiporomoka wataishia kutoa pole tu wakati sisi tunapoteza watu wetu!!!!!!!!!!

Wamepewa hiyo certificate lakini hakuna ndege yao itakayoruka. Hili shirika ni muffilisi na kila mtu anafahamu hivyo lakini wanaogopa kutangaza tu. Last week, wakati serikali ilipojifanya kuwabana akina Nyang'anyi, huyu mzee alikuwa anaishawishi bodiw atangaze kuwa shirika ni muflisi lakini akapigwa mkwara na serikali kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kuathiri jitihada za ualaji za kusaka mwekezaji
 
Kuna masihara lakini ktk kifo ebu tuepuke masihara.Kuruhusu ndege uku ATCL ikiwa imefungiwa haiingii akilini naona kifuatacho ni hawa TCAA kufungiwa na hao IATA kama inawezekana bse ninachoona hapo ni usanii mtupu.
Kama uendako kuna altenative ya ndege ingine ni kheri upande iyo altenative kama hamna anyway mwachie mungu.
Ni lini tutakuwa seriuos!Ingawa iyo haina tofauti na uingizwaji wa dawa feki na watz wakaambulia CANCER na mengineyo ila hii ya sasa ni kifo.
Ushauri wangu hao ATC waendelee kufungiwa mpaka masharti yatimizwe na ndege nazo pia bse bila ndege ATC haipo bse wao ndo wanazioperate.
 
ATCL yapata mbeleko serikalini
Gloria Tesha
Daily News; Friday,January 02, 2009 @20:15

Serikali imetoa Sh bilioni 2.5 kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ikiwa ni fedha za awali za kuendesha kampuni hiyo na kulipa baadhi ya madeni kati ya Sh bilioni 3.3 zilizoombwa na kampuni hiyo kama mtaji wa haraka.

Sambamba na hilo, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa ameunda Tume na kuitaka ifanye kazi kwa siku 21 tangu Desemba 29, mwaka jana ili kubainisha kiini cha matatizo ya ATCL baada ya ripoti ya Bodi ya kampuni hiyo kutotoa maelezo ya kutosheleza.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ya watu saba ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrissa Mshoro na wajumbe wengine sita, alisema Dk. Kawambwa. Kuhusu mtaji huo wa Sh bilioni 2.5, Dk. Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa serikali imeamua kuibeba ATCL kuanzia mtaji mpaka ulipaji wa madeni kwa kuwa ni mmiliki wa kampuni hiyo na kwamba itatoa fedha kwa awamu kulingana na mahitaji ya wakati ya kampuni hiyo.

Alisema hapo awali wakati mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini unakufa, kulikuwa na deni la takribani Sh bilioni 30 ambazo ni pamoja na Sh bilioni 9.1 za watoa huduma kama ya mafuta ambao ni BP na wasambazaji wa chakula, Sh bilioni saba za uendeshaji na Sh bilioni 17.5 zilizotolewa na serikali kama mkopo.

Alisema deni lingine ni dola za Marekani milioni 4.2 sawa na Sh milioni 5.04 linalodaiwa na SAA ambapo pamoja na kuibeba kampuni hiyo alisisitiza kuwa waliohusika kuihujumu watashughulikiwa ipasavyo, tena mapema.

Alikiri kuwapo matatizo ya utaalamu mdogo katika menejimenti yanayosababisha utendaji mbovu na kusema ni mapema kuchukua uamuzi wa kisiasa kumwajibisha mtu, lakini aliahidi kufanya mkutano karibuni na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL, Balozi Mustafa Nyang’anyi ili kumpa mwongozo wa namna ya kuchukua hatua za nidhamu kwa waliohusika kuhujumu kampuni.

“Wale ambao watakuwa juu ya uwezo wa Bodi kuwajibishwa, basi Mwenyekiti atapeleka mapendekezo kwa mamlaka ya juu inayohusika ili wawajibishwe na kamwe hatutasita kuchukua hatua zaidi ya hapo kama za kisheria na nyingine kwa wahusika pale itakapobidi,” alisema.

Alisema mbali na madeni hayo ambayo yataendelea kulipwa kwa awamu kulingana na fedha, deni la Sh bilioni 17.5 serikali imelifanya kama mtaji tena kwa kampuni hiyo na pia serikali itatoa Sh milioni 320 kulipa mishahara ya Desemba mwaka jana ya wafanyakazi 300 ambao mpaka leo haijalipwa.

Kuhusu mtaji wa Sh bilioni 91.2 ambao ATCL uliiomba serikali awali, alisema hana kauli kuhusu mtaji huo, lakini alisisitiza kuwa tangu kampuni hiyo iombe mtaji, imenunua ndege mbili aina ya Bombadia, DASH8-Q300 na kukodisha moja, Air Bus 320 kwa gharama za dola za Marekani 370,000 kwa mwezi (Sh milioni 444).

“Lengo ni kuona kampuni yetu inasimama na ndege zinaruka tena, siku za baadaye kuna mpango wa uwekezaji wa mabilioni ya shilingi kwa kununua ndege nyingine, kukodi na kununua vifaa pamoja na kufanya mafunzo…kwa hivyo utaona fedha hizo ni za mahitaji ya dharura ya sasa,” alifafanua Dk. Kawambwa.

Alisema katika hatua hizo zilizochukuliwa na serikali bado mazungumzo yanaendelea baina yake na mwekezaji wa China, ingawa hakuwa tayari kumtaja ila alisema yatakapofikia hatua ya kuridhisha wataweka suala hilo wazi.

Kuhusu ripoti iliyosababisha kuundwa Tume hiyo, alisema kuna mkanganyiko wa maelezo katika taarifa hiyo na mambo kadhaa hajapatiwa majibu hivyo Tume hiyo inapaswa kufuata hadidu tatu za rejea alizozitaja kuwa ni; kubainisha matatizo ya ATCL kitaalamu na kwa kina, kubainisha chanzo chake na kutoa mapendekezo ya mkakati wa kuyatatua na kuhakikisha hayajitokezi wakati mwingine.

Aliwataja wajumbe wengine na wanakotokea katika mabano kuwa ni Dk. Marcellina Chijoriga (Mwenyekiti, Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Profesa Ibrahim Juma (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Dk. Gideon Kaunda (Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo-TCCIA), Mtesigwa Maugo (Shirika la Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga Afrika Mashariki – CASSOA), Dk. Mussa Assad (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Dk. Hamisi Kibola (Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania-UTT).

Wiki tatu zilizopita Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) iliinyang’anya leseni ATCL kutokana na dosari za kukidhi viwango na kanuni za kiufundi na usalama wa anga. Ilirejeshewa Jumanne wiki hii.

Katika hatua nyingine, serikali imeunda Kamati ya kupitia upya mkataba baina yake na kampuni yenye ubia katika usafiri wa reli ya Rites kutoka India ili kuangalia namna ya kufanya mabadiliko katika Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) baada ya kubainisha kasoro zilizopo katika mkataba huo.

Dk. Kawambwa alisema tayari kikao cha kwanza kimefanyika Novemba mwaka jana na cha pili kinatarajiwa kufanyika siku yoyote katika mwezi huu; lengo ni kuleta uwiano wa kiutendaji katika ngazi mbalimbali za kampuni hiyo kutokana na sasa kuonekana kuwa nafasi kubwa nyingi zinashikwa na wabia wa Rites zaidi.
 
Govt moves to bail out ATCL
PIUS RUGONZIBWA
Daily News; Friday,January 02, 2009 @20:15​

The government has injected 2.5bn/- into the crisis-ridden Air Tanzania Company Limited (ATCL) and formed a task force to thoroughly look into the company’s problems and advise on measures to rescue it.

The Minister for Infrastructure Development, Dr Shukuru Kawambwa, said yesterday that the government would gradually inject more funds to ATCL after being satisfied that it can run commercially.

ATCL management earlier submitted application worth 3.3bn/-to put it back on track. But the Company’s Board Chairman, Mr Mustapha Nyang’anyi, has been quoted as saying about 92bn/- was needed to revamp operations of ATCL. The Minister said the ATCL workers would have to be patient, as the government was looking for other sources of funds to pay their December salaries amounting to 320m/-.

Dr Kawambwa, however, admitted that there were serious technical problems within ATCL. He said the task force which started its duty from December 29, last year, was required to submit its report within 21 days. Terms of reference of the task force include: establishing causes of ATCL problems and recommending possible technical and financial solutions, according to the minister.

Members of the task force are Prof Idrissa Mshoro from Ardhi University who will chair the team. Others are Dr Marcellina Chijoriga, Prof Ibrahim Juma, Dr Gideon Kaunda, Mr Mtesigwa Maugo, Dr Mussa Assad and Dr Hamis Kibola. On the initial investigation, whose report was recently submitted by the ATCL Board on reasons for the current situation, the Minister said he was not happy with the report.

According to him, the report lacked many facts on the real cause of the problems at ATCL, to the extent of the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), had to suspend its operations due to technical faults. TCAA suspended ATCL licence on December 8, last year, following directives from the International Air Transport Associations (IATA), after the national flag carrier had failed to observe IATA requirements.

“I must be clear that the government is going to spare nobody on this. I have directed the Board to hold accountable all responsible officials who contributed to the suspension of the company’s air operating licence,” said Dr Kawambwa. He explained that the government was looking for ways to put more capital to ATCL, the company was also overstaffed comparing to the number of aircraft it was currently operating.

With three planes, the company is reported to have more than 300 staff. On ATCL’s debts, Dr Kawambwa said it owes South African Airways (SAA) $4.2m, various service providers and suppliers 9.1bn/- and the government about 17.5bn/-. But he explained that the government’s debts had been transferred as capital of the company.

Meanwhile, the government has decided to review the management contract of Tanzania Railways Ltd (TRL), with India’s investor Rites that was signed last year. The Minister of Infrastructure Development, Dr Shukuru Kawambwa, told reporters yesterday that anytime this month Rites top management would be in the country for discussions on the contract.

He said one of the issues to be discussed was the need of a joint management of TRL which is currently run by 100 per cent by officials from Rites. The government owns 49 per cent shares in the TRL, while Rites owns the rest 51 per cent.

Copyright @TSN 2007 All Rights Reserved
 
JK anataka kujinasua na uswahiba anataka apate report toka task force ili aujue nini cha kufanya...ila uswahiba utaua nchi ok ngoja tusubiri hadi 21 days tusikie next episode
 
Nimesoma habari zinazoonesha jitihada za serikali za kuifanya ATCL iweze kurudi tena katika shughuli zake za biashara ya anga. Mimi binafsi ninaipongeza kwa hatua ambazo imeshazichukua kuhakikisha shirika hilo linasimama tena.

Lakini hata hivyo ninaishauri serikali katika muda huu ambao inafanya michakato mbalimbali ikiwemo ya kupata taarifa ya tume maalum iliyoundwa na Mh. Waziri, ingekuwa ni vema serikali pia ikaunda menejimenti ya muda itakayosimamia shughuli za ATCL pending hiyo ripoti na maamuzi ya serikali. Sababu ya kusema hivi ni kwamba zoezi zima la nia njema ya serikali kuisaidia ATCL litaingia dosari endapo uchunguzi unafanyika wakati menejimenti ikiwa imo ndani. Ni vema menejimenti ipewe likizo ili serikali iweze kufanya kazi yake kwa ukamilifu. Sasa hivi menejimenti ya ATCL inafanya juhudi mbalimbali za kujinasua kutokana na kashfa ya kufungiwa kurusha ndege kwa gharama yeyote. Ni wasiwasi wangu kuwa kunawezekana kutokea upotoshwaji mkubwa wa taarifa mbalimbali kwa malengo ya kujihami.

Pili, ninasisitiza kuwe na uongozi wa muda kwa sababu u-tatu wa ATCL yaani Bodi-Menejimenti-Wafanyakazi kwa sasa hivi haufungamani. Nina hakika Mh. Waziri anazo taarifa rasmi juu ya jambo hili kwani taarifa zilizopatikana kupitia vyombo vya habari zilieleza wazi kuwa Wafanyakazi hawana imani na menejimenti na bodi ya wakurugenzi. Pia taarifa zinaonesha kuwa Mh. Waziri baadae alikutana na viongozi wa wafanyakazi, kwa hiyo basi ninauhakika kuwa alielezwa na kuelewa kuwa utatu wa ATCL haupo, sasa, kitendo cha kuiagiza bodi iwashughulikie wanaoihujumu ATCL huenda kinaweza kutoa mwanya kwa lile kundi lenye mamlaka ya kuwashughulikia wengine kulipiza kisasi. Na jambo hili ninavyoliona mimi linaweza kutokea wakati wowote kwani haitakuwa mara ya kwanza kwa kundi lenye mamlaka kufanya hivyo.

Mwisho, kwa vile nimeona majina ya wajumbe kwenye kamati aliyoiteua Mh. Waziri, si vibaya kutoa angalizo linalomhusu mmjoa kati ya wajumbe hao.
Gideon Kahunda (ama kama ambavyo anapenda kujiita mwenye Gideon Kaunda). Huyu ndugu anahusika sana katika mikakati mingi iliyopangwa na SAA kuidhoofisha ATC. Aliwahi kuwa mjumbe katika bodi ya Air Tanzania wakati wa Mungai akiwa Mwenyekiti. Bodi ile ndiyo iliyobariki pamoja na mambo mengine uanzishwaji wa Alliance Air ili baadae ichukue nafasi ya ATC kinyemela. Gideon Kahunda akiwa pia ni mshauri wa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi katika masuala ya anga, alitumia nafasi yake vibaya kwa kufanya lobbyings mbalimbali ndani ya serikali kwa manufaa ya Alliance Air. Vile kwa nafasi ambayo haijulikani ndani ya Alliance Air na wakati huohuo akiwa mjumbe wa bodi ya ATC alikuwa akionekana wazi hadharani kama msemaji wa Alliance Air ilhali akiwa ni mtumishi wa serikali - mshauri wa Waziri. Kwa jinsi ninavyomfahamu Kahunda, atajaribu kuteka hiyo kamati ili ikiwezekana apate big role to play na hatimaye kuwashawishi wajumbe wengiine (ambao mimi ninaona ni watu ambao wanashughuli nyingi katika kazi zao za kila siku) wakubaliane na mawazo yake. Kwa vile mkakati wa SAA juu hatimaye ATCL haujafutika, Kahunda kama lobbist mzoefu anaweza kutumia nafasi hii kuwasiliana na his SAA allies wakapenyeza yale ambayo yana weza ku-influence kamati iliyoundwa ya 'ma-dokta'
Ninawasilisha
 
Govt moves to bail out ATCL
PIUS RUGONZIBWA
Daily News; Friday,January 02, 2009 @20:15​

The government has injected 2.5bn/- into the crisis-ridden Air Tanzania Company Limited (ATCL) and formed a task force to thoroughly look into the company’s problems and advise on measures to rescue it.
.......

With three planes, the company is reported to have more than 300 staff. On ATCL’s debts, Dr Kawambwa said it owes South African Airways (SAA) $4.2m, various service providers and suppliers 9.1bn/- and the government about 17.5bn/-. But he explained that the government’s debts had been transferred as capital of the company.

Meanwhile, the government has decided to review the management contract of Tanzania Railways Ltd (TRL), with India’s investor Rites that was signed last year. The Minister of Infrastructure Development, Dr Shukuru Kawambwa, told reporters yesterday that anytime this month Rites top management would be in the country for discussions on the contract.

He said one of the issues to be discussed was the need of a joint management of TRL which is currently run by 100 per cent by officials from Rites. The government owns 49 per cent shares in the TRL, while Rites owns the rest 51 per cent.

Copyright @TSN 2007 All Rights Reserved

Hawa wanajaribu kujaza maji kwenye gunia.
 
Habari zilizonofikia hivi punde huku ugahaibuni ni kwamba bodi ya kampuni ya atcl ikishirikiana na management yake wameamua
kuwaadhibu wafanyakazi wote kwa kuwaandika na kuwachafua kwenye magazeti na hivyo kuamuru wafanmyakazi wote kwenda likizo bila malipo mpaka hapo hali itakapo tengemaa
chanzo chetu cha habari kutoka kwa mhandishi wetu L.BAHATI
kimesema mkurugenzi wa kampuni ya atcl bwa David mattaka alikuwa akitarajia kukaa na chama cha wafanyakzai leo hii jumamosi mchana kuwatangazia uamuzi huo wa gafla kutokana na jazba za kisiasa.katika mkutano huo ambao ungekaa na kuongelea mambo mbalimbali mwandishi wetu ametuabahalisha kuna mambo mbali mbali yatazuka likiwamo kutaka kuwarudisha wale tu ambao wameona wanafaa kwa kampuni na kuwatimulia mbali wale ambao wanahisi kwa namna moja ama nyingine kushiriki kuwapaka matope na kushindwa kulinda kitumbua chao.....
katika kuhalalisha hili mkurugenzi ameoa akutane na chama cha wafanyakazi kuona jinsi gani atafanikiwa katika zoezi lao hili ambalo nina hakika ama uhalali kwamba litawasha moto ambao bw mattaka ajawahi kuuona katika maisha yake yote ya uongozi ....
wakati serikali imetangaza kutoa hela kwa ajili ya ATCL...kuna baadhi ya wakurugenzi wameshangilia na wengine kuapa kwamba hakuna atakaeondoka kwa maana serikali aishi kwa niaba ya magazeti....katika kujiakikishia hilo mmoja wa mameneja walioko kwenye uongozi huo amesema na kuwaapia wenzake atakuwa wa mwisho kuresign ,,mimi siwezi kujiuzulu kirahisi hivyo.......
ushauri wa jf wa bure kwa hao wanaoojiita atcl task force

1))tunaomba mjue lolote mtakalofanya na kutoa kwa mh waziri ni kwa ajili ya watanzania wote..hivyo kama kuna mchezo mchafu unaojulikana kwa menejiment nying za tanzania kuhonga wale wanaowachunguza mjue dhmbai ya watanzania haitowaacha

2))Mkiwa mnajiandaa kuanza kwa kazi hiyo ni vyema na busara kukutaana na wafanyakazi wa ATCL kwanza ambao kwa mujibu wa sheria walikaa na kuamua hawaiitaji bodi ya ATCL na menejiment yake..ambayo waziri amekuwa akiilea na kuibeba bila hata kubebeka
na hivyo kuwasaidia kuwa na njia rahisi zaidi badala ya kufika siku 21 na kutuambia chache ...hazikutosha huku watanzania wakiteseka kutafuta usafiri wa anga wenye uhakika

3)Baada ya kukutana na wafanyakazi ni ushauri wa bure kutana na chama cha wafanyakazi...huku nje hivi vyama vinaheshimika na kuabudiwa wacha mtu akitaka kufukuzwa kazi pia hata kwenye masilahi ya wafanyakazi kifwedha na mengineyo...wakiamua hakuna kwenda kazini watu awaendi ,,hivyo hawa watu tuliowasaidia kuwatajia ndio wanaojua matatizo halisi ya atcl ...

4))Nawashauri katika huu muda msitumie muda mwingi kuongea na bodi na menejiment ambayo inajipanga kukaa sawa ili wasiondoke kwa gharama zozote ama kwa kuwahonga .....tunajua lazima muwasiliane nao ila jaribuni kukaa na hawa watu EX- ATCL CEO

MR EMANUEL KIMARO

MR CHIZI

Na wengine wengi waliopita atcl wanajua mambo mengi tu ambayo yatawasaidia badala ya kukalishwa na kupewa kahawa kempinsiki wmijitahidi kukaa na wadau wanaoijua atcl...

5))Kuna madhambi mengi tu na yenye ushaidi msitumie njia ya kuwatishia watu wameopata wapi docs nk...la maana jitahidini kujua chanzo cha uchafu mtakachoelezwa ni nini na kumwambi mh raisi wapi hii kampuni inaelekea


6)) Baada ya kumaliza kazi yenu nzuri ambayo hmjaanza nafikiri ningewapongeza kwa kuchaguliwa kuisaidia kampuni hii ambayo inakaribia kufa....
USHAURI WA JF BAADA YA KUPEWA USHAHIDI NA UFUJAJI WA PESA WOTE ULIOFANYWA NA MENEJIMENT HII TAFADHALINI MWISHO WA MAONI YENU MMALIZIE

.........TUNAOMBA MENEJIMENT NZIMA IFIKISHWE MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO KUJIBU TUHUMUZA ZINZOWAKABILI NA KURUDISHA MALI ZOTE WALIZOTUMIA ZA KAMPUNI......
 
Last edited by a moderator:
Mod tunaomba ikae kwa muda na rasi wetu aweze kujua wapi atcl inaelekea
 
Hehehehe Tanzania eeeee Nchi yangu eeee Nakupenda zaiiidi Watu wote wajua.. Kuna mabonde na milimaaa ndege nao Wanyamaaaaaa....... Hakika Tanzania nakupenda
 
labda hapo wanaongezewa likizo, manake malipo hata mwezi wa 12 hawakulipwa.
 
Waziri akataa ripoti ya ATCL

2009-01-03 12:03:28
Na Joseph Mwendapole​

Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, ameiponda ripoti ya Bodi ya Shirika la Ndege Nchini (ATCL) iliyowasilishwa kwake, kuwa haina maelezo ya kutosha kuhusu matatizo ya shirika.

Badala yake, ameunda kamati ya watu sita kuchunguza kiini cha matatizo yaliyoliyumbisha shirika hilo.

Kadhalika, amesema Shirika hilo limerejeshewa leseni yake ya biashara baada ya kutimiza vigezo vilivyotakiwa na Mamlaka ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO) na ndege zake zitaanza safari wakati wowote.

Akizungumza na Anga (ICAO) na ndege zake zitaanza safari wakati wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk. Kawambwa ambaye pia alikiri kuwa menejimenti ya shirika hilo ina kasoro, alisema ripoti hiyo imemwachia maswali mengi yasiyo na majibu.

Waziri alisema kuna mambo mengi ambayo anahitaji kuyafahamu, lakini hayakuainishwa kwenye ripoti hiyo ambayo alisema ilikuwa na kurasa chache.

Kamati hiyo ilianza kazi Desemba 29 mwaka jana na ameipa siku 21 kukamilisha kazi yake.

Alisema endapo kamati hiyo itamshauri kuvunja menejimenti ya shirika hilo hatasita kufanya hivyo.
Wakati huo huo, alisema tayari ameiagiza menejimenti kuwachukulia hatua za kinidhamu wale waliohusika kulifikisha shirika hapo lilipo.

Aidha, alisema endapo menejimenti itatoa adhabu kwa watumishi wa shirika ambayo hataridhika nayo atawashughulikia yeye mwenyewe.

Aidha, Dk. Kawambwa alisema hadidu za rejea za kamati hiyo inayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrisa Mshoro, ni kujua kwa kina matatizo ya shirika, vyanzo muhimu vya matatizo na baada ya hapo ipendekeze mikakati na hatua za kuchukua kulifanya shirika hilo lijiendeshe bila matatizo.

Alisema awali isingekuwa rahisi kuwashughulikia watu waliohusika na uzembe kwa kuwa ingekuwa vigumu kwa shirika hilo kurekebisha kasoro zilizopo ili kurejeshewa leseni tayari kwa kuendelea na biashara.

``Tungewawajibisha watu waliozembea kabla hatujarudishiwa leseni hivi hizo kasoro angerekebisha nani, tulipokaa kimya maana yetu ilikuwa tuweke mambo sawa kwanza, lakini sasa tunaweza kuwajibishana kwa kuwa leseni tayari tunayo,`` alisema.


Alisema ili shirika hilo liweze kuanza biashara linahitaji Sh. bilioni 3.3 na tayari serikali imeshalipatia Sh. bilioni 2.5 na kwamba linadaiwa zaidi ya Sh. bilioni 9.1 na wadau wanaolipatia huduma mbalimbali.

Alisema serikali italipa mishahara kwa wafanyakazi wote inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 320 ikiwa ni hatua ya kulinusuru ili liendelee kufanya biashara.

Alisema serikali itaendelea kuliwezesha shirika hilo kifedha na kuliongezea ndege ili kukidhi mahitaji yaliyopo.

Dk. Kawambwa alisema tayari serikali inafanya mazungumzo na shirika moja la China ili kuangalia uwezekano wa kuingia ubia na ATCL.

Alisema safari hii serikali itakuwa makini zaidi ili isije ikaingia ubia na shirika la kibabaishaji na hatimaye kupata hasara kama ilivyokuwa kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).

Alisema ATCL inapaswa kujipanga upya ili ndege hizo zianze safari zake kama kawaida na idumishe viwango vya kimataifa ili isije ikapokonywa leseni ya biashara tena.

Alisema ATCL ina ndege mbili tu, lakini wafanyakazi 300 na alisema endapo itabainika wafanyakazi ni mzigo kwa shirika watapunguzwa.

Alisema ndege hizo zinazofanya kazi kati ya Mwanza na Mtwara zina uwezo wa kuchukua abiria 50 kila moja, na ndege moja ya kukodi Air Bus A320 ina uwezo wa kuchukua watu 150.

Wajumbe wa kamati hiyo ni Marcelina Chijoriga, Dk. Ibrahim Juma, Mussa Assad, Dk. Gideon Kaunda, Dk. Hamis Kibola na R. Mango.

Mkurugenzi Mtendaji wa (ATCL), David Mattaka alisema hivi karibuni kuwa shirika hilo limesimama kutoa huduma kutokana na kunyang\'anywa leseni na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kutokana na mapungufu mengi ya kiutendaji.

Alisema ukaguzi uliofanywa na taasisi ya Ukaguzi ya Kimataifa ya Usalama wa Anga IOSA Desemba mwaka jana ulibaini mapungufu 482 ya viwango, kwa mujibu wa Mamlaka ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO).

Alisema mapungufu hayo yalibainika katika idara za oganaizesheni na utawala, miruko ya angani, usafiri, matengenezo, cabin, huduma za ardhini, mizigo na usalama.

Mattaka alisema kasoro hizo hazikuwa kubwa kiasi cha kuweza kuathiri usalama wa ndege na abiria.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom